Sunday, November 25, 2012

EXCLUSIVE INTERVIEW WITH REDDS MISS TANZANIA TOP MODEL 2012 (MAGDALENA ROY). Miongoni mwa Warembo Waliokuwa kwenye ushindani mkubwa kwenye mashindano ya mwaka huu ya Miss Tanzania ni Magdalena Roy. Huyu Ni Miongoni mwa warembo walioleta ushindani mkubwa kwenye mashindano yale na hasa ikizingatiwa kuwa tayari alishakuwa mshindi kwenye kinyang'anyiro cha Redds Miss Tanzania Top Model na kupata nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye nusu fainali ya mashindano yale. Nimepata nafasi ya kufanya naye interview Mrembo huyu ambaye pia ni Super Model Na Pia Ni Video Vixen kuweza kufahamu mengi kumhusu na alikuwa na haya ya kusema; 1 . Nini kilikufanya Ufikirie Kuwa model na ulianza lini? Maggie; nimeanza kujishughulisha na mambo ya fashion kwa ujumla mwaka jana mwezi wa sita na ni kwa sababu ilikuwa kwenye damu yangu tangu zamani na ndio maana sikuona tabu sana kuacha kazi yangu niliyosomea ( Civil Engineering) na kuingia huku kwenye mambo ya fashions pamoja na wengi wa watu kuwa na mtazamo hasi kuwa kazi hii ni uhuni lakini ninaamini nimefanya uamuzi sahihi. 2. Unakumbuka kazi yako ya kwanza kufanya ilikuwa ipi? Maggie; Kazi yangu ya kwanza ilikuwa ni Dar Fashion Festival ambayo hufanyika kila mwaka na nilipata experience ya kutosha sana na nilikutana na designers wengi ambao walionyesha moyo wa kufanya kazi na mie. Baada ya hapo nikaja kufanya kazi Ya Photoshoot kwenye kampuni za Susneakers Inc Na Pedama Communications Agency Chini Ya Fashion Photographer, Eric Shio Na Mkurugenzi Wa Pedama, Mr. David Ndaiga. Kilichofuata baada ya hapo ni mafanikio zaidi. 3. Unaionaje Tasnia Ya Fashion Kwa Ujumla Hapa Tanzania? Maggie; Kwa navyoona tasnia ya fashion kwa hapa tanzania inakua tena kwa kasi, models wanaongezeka na Young designers wanakuja kwa kasi sana na hata malipo kwa sasa at least sio mabaya sana hasa nikizungumzia kwa upande wangu. 4. Umewahi kushiriki mashindano makubwa kama Miss Dar City Center, Miss Ilala Na Hatimaye Miss Tanzania, Umejifunza nini na unawashauri nini wanaotamani kuingia kwenye sekta hii? Maggie; Ni Kweli nimejifunza mengi sana na hasa jinsi ya kuishi na watu tofauti, kuwa na uvumilivu na cha muhimu zaidi msimamo kwenye maisha, nawashauri wanaotaka kuingia humu wawe na effort ya kutosha, when you real need something then go fot it, dont hesitate and have faith. usisikilize watu wanasema nini bali jiamini na usonge mbele. 5. Miss Tanzania ndo hiyo imeisha na umefanikiwa kuwa Redds Miss Tanzania Top Model, Nini matarajio yako ya baadae? Maggie; Ni kweli nimepanga kuwa kuwa role model kwa wanaochipukia na kuwajengea msingi imara wengine wanaotaka kufika mbali so nitajitahidi kwa khali na mali kuwa international model na kuwa mwanga bora kwa wote wanaotaka kufika mbali. 6. Nani ni role model wako na kwanini?? Maggie; Flaviana Matata ni role model wangu kwa sababu ana juhudi na ninaamini nitafika kuwa kama yeye, hajawahi kuni-dissapoint hata siku moja. 7. Siku za hivi karibuni kumezuka taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa wewe ni LESBIAN na ulitangaza hivyo, Je Ni Kweli Au Lah??? Maggie; Habari Hizo Hazina Ukweli Wowote na ni kwamba ilitokea tu siku moja simu yangu iliibiwa tulipokuwa kwenye event na aliyeiba nadhani alikuwa ananifahamu na sikuwa nimeweka security code hivyo akatumia nafasi hiyo kuweza kuandika hivyo kwenye Facebook Na BBM kwa nia ya kuniharibia kwa sababu nilishakuwa kwenye mashindano. 8. Kwa wasiokufahamu unaweza kuwaeleza ulipotoka na hadi ulipo sasa kihistoria zaidi? Maggie; Nimezaliwa mwaka 1991 nikiwa ni first born kwa familia yetu na nimesoma shule ya msingi Leganga, Usa-River na sekondari nimesoma Ailanga Seminary iliyopo hifadhi ya taifa ya arusha na baada ya hapo nikajiunga na Arusha Technical College kusomea Civil and Highway Engineering kwa miaka mitatu na baada ya hapo nikaingia kwenye mashindano ya Miss Universe 2011 ambapo nilifanikiwa kuwemo kwenye tano bora na baada ya hapo nikapata nafasi ya kufanya training pale Qatar Airways kwa miezi 3 na baada ya pale ndo kama unavyoona nimefika hapa nilipo leo. 9. Ukipewa nafasi ya kushukuru watu 5 utawashukuru nani na nani?? Maggie; Kwanza ni Mungu kwa kunifikisha nilipo leo, Pili ni Familia Yangu Yote Kuanzia Baba, Mama, Aunty Neema Na Wengineo, Tatu ni marafiki wote, nne ni Manager Wangu Mr. Martin na Endless Fame Management na mwisho ni Fans wangu wote. 10. Ni Swali gani hujawahi kuulizwa na ungependa siku moja uulizwe, na jibu lake ni lipi? Maggie; ha ha ha ha labda Hobbies zangu, napenda sana music na hasa ya Rihana, Ciara, Nicole, Beyonce,etc. pia mazoezi ya viungo na michezo mbalimbali na pia movies hasa horror movies and series. Posted by David Ndaiga at 12:08:00 PM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook Reactions: Friday, November 16, 2012 DHAMBI HIZI 2 HUTASAMEHEWA; Dhambi zote Mungu anasamehe isipokuwa mbili... Je unazifahamu? Ninamshukuru Mungu kwa kunipa wasaa huu wa kuongea neno lake hapa. Leo ningependa tuongelee dhambi, wote tunajua Mungu anasamehe dhambi unapomwomba msamaha..., Lakini je tunafahamu kuwa kuna dhambi mbili ambazo Mungu hasamehe? Kama ulikuwa haufahamu basi ni vyema leo ukazifahamu ili kuhakikisha unajiepusha na dhambi hizo. - Dhambi ya kwanza ni ya kumkashifu roho mtakatifu. Katika biblia takatifu tunaiona kwenye kitabu cha Mathayo mtakatifu 12: 31-32. Neno la Mungu linasema....... .......12:31 Kwa sababu hiyo, nawaambieni, watu watasamehewa dhambi na kufuru zao zote, lakini hawatasamehewa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. 12:32 Tena, asemaye neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa, lakini yule asemaye neno la kumpinga Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao. Dhambi ya pili ni kutokusamehe. Hii tunaipata katika kitabu cha Mathayo Mtakatifu 6:14-15, neno la Mungu linasema...... ..........6:14 Kwa kuwa kama mkiwasamehe watu wengine wanapowakosea, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe pia na ninyi. 6:15 Lakini msipowasamehe watu wengine makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. Hivyo basi wandugu ni vyema tukajiweka wasafi mbele za Mungu kila wakati, ili siku ya hukumu tusijejikuta tunahukumiwa kwa dhambi ambazo zinaepukika. Posted by David Ndaiga at 5:30:00 PM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook Reactions: Monday, November 5, 2012 New Hit In Town '' Oweoo'' -- J4C Wengi Walimfahamu kwa mara ya kwanza alipotoka na wimbo wake ulioitwa ''Fimbo Ya Mbali'' akimshirikisha Mkali Q-Jay. Jina lake kimuziki anaitwa J4C na kwa mara nyingine tena amerudi akiwa na 'Club Banger' Matata sana safari hii na kazi imefanyika pale Arusha katika studio za NoizMekah na wimbo unaitwa ''Oweoo''. Listen/Download Here; Oweoo -- J4C Posted by David Ndaiga at 3:58:00 PM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook Reactions: Tuesday, October 30, 2012 '' Nataka Kulewa '' -- Diamond Sikiliza ''Nataka Kulewa '' By Diamond Hapa; Posted by David Ndaiga at 6:58:00 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook Reactions: Saturday, October 27, 2012 WASHIRIKI WA MISS EAST AFRICA 2012 Wafuatao Ni Baadhi Ya Washiriki Waliokwishateuliwa Na Nchi Zao Wa Mashindano Ya Miss East Africa 2012 Yanayotarajiwa Kufanyika Tarehe 7 December Mwaka Huu Dar Es Salaam, Tanzania. Fainali za mashindano haya zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius. Mashindano Haya Huandaliwa Na Kampuni Ya Rena Events Ltd. Ariella Kwizera - Burundi Akuot Phillip - South Sudan Ayisha Nagudi - Uganda Jocelyn Diana Maro - Tanzania Lula TekleHaiManot - Ethiopia Rahwa Afeworki - Eritrea AnnaBelle Pointe - Seychelles Ellidas Chirwa - Malawi Posted by David Ndaiga at 7:07:00 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook Reactions: Thursday, October 25, 2012 EXCLUSIVE INTERVIEW WITH JOKATE MWEGELO. Tulipokuwa tunaelekea mwishoni mwa wiki iliyopita,kuna jambo jipya lilikuwa linatokea. Jokate Mwegelo ambaye kwa wengi hahitaji utambulisho wa kina,alikuwa akizindua kampuni yake inayokwenda kwa jina la Kidoti Loving ambayo itajikita zaidi katika bidhaa mbalimbali zinazoendana na masuala ya urembo.Kwa kuanzia, Jokate alizitambulisha aina nane za nywele(weaving) ambazo Kidoti Loving tayari imeshaziingiza sokoni. Baada ya pale nilimtafuta Jokate kuongelea zaidi Kidoti Loving na mengineyo. Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; BC: Jokate,karibu tena na naomba nianze kwa kukupa hongera nyingi sana kwa hatua uliyofikia ya kuzindua rasmi Kidoti Loving Brand.Hongera sana. JM: Asante sana…. BC: Kidoti bila shaka,na wewe mwenyewe umeelezea kwamba hilo jina linatokana na “birth-mark” uliyonayo hapo usoni kwako. Fine.Unakumbuka ni mtu gani wa kwanza kuanza kukuita kidoti? Na ilikuwaje ukafikia uamuzi wa kuiweka kidoti kuwa ndio brand name? JM: Mtu ambaye naweza kusema ndio alichangia kwa mapana zaidi jina la “Kidoti” ni mdogo wake rafiki yangu wa karibu sana. Ilikuwa mwaka jana na nakumbuka nilikuwa kwenye pressure ya kutafuta jina la kuweka kwenye meza kwenye hafla ya Red Ribbon. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kushiriki na mwandaaji mkuu wa Red Ribbon Gala,Khadijah Mwanamboka alikuwa akihitaji jina la designs zangu. Nikiwa kwenye pressure hiyo yule mdogo wake rafiki yangu ndio akaniambia kwanini usiziite Kidoti? Basi nikajikuta nasema tu zinaitwa Kidoti na kuanzia hapo ndio jina la Kidoti likawa rasmi na ndio mpaka sasa limeshazoeleka hivyo. BC: Nguo,nywele na viatu ni miongoni mwa vitu vitatu ambayo vina nafasi ya kipekee kwa binadamu na hususani wa jinsia ya kike. Kwanini wewe umeamua kwamba uanze na nywele na kama ulivyosema, nguo zitafuata. Kwanini nywele? JM: Yapo mambo kadhaa yaliyochangia uamuzi wa kuanza na nywele. Lakini muhimu zaidi ni kwa sababu kwanza brand yangu nataka iweze kuhudumia mass market hivyo inahitaji investment/capital ya kutosha na vile vile reliable producer. Nilifanikiwa kuvipata hivi kwa uharaka zaidi kwa upande wa nywele hivyo nikaanza kulifanyia kazi. Na nimefanyia kazi kwa mwaka mzima mpaka jana ndio tumeingia sokoni.. BC: Tunaposikia habari za nywele(hususani hizi za bandia-weaving,wigs,etc) ni vigumu wakati mwingine kwa mtu wa kawaida kuelewa tofauti inayoweza kuwepo katika brand fulani mpaka nyingine.Kwa lugha nyepesi tu Kidoti Loving inajitofautisha namna gani na nywele zingine zilizopo madukani? JM: Kama nilivyosema awali tumefanyia kazi hili suala kwa muda wa mwaka mzima. Na ninaposema kazi, ninamaanisha ninamaanisha pamoja na utafiti wa kina kujua nini hakipo kwenye soko la sasa hapa nchini kwa mfano, ambapo sisi tunaweza kuingia sasa. Nywele za Kidoti ni za kiwango cha hali ya juu lakini muhimu zinapatikana kwa bei nafuu. Tumezijaribu na wasusi mbalimbali na wamezipenda kuanzia material yake, urahisi wake wa kusukia, haizifungamani, nyepesi, style na rangi tulizochagua ni za kisasa kabisa. Na hata branding/packaging ina mvuto wa kipekee. BC: Mwaka 2006 ulishiriki mashindano ya Miss Tanzania na kuibuka mshindi wa 2. Baada ya hapo ukaenda au kurudi shuleni na kupata degree yako.Unadhani ushiriki wako katika masuala mbalimbali ya urembo na elimu vimekusaidia vipi kujiandaa na hii ngwe ya ujasiriamali ambayo umeianza rasmi? JM: Urembo umenisaidia kupata platform ya ku-network na kuonekana na style zangu mbalimbali ambazo zimekuwa zikivutia watu mbalimbali mpaka wengine kuniita “fashionista”. Pia nimekuwa nikishirikiana na wabunifu wa mitindo na shughuli zingine ambazo ziliwavutia hata business partners wangu na kujenga imani yangu kwao. Lakini shule imenisaidia zaidi kwenye jinsi ya kupanga mikakati na kuelewa soko na jinsi ya kuingia sokoni.Pia discipline ya kazi na professionalism kwenye kazi. BC: Wakati wa uzinduzi wa Kidoti Brand umekaririwa ukisema kwamba unaanza ujasiriamali rasmi ili uweze kujitegemea na kusimama wewe kama wewe. Unaweza kuipanua kidogo hoja hiyo? Ulikuwa unamaanisha nini hasa? JM: Kama kuna kitu nakiogopa maishani ni kuombaomba au kuwa tegemezi kwa mtu fulani hasa mwanaume. Naona ni kama utumwa hivyo. Iko kwenye damu yangu na kila siku naomba Mungu anisaidie niweze kujitegemea kimaisha, kujiingizia kipato kitakachonisaida kukimu mahitaji yangu ya kila siku na ya ndugu zangu bila kuwaza kumtegemea mtu. BC: Umejipanga vipi kwenye suala la usambazaji na kuhakikisha kwamba unakidhi mahitaji (demand and supply)? Na tukiongelea upatikanaji wake,nywele za Kidoti zitakuwa zinapatikana wapi na wapi? Bei? JM: Supply itategemea sana na demand. Producers wangu wako tayari so haina neno…. Nywele zinapatikana Kariakoo, Msasani, Mwenge, Sinza kwa kuanzia ila tutakuwa nchi nzima na nchi za jirani very soon inshallah! Bei zinaanzia elfu 9-12. BC: Tofauti na makampuni au brand zingine kadhaa ninazozijua wewe umeanza na tayari unao mwelekeo wa jinsi ya kusaidia jamii.Hebu nieleleze kidogo kwa faida ya wasomaji wetu…Kasikana ni nini hasa na uhusiano wake na Kidoti Loving ukoje? JM: Kwa lugha ya Kingoni, Kasikana inamaanisha “kasichana” ime-inspire Kidoti. Wengi wanafahamu ninapenda sana kujitoa katika mambo ya kijamii. Nina project yangu nataka niifanye kwa kuanzia mkoani Ruvuma kwa ajili ya wasichana. Sasa kama tunavyojua, ili liweze kufanikiwa lazima kuwe na hela. Sehemu za mapato ya Kidoti zitasaidia kulifanikisha hili. Kituo cha wasichana wanapoweza kubadili mazingira, kufanyia kazi talanta zao na kujenga kujiamini zaidi. BC: Mpaka hapo ulipofikia bila shaka umekumbana na changamoto kadha wa kadha.Kwa maana hiyo upo katika mazingira mazuri ya kumpa mtu(mjasiriamali mtarajiwa) ushauri kuhusu biashara, kuthubutu nk. Angetokea mtu akakuomba umpe ushauri ungemwambia azingatie mambo gani? JM: Awe na team yenye moto wa kuona kitu chenu kinasimama hata kama hakuna hela kwanza. Na hiyo timu iwe na watu wenye background na expertise , network na experience mbalimbali ili hata kama hela haipo bado ( which is normally the case) muweze kutumia networks na vipaji vyenu kwa kuanzia. Kidoti haijaanza na hela nyingi, uzuri kupitia urembo na chuo nimekutana na watu wengi sana tukashirikiana vizuri na kuheshimiana kiasi wamekuwa mstari wa mbele kutoa msaada kwangu wa hali na mali. Team yangu ni ya wasomi waliomaliza chuo wenye kiu ya kusaka na kufanya kitu tofauti tulikutana chuo pia. So ni baraka tu. Usidharau mtu huwezi jua atakusaidiaje mbeleni. BC: Bila shaka Kidoti Loving ina mipango mingi ya mbeleni.Nini mipango ya miaka kumi baadaye.Where do you want to see Kidoti Loving reaching? JM: Nataka Kidoti isimame yenyewe bila jina Jokate. Kuanzia mwaka kesho nitakuwa na mashindano ya kusaka The New Face Of Kidoti ili brand iwe sustainable. Nitatambulisha rasmi nguo na vitu vingine mwaka kesho Q1. Ila speaking long term nataka brand iwe kubwa zaidi yenye mvuto wa kipekee na kukubalika, madukani kote na kwenye mikoa mikubwa nk… Ila kwa mfano unaoonekana napenda sana nitengeneze kitu Kama Victoria’s secret, Zara…. Hiyo ndio mifano ninayoisoma kwenye biashara hii. Sasa mchanganyiko wa brand kubwa kama hizo lakini iwe na taste ya kiafrika ni hatari sana… BC: Asante sana kwa muda wako Jokate na kwa niaba ya timu nzima ya BC,nakutakia kila la kheri JM: Asante sana. Special Thanks To; Jeff Msangi (www.bongocelebrity.com). Posted by David Ndaiga at 9:57:00 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook Reactions: Monday, October 22, 2012 CHAPA LAPA -- NURU Ft. VEDASTO (New Hit On Town). Umeshamsikia Kwenye Nyimbo Nyingi Na Baadhi Ya Hizo Ni Pamoja Na Ile Aliyoitoa Kwa Ushirikiano Na Bob Junior Kutoka Sharobaro Records Iliyokuwa Ikiienda Kwa jina la '' Muhogo Andazi''. Alikuja tena kivingine akikwambia ''Super Star'', wimbo ambao ulifanya vizuri pia kwenye masikio ya wengi. Huyu hapa amerudi tena na safari hii anatuletea kitu kingine kutoka G-Records, akiwa amemshirikisha Vedasto na wimbo unaitwa '' CHAPA LAPA''. Uangalie Hapa Chini; Posted by David Ndaiga at 2:26:00 PM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook Reactions: Friday, October 19, 2012 '' JUST SIMPLE '' WEDDING DRESS 2012/13 Posted by David Ndaiga at 9:14:00 AM No comments:

No comments:

Post a Comment