Sunday, November 25, 2012
HATA WEWE UNAWEZA KUFANIKIWA
MAFANIKIO hutokana na jitihada katika maisha tunayoyaishi. Watu wengi wanaopenda kufanikiwa mara zote hutafuta mbinu mbalimbali ili kutimiza ndoto zao. Hivyo basi unatakiwa kuota ndoto ya mafanikio yenye malengo makubwa.
Binafsi ninaamini katika malengo hayo kuwa kuna mafanikio endapo utamaanisha. Wakati mtu anapoanza kuwa na malengo makubwa, anaanza kwa kufikiri jinsi Mungu alivyomwezesha katika jambo hata kufikia hatua na kufanikiwa.
Ndoto hiyo ya mafanikio haina gharama, ni jinsi ya unavyoweza kujipangia muda na ratiba zako. Kumbuka ukiwa na malengo ya mafanikio haitakugharimu chochote.
Unaweza ukawa na malengo ya kuanzisha mradi mkubwa pasipokuwa na fedha, inabakia kuwa ni ndoto tu. Mungu alianza kuumba dunia ikiwa haina kitu. Tunaweza kuwa na malengo makubwa ya mafanikio katika maisha yetu, haijalishi ni ya aina gani.
Unapokuwa na ndoto hiyo ya kutaka kufanikiwa, kamwe usiruhusu moyo wako kuvunjika au kuwa katika hali ya kukata tamaa na wasiwasi. Kwani hali hiyo itakudhoofisha na kukufanya usisonge mbele, bali urudi nyuma.
Unapohitaji jambo kubwa kutokea katika maisha yako unatakiwa kuwa na maono mapya. Kumbuka hata wewe unaweza ukawa na maono makubwa ya ajabu.
Haijalishi ni mtu wa aina gani, umetoka wapi au umepatwa na jambo gani, katika hali uliyonayo unaweza kuwa na maono mapya. Kumbuka malengo makubwa hayawi kwa watu waliofanikiwa, bali ni kwa wale wanaotaka kufanikiwa.
Vyovyote uwazavyo, ndoto inainua na kuweka kitu kipya katika maisha yetu, inatutengeneza na kutusogeza mbele, inatuwezesha kufikia malengo makubwa tofauti na ilivyokuwa awali. Inatuwezesha kufanya kitu kikubwa ambacho hatujawahi kukifanya tena kabla ya hapo.
Je, wataka kuwa fulani? Kusimama nje ya kusanyiko kubwa? Kukumbukwa? Hali hiyo inakuwepo ndani ya mioyo yetu inayodunda na kutaka kupata siri ya mafanikio.
Tunataka kuwa fulani. Inawezekana, ndiyo inawezekana. Mungu ametoa kwa kila mtu uwezo na vipaji mbalimbali. Wakati Mungu anakuumba alikupa kipaji na akasema kama utatumia kipaji ulichonacho atakiongeza, na kama hutatumia kipaji ulichonacho utakipoteza. Kukitumia kipaji chako au kukiachia ni juu yako wewe!
Dunia yetu imejaa vipaji vingi na uwezo ambao hautumiwi. Unatakiwa kulima kwa bidii, na kupalilia ili upate mavuno bora. Tumia kipaji chako kabla hujakipoteza.
Unaweza kudhani kuwa hauna kipaji chochote, si kweli, labda inawezekana haujagundua kipaji chako. Inawezekana umekiweka kipaji chako kabatini. Amini kuwa kila mmoja anacho kipaji chake alichopewa na Mungu.
Waweza kutumia kipaji ulichonacho au kukipoteza. Maisha yetu yamejengwa katika kanuni hiyo. Kuna mifano mingi ya kupoteza au kupata, hiyo ni kanuni ya kawaida.
Chukua hatua ambazo zitaifanya ndoto yako kuwa kweli. Ota ndoto yenye thamani katika maisha yako. Kama hauna malengo, haitawezekana matarajio yako kutimia. Ndoto inaanza unapokuwa na wazo. Kumbuka watu huvutiwa na wenye maono makubwa.
Chagua maono yenye matarajio. Baadhi ya watu wanapoteza muda wao kwa kuwa na malengo ambayo hayatawasaidia. Mfano, kuna kijana katika miaka iliyopita alisaidiwa kupewa ushauri baada ya kupoteza muda wake mwingi akifikiria ni jinsi gani ataweza kumpata mke wa jirani yake na kumfanya awe wake. Ndoto yake hiyo haikuwa ya thamani ya muda mrefu.
Wakati wazo linapokujia katika ufahamu wako, iulize nafsi yako maswali matatu. Je, jambo hilo litampendeza Mungu? Litawasaidia watu wanaoteseka? Kwa maneno mengine litakuwa msaada kwa watu? Litaleta mafanikio mazuri kwako? Kama jibu lako ni ndiyo katika maswali yote, utakuwa na maono yenye mafanikio.
Unapoamua kufanya jambo fulani, usijiulize ulize kuwa hii ni njia nyepesi ya mafanikio? Au ni njia rahisi? Inaweza kuwa na usalama? Haitakuwa na vikwazo? Hakuna utakachoshindwa utakapofanya bidii. Hakuna mwenye nguvu ya kuua ndoto yako, isipokuwa wewe mwenyewe.
Panga mipango vizuri kwa kuwa huwezi kujenga bila ramani. Huwezi kufanikiwa matarajio yako pasipokuwa na malengo makubwa. Ninamfahamu mtu aliyekuwa na maono makubwa lakini yalikuwa hayafiki mbali. Ni kwa sababu alikuwa hana ramani ya maono yake.
Hakikisha unatimiza ndoto uliyojiwekea. Malengo yako hayawezi kufanikiwa kama hujajitoa kufanya hivyo. Ili kufanikiwa katika mipango yako unahitaji juhudi na kufanya kazi kwa bidii ili upate mafanikio.
Amua pa kuanzia. Fanya uamuzi sahihi. Panga muda wa kuanza. Usitafute sababu ya kuacha kufanya malengo yako kwa muda ulioupanga. Katika dunia yetu kuna watu wengi wenye mipango mingi lakini hawaifanikishi. Jiondoe katika kundi hilo. Fanya kitu. Andika barua, piga simu. Anza hatua ya mafanikio.
Jiamini waweza kutimiza ndoto zako. Wakati unajaribu kupata mafanikio utaona kuwa ni kipindi kigumu kwako. Hali ya kukata tamaa inakuwepo katika moyo wako, ikisema jiondoe katika hatua ambayo unataka kuianza ya kupata mafanikio katika maisha yako, kataa.
Kama unakutana na kipindi cha majaribio katika biashara, ndoa, mambo yako binafsi, kwenye wingi wa watu au hali ya maisha uliyoizoea na uko tayari kukabiliana nayo, songa mbele usikate tamaa.
Unachofanya ni kujaribu kupata mafanikio, tena mafanikio makubwa. Katika kila mafanikio unayoyapata, kuna gharama ya kulipa. Kumbuka huwezi kupata ushindi bila kulipa gharama.
MAMBO YA KUHUZUNISHA NA NAMNA YA KUYAKABILI
KUFIWA NA MUME/MKE
Jambo la kwanza linalohuzunisha zaidi ambalo lina kiwango cha asilimia 100 ni mtu kufiwa na mke au mume. Rekodi zinaonesha kuwa, watu wanaofiwa na wapenzi wao huwa na huzuni kubwa kiasi cha kutishia maisha yao.
Msongo wa mawazo, mauzauza ni mambo ambayo yanatajwa kusababisha vifo vya ghafla na vya muda mfupi kwa watu waliofiwa na waume/wake zao, huku sababu ya vifo hivyo ikibaki kuwa ni msongo wa mawazo (stress).
Licha ya ukweli kwamba kufiwa mume/mke ni jambo zito lakini, huzuni inapokuwa ya kudumu kiasi cha kutishia maisha ya mtu, suala la uzembe wa kufikiri huchukua nafasi.
Hivyo, ili mtu aweze kuepukana na matatizo yanayotokana na kufiwa ni lazima afuate muongozo ufuatao ambao utamsaidia kuipunguza au kuiondoa huzuni hiyo ambayo ni mbaya kuliko nyingine zote duniani.
Kwanza, ni kukubaliana na ukweli kwamba mwenza amefariki na hatarudi, kulia na kuhuzunika hakusaidii. Pili ni kuziondoa taratibu kumbukumbu zote zinazokuja na kutawala mawazo kuhusu mkeo/mumeo aliyekufa.
Usiyazamishe mawazo kwenye tukio hilo, ukiona kuwaza kunajitokeza ni bora kupuuza mawazo hayo kwa kutoyapa nafasi ya kukutawala. Usipende kukaa peke yako kwa muda mrefu. Usiangalie picha na kutembelea kaburi la marehemu mara kwa mara bila kuwa na sababu za msingi.
Usivute taswira ya maisha mliyokuwa mkiishi zamani. Kaa karibu na watu uwapendao, tembelea sehemu zenye kuvutia. Epuka kuzungumzia mambo ya marehemu wako. Badili mazingira ya chumba mlichokuwa mkilala, kuwa bize na majukumu yako na andaa mipango ya kumtafuta mwenza mpya.
TALAKA
Suala la kutalikiana linahuzunisha watu kwa asilimia 73, wengi kati ya wanaokumbwa na kadhia hii wanatajwa kuwa ni wanawake, ambao kwa nchi za dunia ya tatu ndiyo wanaoondolewa kwenye himaya zao za ndoa kwa vile wanaume ni watumwa wa mfumo dume. Hata hivyo imebainika kuwa wanaoumia zaidi ni wale wanaoachwa bila kuwa na makosa ya msingi (haibagui wanaume au wanawake).
Mwanamke au mwanaume aliyetendwa, hukumbwa na msongo wa mawazo, hasa anapofikiria sababu dhaifu za kuachwa kwake na pengine kulinganisha kuachwa na wema aliomtendea mwenzake wakati wakiishi pamoja. Kwa mujibu wa uchunguzi, watu wanaohangaika na mawazo ya kuachwa ni wale wanaodhani wamedhalilika (Inferiority complex) kwa kuachwa kwao. Mara nyingi huwa ni watu wa kutojiamini juu ya kuweza kuishi maisha ya upweke na wakati mwingine kudhani jamii inawacheka.
Ifahamike kwamba kuachana si kashfa, mtu anayeachwa anatakiwa kujiamini na kuishi kwa wema ili kuiaminisha jamii kuhusu tabia yake njema na kuwafanya watu waone kuwa mhusika hakustahili kuachwa.
Aliyeachwa lazima ajitume kufanya kazi kwa bidii na apange mipango yake mipya ya kimaisha, lengo likiwa ni kuonesha uwezo wake wa kuishi peke yake. Asijenge chuki kwa mwenzake, asipange kulipa kisasi aepuke kuchunguza mwenendo wa mwenziwe, kukutana au kuwasiliana naye. Aishi karibu na rafiki, watoto au ndugu zake, awapende na aombe ushauri kwao mahali anapoona anakwama, azuie mawazo ya kuachwa.
MIGOGORO YA NDOA
Watu ambao hawaishi kwa amani kwenye ndoa zao ni wepesi wa kupatwa na msongo wa mawazo. Ndoa zenye wanaume/ wanawake wasaliti zinahuzunisha wengi. Lakini ushauri wa kitaalamu unaotolewa kuhusu jambo hili ni kila mwanandoa kumtambua mwenzake kitabia na anapoona hakuna ulinganifu amchukulie mwenzie kama mgonjwa mwenye kuhitaji tiba na wala si mtesaji.
Haifai kumfumania mwezako na kuanza kuwaza na kulia badala ya kutafuta ufumbuzi au kwa lugha nyingine tiba. Ni vema kila tatizo limalizwe kwa mwafaka, kasoro za mume au mke zisihifadhiwe kifuani na kupewa muda wa kuumiza akili.
Viongozi wa dini, ndugu, wazee, rafiki, wanaweza kusaidia kujenga nyufa za ndoa. Pale inapothibitika kwa ushahidi kuwa mwanaume/mwanamke hawezi kujirekebisha hakuna njia salama ya muumizwaji zaidi ya kuvunja ndoa au uhusiano wake na huyo mwanaume/mwanamke. Haipendezi kuzidisha kiwango cha uvumilivu kwa vile madhara yake huwa ni makubwa.
KUFUNGWA JELA
Maisha ya gerezani yanaumiza. Wafungwa wengi hasa wa magereza yaliyopo ulimwengu wa tatu, hali za wafungwa huwa ni mbaya. Wengi hufariki kifungoni au muda mfupi baada ya kumaliza. Hii inatokana na magonjwa ambayo hutokea kwa sababu ya kushindwa kumudu mazingira na wakati mwingine kutokukabiliana na matokeo ya hukumu, jambo ambalo huwafanya wafungwa wengi kuwa na sononi zisizo isha. Hivyo ili kukabiliana na huzuni ya kufungwa lazima mfungwa mwenyewe akubaliane kwanza na matokeo.
Jambo la pili ni kuacha kushindana na mshtaki wako kwa kutumia akili, usikaribishe mjadala wa mawazo kwenye akili yako, chukulia kwamba hiyo ni bahati mbaya ya maisha yako sawa na ajali. Hesabu kuwa hayo ni mapito na ipo siku utatoka ukiwa mshindi na ukweli utajulikana.
Nelson Mandela alipofungwa alituliza mawazo na hatimaye alitoka na kuwa rais wa nchi na leo ukweli wa kuonewa kwake kila mtu kaufahamu. Ushauri mwingine ni kuzidisha upendo kwa wenzako, kuwa mwema, ridhika na upatacho na wakati mwingine tumaini siku njema kwa kuiambia nafsi yako kuwa, maisha ya gerezani yatapita au kama kifungo ni cha maisha, huna budi kukubali kuishi kama mfungwa.
KIFO CHA NDUGU WA KARIBU
Anapofariki baba, mama, kaka, dada, mtoto wako huzuni hutamalaki. Lakini ni vema ukarejea sehemu ya kwanza kwa masaada zaidi. Ila kwa nyongeza usiwe mtu wa kulinganisha matokeo ya maisha yako ya uyatima na yale yaliyokuwepo wakati wazazi.
Kwa mfano usidhani unateseka kwa sababu wazazi wako hawapo (wamekufa), inawezekana hata wangekuwepo ungeteseka vile vile. Pambana na maisha wewe kama wewe hatimaye utashinda. Kumbuka kadiri unavyolia ndivyo unavyozidi kujitesa na kujisogeza kwenye hali mbaya na pengine kufa mapema.
Hebu fikiria wangapi wamefiwa na wazazi wao, lakini wanaishi leo maisha ya raha, kwa nini wewe usiweze. Au ni wangapi walifiwa na watoto na leo wamepata wengine wazuri.. Kumbuka kupenda kilichokufa ni kukinai kilicho hai na kutopenda kijacho. Hivyo kama unampenda zaidi mtoto aliyekufa sina shaka utamdharau uliyenaye na upo uwezekano hata usipate mwingine kwani mawazo yako yanaweza kuharibu afya yako na kukufanya usishike mimba maisha yako yote.
KUUGUA AU KUJERUHIWA
Watu wengi wanapojeruhiwa hasa vibaya au kupatwa na magonjwa sugu yanayotajwa kuwa hayana tiba hufadhaika sana. Mgonjwa kama kansa, kisukari, ukimwi, BP yamewahuzunisha wengi, hii inatokana na hofu ya kufa, ingawa ukweli unabaki kuwa kifo hakina ushirika na magonjwa hayo tu kwani kuna wanaokufa bila kuugua magonjwa hayo.
Jambo kubwa la kufanya ni kuondoa hofu kwa kuchukua mifano ya watu ambao wameishi/wanaishi kwa muda mrefu wakiwa na magonjwa hayo, lakini hawajafa. Usijifananishe na waliokufa mapema kwani inawezekana walikuwa na hofu ndiyo maana wakafa. Hofu ndiyo inayotajwa kuua watu wengi kuliko hata magonjwa yenyewe. Acha kufikiria mawazo ya kufa, usikate tamaa, endelea kufanya mambo yako kama kawaida na uwe karibu na watu wa kukufariji si wa kukuvunja moyo.
Usijihukumu kuwa ni mkosa mbele ya jamii na usione kama umeonewa na Mungu. Tembelea wagonjwa wengine hospitali, huko utaona wenye shida zaidi yako, hiyo itakupa unafuu wa kubeba udhaifu wako. Kwa wale waliopata ajali ni vema wakakubaliana na matokeo, wakatulia na kuwatembelea watu wenye ulemavu ili kupata msaada wa kimawazo na wakati mwingine kufanya ibada ya kuomba wapewe uvumilivu.
Ifahamike kuwa, ulimwenguni kuna walemavu wengi ambao wana maisha mazuri kuliko hata wazima, hivyo basi kuwa kilema haimaanishi kuwa umefikia mwisho wa maisha.
NDOA
Mazingira ya ndoa hasa yanapokuwa magumu tofauti na mategemeo ya awali hutia huzuni. Pesa inapokosekana, mke/mume anapokuwa haeleweki, ndugu na jamaa wanapokuwa na tabia mbaya zinazokwenda kinyume na misingi ya ndoa ni mambo yanayotia simanzi. Lakini pamoja na hayo kukosekana kwa mtoto ni jambo linalowafadhaisha watu wengi.
Namna ya kwanza ya kufanya ni kwa wanandoa wenyewe kuondoa mikwaruzano baina yao, hili likifanyika litawapa uwezo wa kukabiliana na matokeo yote mabaya na kupata ushindi, lakini pia wanandoa wanaopatana ni rahisi kufarijiana katika shida kuliko wenye migogoro.
Ni jukumu la wanandoa kukuza uhusiano na upendo ili kutiana moyo nyakati za shida. Kuepuka maneno ya kusikia na wakati mwingine kutozingatia kejeli za watu wa pembeni wanaobeza maisha yao ya ndoa. Kuwa na imani kwamba nyakati za kufanikiwa kwa kupata mtoto zipo na hakuna kukata tamaa kwa kuangalia muda mlioishi kwenye ndoa.
Lakini hata kwa wale ambao bado hawajaolewa nao wasihuzunike, kwani mara nyingi ndoa hutengenezwa na watu wenyewe kupitia wapenzi ambao uchunguzi unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wanaotaka ndoa wana wapenzi.
KUFUKUZWA KAZI
Watu wengi huchanganyikiwa au hushindwa kumudu maisha muda mfupi baada ya kufukuzwa kazi. Hii inatokana na vyanzo vya mapato kukoma na pengine heshima ndani ya jamii kupungua. Jambo kubwa la kufanya baada ya kutimuliwa kazi ni kutulia. Kama ilivyo kwa vifungu vingine ni vema mtu aliyefukuzwa kazi akawa karibu na marafiki sahihi ambao watamshauri na kumkutia moyo.
Aliyefukuzwa kazi hatakiwi kujifungia ndani na kuwaza. Jukumu la kwanza kabisa ni kupunguza matumizi, kutafuta vyanzo mbadala vya kuingiza kipato kama kufanya kazi za ‘party time’ na kadhalika.
Kuanza kutafua ajira mpya kwa kupitia watu wako wa karibu uliokuwa nao kazini ni jambo la muhimu. Usikimbilie kurudi kijijini, kwani huko unaweza usimudu mazingira ya kimaisha. Omba msaada kwa ndugu pale unapoona mkwamo. Acha anasa na ulevi kwani utakuingiza kwenye matumizi makubwa pesa yasiyostahili kwa wakati huo na wakati mwingine kukuharibu fikra.
Kuwa mwaminifu na usimweleze kila mtu shida zako. Epuka ushawishi wa kimakundi. Itafute furaha kila wakati kwa kusikiliza muziki ili kuifanya akili iwe imara katika kukupa majibu ya nini cha kufanya baada ya kufukuzwa kazi. Maisha yanawezekana pia bila ajira kwani kuna wengi wanaishi bila kazi za viwandani. Kama kuna mafao uliyopewa baada ya kuondolewa kazini ni vema ukayatumia vema, ili yakusaidie wakati ukitafuta ajira mpya.
SULUHU BAINA YA WANA NDOA
Wapenzi na hasa wanandoa wanapokosana na mmoja kati yao akawa hataki suluhu, yule anayekataliwa huingia katika msongo mkubwa wa mawazo. Mawazo hutawala juu ya kufikia makubaliano na yule aliyempenda, hangaiko la moyo hutikisa mwili kiasi cha kutoweza kula wala kulala, hatimaye mtu hupata ugonjwa wa moyo na baadaye kupoteza maisha.
Inashauri kuwa mkishahitilafiana na mpenzi wako, mtafute umuombe radhi, akikataa washirikishe ndugu au rafiki wa karibu anayesikilizwa na mpenzi wako ili akusaidie kutafuta suluhu. Wazazi na wazee ni budi wakapewa nafasi pia.
Unapoomba msamaha usilazimishe sana kusamehewa, kufanya hivyo kunaweza kumpa kiburi mpenzi wako na kukataa kukusamehe kwa kujua huna pa kwenda na kwamba kukuacha kwake kunakuumiza. Suluhu inapokosekana unatakiwa kutuliza mawazo kwa kuutumia muda wako wa mapenzi kufanya kazi zako za kukuingizia kipato.Pendelea kubadilishana mawazo na watu wengine hasa wenye mafanikio.
KUSTAAFU KAZI
Uchunguzi unaonyesha kuwa, watu wengi hufariki dunia muda mfupi baada ya kustaafu kazi, hii inatokana na wengi wao kushindwa kumudu mazingira mapya ya maisha nje ya ajira zao. Kasoro kubwa inayopatikana kwa watu wa aina hii ni maandalizi mabaya ya kuelekea kustaafu.
Angalia mada kuhusu maisha ya uzeeni iliyopo ndani ya kitabu hiki ili kufahamu namna ya kustaafu kazi bila madhara. Lakini ni vema mtu aliyestaafu akatafuta shughuli mbadala itakayomfanya awe ‘bize’, asijiingize kwenye starehe na matumizi makubwa ya pesa, asikurupuke kufanya biashara na kuanzisha miradi mpaka ashauriwe, apunguze matumizi ya familia ili asome upya mfumo wa maisha bila kutegemea mshahara.
KUUGUZA NDUGU
Ni wazi kuwa watu wanapouguza ndugu zao huwa na huzuni hasa wanapowaona jinsi wanavyohangaika na maumivu. Ni kweli, inatia simanzi pale unapomuona mjomba, shangazi, mama mkubwa au shemeji yako akiugua, lakini njia ya kukabiliana na huzuni hiyo ni kutopima kwa kina namna anavyojisikia mgonjwa wako.
Elekeza nguvu katika kumsaidia, kumpenda kila anapoonekana kuumia, kuwa naye karibu na kumfariji, usioneshe huzuni mbele ya mgonjwa kwani kufanya hivyo ni sawa na kumvunja moyo na kumfanya mgonjwa wako ajisikie vibaya zaidi. Mara nyingi njia sahihi ya kumuuguza mgonjwa si kumuonea huruma bali ni kumpa faraja na kuamini kuwa atapona.
UJAUZITO
Ujauzito nao unatajwa kuwatia huzuni baadhi ya wanawake wajawazito. Wanawake wengi huwa na hofu ya kujifungua salama. Njia sahihi ya kuepuka tatizo hili ni kwa mjamzito mwenyewe kukwepa upweke na afanye mazoezi. Asikaribishe hofu kwa mambo ya kusikia juu ya mwanamke fulani aliyekufa wakati akijifungua au kutumia muda mwingi kuwaza namna atakavyoukabili uchungu wa kuzaa na hata kuhofu kupatwa na kifafa cha mimba na kupoteza maisha.
Wanaume na ndugu hawatakiwi kuwaudhi wajawazito. Kusikiliza muziki, kuangalia sinema za kufurahisha ni muhimu kwa mjamzito ili kumuondolea hofu ya kujifungua. Mjamzito hatakiwi kupewa taarifa za mtu aliyekufa akijifungua au kuogopeshwa kwa maneno kupitia hali aliyonayo. Kwa mfano “hee, miguu inavimba hii ni hatari sana inawezekana ukapata presha wakati unajifungua” Maneno haya hayafai kumwambia mjamzito na kama ana dalili mbaya ni vema apelekwe kwenye tiba kuliko kutishwa.
MATATIZO YA KUJAMIIANA
Hitilafu katika mambo ya kujamiiana hutia huzuni pia. Wanaume wenye kasoro za kimaumbile na upungufu wa nguvu za kiume, wanawake wasiohisi tendo hukabiliwa na msogo wa mawazo. Njia pekee ya kukabiliana na matatizo haya ni kuwaona wataalamu.Haifai kuumia kwa kuwaza namna ya kuondokana na tatizo la kasoro za kufanya mapenzi wakati tiba ipo.
Jambo jingine ni kwa wapenzi kuwa wawazi pale hisia zinapokosekana. Ni lazima kusaidiana kwa kushauriana, haipendezi kuyafanya mapenzi kuwa kitu cha siri. Kama mwenzio hakutoshelezi, ni vema kuwekana wazi na kutafuta suluhu ya tatizo kwa kuwashirikisha wataalamu na baadhi ya wazee ambao kimsingi wanafahamu mambo mengi.
KUISHI NA FAMILIA MPYA
Inashauri kwamba mtu anapoingia kwenye familia mpya (akiolewa, akiishi na ndugu katika ukoo, baada ya wazazi wake kufariki dunia), hatakiwi kujihukumu, akwepe kutafsiri atendewayo kama mtu ambaye si ndugu, bali kwa kila jambo aone anafundishwa na afanye kila awezalo kufuata kanuni na mazingira mapya.
Mara nyingi kinachowahuzunisha watu wengi wanaoishi ndani ya familia mpya ni mawazo yao, ambayo huwashawishi kufikiri kila baya wanalofanyiwa basi linatokana na sababu ya ujane au uyatiwa wao, wasifahamu kuwa kukoseana ni sehemu ya maisha tu na kinacholeta maana mbaya ni mawazo ya mtu si tendo lenyewe.
Jambo la msingi zaidi kwa mtu anayeishi na familia mpya ni kuwa na nidhamu ya hali ya juu, ajitume katika kufanya majukumu yake ya kimaisha na awe tayari kubadili tabia sawa na walezi wanavyotaka.
MABADILIKO YA KIBIASHARA
Kushuka kwa biashara, kubadili maeneo na hofu za kufilisika ni mambo ambayo huwatia simanzi watu katika kufikiri. Inashauriwa kuwa mtu anayeendesha biashara akiona dalili za biashara yake kushuka anatakiwa atafute mshauri wa biashara ili apate muongozo mpya.
Hifai kubabaika na kuwaza bila kutafuta kasoro zinazoporomosha biashara yako. Ni vema kupitia mapato na kubuni mikakati mipya ya kujenga panapobomoka. Ushauri wa rafiki mzoefu wa kibiashara ni mzuri pia. Lakini kujifunza mbinu mpya na kukabiliana na changamoto za kibiashara kwa kusoma masoko upya ni jambo linalotakiwa kufanyiwa kazi na mfanyabiasha yeyote. Haifai kuishi na wasiwasi wa kufilisika, kwani kufanya hivyo kuna madhara makubwa kisaikolojia.
KUHAMA NCHI
Unapohama nchi ambayo imeendelea kiuchumi na kuhamia nchi maskini utafadhaika au unapoambiwa kuwa unakwenda kuishi nje ya nchi unaweza kuwa na huzuni kwa upande mmoja, kwa mfano kufikiria maisha mapya mbali na jamii uliyoizoea na mambo kama hayo. Unachotakiwa kufanya ni kutobabaika na badala yake unachotakiwa kufanya ni kujifunza tamaduni za huko na kuwa tayari kubadilika na wakati mwingine kuyakubali mabadiliko hayo kama hatua za maisha yako. Mwisho ni kuwatumia wenyeji wako kama dira na kujitahidi kuwazoea na kuwafanya rafiki na ndugu zako.
RAFIKI KUFARIKI
Fuata muongozo wa kipengele cha kwanza na cha tano katika kupata ufumbuzi wa tatizo hili la kufiwa na rafiki yako. Haifai kusononeka kupita kiasi kwa suala ambalo huwezi kubadili matokeo yake.
MABADILIKO KAZINI
Ukibadilishwa kazi kutoka kitengo kimoja kwenda kingine kunaweza kukuhuzunisha, lakini unachotakiwa kufanya ni kuonyesha uwezo wako kwa kufanya kazi kwa furaha bila kupunguza nguvu, maana inawezekana ulipopangiwa, bosi wako kaona wewe unafaa au pengine unajaribiwa katika safari ya kupandishwa cheo.
KUPINGWA NA MKEO/MUMEO
Unapopingwa katika maamuzi yako na mumeo au mkeo ambaye awali alikuwa hafanyi hivyo unatakiwa kujiangalia mwenyewe mahali ulipokosea na kuangalia hoja za mwezako kuliko kuumia moyoni kwa kudhani unadharauliwa. Fanya uchunguzi, kuwa na mazungumzo ya kina na mwenzi wako ujue sababu ili marekebisho yafanyike haraka.
KUKOPA MKOPO MKUBWA
Watu wengi hushawishika kirahisi kukopa pesa nyingi, lakini wanapopewa na kuanza kutafakari namna ya kulipa huingiwa na huzuni, hivyo inashauriwa kuwa kabla ya kukopa mkopaji lazima ashauriwe na watalaamu namna ya kuutumia mkopo huo, ili aweze kujiamini na kuwa makini na urejeshaji ambao ndiyo huwatia hofu wakopaji wengi.
UREJESHAJI MKOPO
Unapokuwa umekopa au kuweka reheni kitu chako na hatimaye tarehe za mwisho za kurejesha zikawa usoni pako wakati ukiwa huna kitu/pesa, unaweza kubabaika na kuhuzunika. Unachotakiwa kufanya ni kutazama namna ya kupata pesa za kurejesha hata kwa kuuza vitu vingine visivyokuwa na umuhimu mkubwa ili kukomboa ulichoweka reheni. Kuwashirikisha ndugu,rafiki na watalaamu wa masuala ya pesa wakiwemo wakopeshaji ni suala muhimu.
KUBADILISHWA MAJUKUMU YA KAZI
Watu wengi hupatwa na huzuni pale wanapobadilishiwa majukumu kazini ikiwemo kuhamishwa vitengo, huku hofu yao ikiwa katika mapato na kumudu majukumu mapya waliyopangiwa. Jambo kubwa linalotakiwa kwa mfanyakazi anayehamishwa kitengo ni kujiamini na kuendelea kufanya kazi kwa nguvu. Kitendo chochote cha kuvunjika moyo baada ya mabadiliko huweza kumfanya apoteze uwezo wa kufanya kazi na kujikuta anafanya kazi kwa kiwango cha chini na kuonekana hafai na hatimaye kufukuzwa kazi.
MTOTO KUONDOKA NYUMBANI
Wazazi wengi huhuzunika pale mtoto ambaye walikuwa wanaishi naye anapofikia uamuzi wa kuondoka kwa sababu za kikazi, kimasomo, kuolewa na hata kujitegemea. Kimsingi huzuni hii ni ya bure kwa vile kukua kwa mtoto ni pamoja na kufikia hatua hizo za kuachana na wazazi na kuishi kama mtu mzima.
Hivyo, wazazi wanachotakiwa kufanya si kuhuzunika bali ni kuhakikisha kuwa wanampatia mtoto wao silaha za kuwa salama huko aendako ili aweze kuwasaidia. Ikiwa mtoto anakwenda shule basi ni lazima wazazi wamuwezeshe kusoma kwa furaha na ikiwa anaanza maisha mapya msaada wa mawazo na elimu ya maisha mapya ni vema kumpatia.
MATATIZO YA KISHERIA
Watu wengi hukumbwa na huzuni pale wanapokabiliwa na maatizo ya kisheria, kwa mfano kesi na tuhuma mbalimbali. Hata hivyo uchunguzi unaonyesha kuwa, huzuni za kupita kiasi zimekuwa chanzo kikuu kinachowafanya watu washindwe kukabiliana na tatizo lililopo mbele yao, hii inatokana na nguvu za mwili na ufahamu kuharibiwa na msongo wa mawazo.
Kwa maana hiyo tunapokuwa na tatizo lolote la kisheria, jambo la kwanza kabisa ni kutulia na kutafakari njia za kumaliza tatizo hilo kwa ushindi. Tafakari hizo lazima ziambatane na namna ya kupatana na walalamikaji, kupata watetezi wa kesi na ushauri wa namna ya kuendesha kesi iliyojitokeza. Si busara kupaniki na kuamua mambo kwa jazba, kufanya hivyo kumewaponza wengi ambao walikuwa na nafasi ya kushinda matatizo, lakini walikwama kwa sababu walipoteza umakini kwa jazba.
KUKWAMA KWA MALENGO
Tunaposhindwa kufikia malengo yetu tuliyojiwekea, kwa mfano kufeli mitihani, kushindwa kuendelea na ujenzi au kufanya hiki na kile tulichokusudia, mara nyingi hutuingiza kwenye huzuni, lakini kanuni za mafanikio yoyote duniani zinaanzia katika mkwamo.
Hivyo basi tunapoona tumeshindwa kufikia lengo la kile tulichotaka kukifanya haimaanishi kuwa hatuwezi, bali tumepungukiwa nguvu ambazo lazima tuzitafute kutoka katika miili yetu kwa kutumia uwezo na uelewa wetu ambao ni mkubwa mara 1000 ya tunaotumia kila siku katika maisha yetu.
Unapokuwa umekwama katika kitu chochote, jiulize sababu kwanini umeshindwa. Baada ya kupata sababu hizo tafakari njia na mbinu mpya za kuelekea kwenye ushindi huku ukiamini kuwa mafanikio yanatokana na juhudi pamoja na kutorudia makosa yaliyoleta mkwamo. Haifai kukata tamaa, hata kama umekwama mara elfu moja.
Tunapokwama mara kwa mara ni vema tukawashirikisha watu katika kila jambo tunaloona kuwa linasumbua akili, ushirikishaji huo unaweza kutusaidia kupata uzoefu kutoka kwa wenzetu ambao pengine wamevuka vikwazo vikubwa tofauti na hivyo tunavyokabiliana navyo.
Jambo la mwisho la kuzingatia tunapoanza hatua mpya za kuelekea katika ushindi tusikubali kurudia kosa, kama kufeli kwako mtihani kulitokana na kutosoma kwa bidii, usirudie kosa hilo ongeza bidii za kusoma au kama umeshindwa kujenga nyumba kwa sababu ya kuwa na matumizi makubwa ya pesa usikubali kuendelea na matumizi hayo, badala yake jibane na utimize nia yako.
MKE KUANZA/KUACHISHWA KAZI
Inaelezwa katika uchunguzi wa kitaalamu kuwa wanaume wengi huhofia wake zao kuanza kazi, hii inatokana na wivu wa kimapenzi . Wanaume hudhani kuwa mke anapokwenda kuajiriwa atakuwa na nafasi kubwa ya kushawishiwa kuanzisha uhusiano mpya na wanaume wengine.
Lakini ukweli ni kwamba huzuni hii mara nyingi huwa ni ya bure na matokeo yake huzaa wivu ambao husambaratisha ndoa na uhusiano. Kitu cha msingi kinachotakiwa kufanywa na mwanaume ni kuwa karibu na mkewe kumjengea hali ya kujiamini na kumtimizia yote anayostahili kama mke, likiwemo tendo la ndoa na ukaribu ambao mara nyingi unatajwa kuwa tiba kubwa ya usaliti.
Aidha kwa wale ambao wake zao wanafukuzwa kazi, jambo la muhimu ni kutiana moyo na kushirikiana kwa ukaribu kutumia muda wa dhahabu kupata kazi. Hili linatakiwa kwenda sambamba na kujaliana wakati wote wa tatizo. Hali yoyote ya kumtenga na kumwacha mkiwa ni hatari kwa uhusiano.
Pamoja na hilo endapo kipato cha mwanamke kilikuwa ni sehemu ya matumizi ya nyumbani basi mume na mke wanawajibu wa kukaa pamoja na kupanga upya matumizi yao ili kuondoa pato ambalo lilikuwa linatumika kutoka katika mshahara wa mwanamke ambaye kafutwa kazi.
KUANZA/KUMALIZA SHULE
Wanafunzi wengi wanapopata nafasi ya kuanza shule kwa hatua yoyote ile hujawa na hofu ya kuweza kukabili mazingira mapya. Inashauriwa kuwa mwanafunzi anapokwenda kuanza shule lazima awe tayari kubadilika kufuatana na mazingira na asiwe mtu wa kuogopa changamoto atakazokutana nazo shule, suala hili limeelezewa kwa kina katika kipengele cha mwanafunzi na mazingira ya shule ambacho kipo ndani ya kitabu hiki.
Hata hivyo, wanafunzi ambao wanamaliza shule wanashauriwa kutohuzunishwa na hilo, badala yake wawe tayari kujifunza maisha kutoka kwa ndugu wanaoishi nao.
MAISHA KUBADILIKA
Hali ya maisha inapoporomoka huhuzunisha, lakini kinachotakiwa katika kukabili tatizo hili si huzuni bali kuwa tayari kutazama kilichochangia kushuka kwa maisha hayo na kukitafutia ufumbuzi wa haraka.
Hata hivyo, watu wengi wanaelezwa kuwa wamekuwa wahanga wa tatizo la kuporomoka kwa maisha kutokana na ubinafsi kwa kutokuwa tayari kubadilishana mawazo na watu wengine katika kupata ufumbuzi wa tatizo na kuhakiki mipango ya maisha yao. Utakuta mtu akipata pesa basi anaamua mwenyewe kuanza biashara bila hata kupata ushauri kutoka kwa watu, hili ni jambo baya.
Ifahamike kuwa kubadilika kwa hali ya maisha ni dalili ya kuwepo kwa makosa makubwa katika mipango ya kimaisha, hivyo basi kila mtu anayepatwa na tatizo hili anatakiwa kutafuta msaada wa mawazo kutoka kwa wataalamu au rafiki, ili apate mbinu za haraka za kujinasua, kwani kuhuzinika peke yake hakufai.
KURUDI KWENYE MAKAZI YA AWALI
Mtu anapokuwa amehama nyumbani na kwenda kuanzisha maisha yake sehemu nyingine na baadaye kushindwa na kurudi nyumbani kwa wazazi au maskani yake ya mwanzo humfanya ahuzunike, lakini kitakachokuwa kinamhuzunisha si kitendo hicho, bali ni hisia za kudhani kuwa atadharauliwa au kuchekwa na watu.
Hili linaweza kuwa kweli, lakini huzuni pekee haisaidii kuondoa tatizo, wakati mwingine mbinu za kijeshi zinaelekeza kuwa unaposhindwa kusonga mbele na ulipo pakiwa na hatari ya kifo hatua za kurudi nyuma hustahili kutumika.
Kurudi huku hakupewi maana ya kushindwa, bali kujipanga katika kushambulia kwa nguvu. Kwa maana hiyo mtu anaposhindwa kuishi peke yake na akabaini kuwa kuwepo kwake katika maisha mapya ni kifo, kurudi nyumbani si kosa, kinachotakiwa ni nia ya kujipanga kuelekea katika ushindi mpya.
USUMBUFU WA BOSI KAZINI
Usumbufu wa mabosi kazini umekuwa ukiwafanya watu wengi kufikia hatua ya kuacha kazi, kuhama vituo au kufanya kazi kwa kiwango cha chini. Hali hii huwapata zaidi wanawake ambao wanafanya kazi na mabosi wanaowataka kimapenzi. Usumbufu wa kutongozwa sambamba na kitisho cha kufukuzwa kazi umekuwa ni huzuni kubwa kwa wanawake wengi makazini.
Inaelezwa na wanawake niliokutana nao wakati wa matayarisho ya kitabu hiki kuwa, kutongozwa na bosi ni kero ambayo haikwepeki hasa pale hisia za kimapenzi zinapokuwa hazipo kwa mtu husika. Wengi kati ya wanawake hukiri kufanya mapenzi na mabosi wao si kwa sababu wanawapenda, lakini kwa lengo la kulinda kazi ambayo huwa hatarini pale maelewano na bosi yanapoyumba.
Kusema kweli uamuzi wa kuwa mtumwa wa mtu kwa sababu ya kazi ni aibu kwa binadamu ambaye ameumbwa na uwezo utashi na nguvu za kukabili matatizo. Njia pekee ya kukabiliana na tatizo hili, kwanza ni kuwajibika katika majukumu kama mfanyakazi na pili ni kujiamini na kujipenda.
Unapowajibika kama ipasavyo unakuwa na ulinzi wa kazi yako si tu kwa yule unayemfanyia kazi, bali hata kwako mwenyewe kwa vile utakuwa na hoja za kujitetea kisheria. Lakini pia kujiamini na kujipenda ndiyo nguzo ya kukulinda wewe na ushawishi usiokuwa na tija kwako. Mfanyakazi lazima awe na msimamo wake kuhusu kazi anayoitumikia, ili asiyumbishwe na kitisho cha kufukuzwa kazi, kwani ajira kwa wachapa kazi zipo nyingi katika ulimwengu.
Mwisho ni kujipenda. Yaani kuwa mwanadamu mwenye utashi na kutokuwa tayari kuuza utu kwa sababu ya kazi. Endapo bosi atakuja na sera za kutongozana kazini, lazima aambiwe uwazi kuwa hilo haliwezekani na yeye auone msimamo, akitambua hilo hataweza kuleta usumbufu ambao hatimaye utamkosesha yeye mfanyakazi na kumtia aibu katika jamii. Lakini kufuata hatua za kisheria ni jambo linalofaa pia.
KUHAMA MAKAZI
Kuhamia katika nyumba mpya kunatajwa kuwatia hofu pia baadhi ya watu, inaeleza kuwa asilimia 20 ya watu wanaohama makazi yao ya awali huhuzunika. Hii inatokana na hofu ya kumudu mazingira mapya.
Watu wengi hushindwa kulala ugenini na kujikuta wakipoteza furaha kwa kiwango fulani. Inashauriwa kuwa mtu kabla hajahamia katika mazingira mapya ni vema akazoea taratibu maeneo anayokwenda, kuwatambua majirani na kusoma tabia zao, lakini zaidi ya yote ni kufuata misingi yote ya ubinadamu na kujiamini.
KUBADILI DINI
Watu wamekuwa wakibadili dini kwa lengo la kutafuta amani katika maisha yao kupitia njia ya kumwamini Mungu, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa wengi wao wamekuwa hawapati amani hiyo kutokana na mambo mawili ambayo ni migogoro ya kifamilia na namna ya kumudu amri za dini mpya.
Asilimia 18 ya watu wanaobadili dini huhuzunishwa na mabadiliko hayo kiasi cha kujutia uamuzi wao, huku idadi yao wakitajwa kurejea katika dini zao za awali au kutaka tamaa ya kiimani na hivyo kupata madhara ya kisaikolojia.
Hata hivyo sababu za kitaalamu zinazotajwa kuchangia ukosefu wa amani hiyo ni udhaifu katika maamuzi. Watu wanaobadili dini wengi wao wamekuwa wakifanya hivyo kwa sababu dhaifu ambazo hutokana na shinikizo la watu wengi wakiwemo wapenzi au tamaa ya kupata pesa na misaada ya kidini, jambo ambalo ni hatari.
Inashauriwa kuwa mtu anayetaka kubadili dini lazima aamue mwenyewe na awe na sababu za msingi zinazodumu si za kimapenzi wala ushawishi wa kipesa, lakini pia awe tayari kukabiliana na matokeo hasi ya uamuzi wake, likiwemo suala la kutengwa na ndugu ambao hawatafurahishwa na maamuzi yake.
Vivyo hivyo, ni busara kuelewa mapema sheria na amri za dini mpya kabla hujajiunga, hili litasaidia katika kupima uwezo wa kutumikia kikamilifu kama muumini. Lakini ikitokea umeshindwa kupata amani uliyotaka, hakuna ubaya kurejea ulipotoka kwa maana ya kujilinda na athari za msongo wa mawazo utakaoletwa na kadhia za dini mpya.
FAMILIA KUBWA
Wazazi na walezi ambao wana familia kubwa wametajwa kuwa ni watu wanaosumbuliwa sana na msongo wa mawazo kwa kiwango ha asilimia 15. Malezi ya familia kubwa ni magumu hivyo walezi wengi hufikia kuona kero na usumbufu mkubwa hasa nyakati ambazo mahitaji ya familia huwa makubwa kuliko kipato. Hivyo ili mtu aweze kuepukana na tatizo hili lazima ahakikishe kuwa anakuwa na familia ndogo ambayo atamudu kuitunza.
Lakini ikiwa ni lazima kuwa na familia kubwa basi ni vema elimu ya kubana matumizi na uzalishaji wa pamoja ikatolewa ili kumfanya kila mtu ndani ya familia awajibike katika kubeba mzigo.
Haifai kuwa na familia kubwa ambayo watu wake hawazalishi. Kama una watoto ambao wanaweza kulima, kufanya biashara, hakikisha unawaongoza katika shughuli hizo, usiwaache walale na kula bure. Wafanye watu wa nyumba yako kuwa msaada kwako pia katika kuendesha gurudumu la maisha.
Njia za kujenga uwezo wa kujiamini
Ni vigumu kuelezea moja kwa moja kujiamini maana yake nini? Lakini mtazamo wa mwanadamu juu ya namna wenzake wanavyomchukulia inaweza kuwa kutafsiri ya neno kujiamini. Ikiwa utajilinganisha na wengine na hatimaye kuhisi aibu, ujue unakabiliwa na tatizo la kujiamini.
Kimsingi kuna mambo mengi yanayoweza kumfanya mtu asijiamini mbele ya wenzake, kiasi cha kujiona duni kwa hili na lile na wakati mwingine hali hiyo humfanya ashinde kufanya hata mambo ambayo anayajua na kwamba amekuwa akiyafanya kila siku
Kisaikolojia huu ni ugonjwa ambao unaweza kuathiri uwezo wa mtu kibaiolojia, nikimaanisha kwamba mtu anaweza kuwa si mlemavu wa miguu, lakini akatembea mbele za watu upande upande, anaweza kuwa na akili lakini akajikuta hawezi kuzitumia kwa sababu si mwenye kujiamini.
Kama ilivyo kwa magonjwa mengine, kuponywa kwa tiba, tatizo hili la kutokujiamini nalo linatakiwa litibiwa. Zipo njia nyingi ambazo mtu anaweza kuzitumia kujenga hali ya kujiamini, Kwangu mimi yako mambo 10 ya msingi ambayo mtu akiyazingatia na kuyafanyia kazi anaweza kuondokana na hali ya kutokujiamini.
Kuchagua mavazi
Ingawa mavazi hayatafsiri moja kwa moja hali ya mtu, lakini katika lugha ya mawasiliano yasiyokuwa na sauti uvaaji wa mtu ni utambulisho wake. Hivyo kama mtu hazingatii uvaaji unaokubalika katika jamii anakuwa katika wakati mgumu wa kujiamini, hasa kama akilini mwaka yeye mweyewe atatambua kuwa amevaa vibaya.
Hii ina maana kwamba kama mtu anataka kujenga hali ya kujiamini, lazima achague mavazi yanayoendana na mazingira na yawe ni mavazi ambayo mwenyewe akiyafikiria yahatamfanya ajione ni wa tofauti kwa wenzake. Mavazi hujenga muonekano, ukionekana vizuri mbele za watu utajiamini, hivyo kuwa makini na uchaguzi wa mishono ya nguo unazovaa kila siku.
Kutembea haraka
Njia rahisi ambayo imethibitika kuweza kumuondolea mtu hali ya kutokujiamini ni kutembea kwa mwendo wa haraka. Haipendezi unapokuwa njiani kutembea kama mgonjwa, uliyechoka. Ukiwa hivyo ni rahisi sana kuwafanya watu wakukodolee macho ambayo yatakufanya wewe uhisi tofauti. Utemebeaji wa haraka una faida nyingi, lakini kubwa kabisa ni kuwafanya watu wengine wakuone wewe ni mtu wa kazi usiyetaka kupoteza muda wako, mtu makini na mwenye mipamgo. Kitaalamu mwendo unaoruhusiwa ni wa asilimia 25, usizidi sana kiasi cha kuonekana kama unakimbia.
Muonekano sahihi
Namna mtu mwenyewe anavyouweka mwili wake linaweza kuwa ni tatizo la kumfanya ashindwe kujiamni. Kwa mfano,mtu kama si mlemavu lakini akajikuta anatembea miguu upande, mabega juu, kichwa chini au juu sana au kutembea akiwa anadundika kama mpira, ni vibaya kwa vile kitalaamu huchangia kumuondolea mtu ujasiri mbele za watu.
Ushauri wangu ni kwamba mtu anatakiwa kuupa mwili wake umuhimu na kuuweka kama alivyoumbwa, haifai kuwa mtu wa kuinama na kuficha uso, kusimama tenge pale unapoitwa au kuwa mbele za watu. Si vema pia kung�ata kucha, kujipapasa mwilini au kutazama pembeni. Ni vizuri kila mtu kulinda muonekano wake wa asili mbele za wenzake.
Kujizoeza kujiamini
Njia moja muhimu sana kisaikolojia ya kujenga hali ya kujiamini ni kupenda kusikiliza maneno ya kutia moyo nay a ujasiri kutoka kwa watu maarufu. Kwa mfano, viongozi wenye msimamo, watetezi wa haki za binadamu, wanasiasa wanaotetea maslahi ya nchi bila hofu na kadhalika. Hotuba na maneno yao yakipata sehemu kubwa katika akili ya mtu, lazima yatajenga hali ya kujiamini kama wale anaowasikiliza.
Kukubali matokeo
Ifahamike kuwa ukiwaza kwa kina sana juu ya mahitaji yako, zao litakalofuata hapo ni akili kukuletea sababu za kishindwa kufanikisha mambo unayoyataka. Sababu hizo ukizipa nguvu sana ya kuziwaza zitakupa jibu la haiwezekani. Unapokuwa na mawazo yenye mlango huo wa kutokufanikiwa, uwezo wako wa kujiamini hushuka na kujikuta unashindwa katika mambo uyafanyayo. Katika maisha lazima mtu akawa na wakati wa kuachia mawazo yake na kukubaliana na matokeo yaliyopo hasa pale hali ya kushindwa inapokuwa kubwa.
Kupingana na wengine
Mtu akijiona duni mwenyewe ni rahisi kwake kudhani kuwa watu wengine ndiyo wenye mambo ya kweli na hivyo kujikuta akifuata mkumbo na kupotoshwa katika ukweli. Ili mtu aweze kuwa sahihi katika mawazo ya vile ananvyoamini ni lazima awe na tabia ya kupingana na wenzake. Ni jambo baya kukubaliana na watu katika mawazo yao bila kupinga katika kile unachoamini, kufanya hivyo kunaweza kuyafanya maneno ya uongo ya wengine yakaaminika na kuuacha ukweli wa mtu asiyejiamini ukipuuzwa kwa sababu tu hakuwa na ujasiri wa kukabiliana na hoja za wenzake.
7. Pendelea kukaa mbele
Katika kujenga hali ya kujiamini ni vizuri zaidi unapokuwa shule, ofisini, kwenye mikutano, semina ukawa na tabia ya kuketi nafasi za mbele. Ni ukweli kuwa, watu wengi hawapendi kukaa sehemu za mbele kwa sababu ya hofu ya kuonekana kwa urahisi na pengine kuwa wa kwanza kuulizwa au kuchangia hoja, tabia hiyo huondoa hali ya mtu kujiamini. Ili kujenga ujasiri ni vema mtu akapendelea kuketi vitu vya mbele na mara nyingi kuwa wa kwanza katika kufanya mambo.
Zungumza bila aibu
Ukimya wa kupita kiasi nao ni tatizo, hasa pale linapokuja suala la kuogopa kuzungumza mbele za watu kwa hofu ya kuonekana hujui. Wapo wanafunzi na wasomo wengi wanapokutana katika vikundi vya mazungumzo maarufu kama Groups Discusions huwa hawapendi kuzungumza wakilenga kujificha na aibu itokanayo na udhaifu wao katika uelewa. Hata hivyo kutochangia mazungumzo na wengine hakuna faida zaidi ya hasara kwa mtu kutoweza kujiamini. Inashauriwa kwamba ili mtu aweze kujenga hali ya kujiamini ni vema akajenga mazoea ya kuongea mbele za watu bila aibu.
Kujenga afya
Kipengele cha kulinda afya ni muhimu sana kwa mtu anayetaka kujenga hali ya kujiamini. Kukonda au kunenepa sana umbo kunaweza kumfanya mtu akajiona wa tofauti na hivyo kupoteza hali ya kujiamini. Hivyo basi kama unakonda hakikisha kuwa unakula vyakula vyenye vitamini ili kuufanya mwili wako usiwe kituko kwa wengine, hali kadhalika kama unanenepa sana fanya mazoezi ili kuupunguza mwili wako. Tafuta afya ili uwe na nguvu za kufanya mambo kwa umakini.
Msaada kwa wengine
Baada ya kufanikiwa katika hatua zote ambazo tumeziangalia hapo juu, jambo jingine la muhimu katika kuhitimisha uwezo wa mtu kujiamini ni kupata msaada wa mawazo kutoka wa watu wengine ambao ni makini katika maisha yao. Kama kuna jambo ambalo linakuwa gumu katika mawazo yako na limekosa ufumbuzi kiasi cha kukufanya usijiamini, washirikishe wengine wakusaidie na kukutia moyo wa kuendelea kukabiliana na hali yakutojiamini.
Miongoni mwa matatizo makubwa kabisa yanayowakabili wanaume katika suala la kujamiiana ni kufika kileleni mapema. Takwimu zisizo rasmi zinaonesha kuwa, wanaume saba kati ya kumi wanakasoro hii.
Malalamiko yanayotolewa na baadhi yao yanakariri kwamba, muda wa kumaliza tendo huwa kati ya nusu dakika na dakika tatu kwa tendo la kwanza, huku wengine wakimaliza hamu katika hatua za awali tu za hamasa ya kimahaba.
Hata hivyo kumetolewa maelezo na nafuu ya ongezeko la muda katika tendo la pili na kuendelea, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla ya mwanamke limekuwa likiwahuzunisha wanaume walio wengi.
Ndoa na wapenzi wengi wameachana kwa kasoro hii waliyonayo wanaume. Karibu kila kona kunasikika vilio toka kwa wanaume wakilalamika kukabiliwa na tatizo la ufikaji kileleni mapema, ambalo limewafanya waonekane si �keki� kwa wapenzi wao.
Ni ukweli usio pingika kuwa mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya mwenzake humsababishia kero mwanamke anayeshiriki naye tendo, kwani humwacha njia panda pasipokuwa na hitimisho la raha ya kujamiiana.
Hali hii inatokana na maumbile ya mwanaume yanayomlazimisha kusinyaa uume mara baada ya kuhitimisha mbio zake, ingawa kwa mwanamke kuwahi si tatizo, kwani hakumfanyi ashindwe kumsindikiza mwenzake hadi kileleni.
Pengine utofauti huu ndiyo unaowafanya wanaume wahuzunike zaidi wanapokabiliwa na janga hilo kiasi cha kufikia hatua ya kwenda kwa waganga kutafuta tiba ya miti shamba ili iwasaidie kuepuka balaa ya kutoka uwanjani na aibu.
Ingawa kumekuwa na mafanikio katika tiba asili, lakini bado wanaume wameshindwa kupata ukombozi wa kudumu wa tatizo hili. Wengi wamejikuta wakijiongezea mzigo wa fikra kwa kuzitumaini zaidi dawa, jambo ambalo huwalazimisha kuzitumia kila wanapofanya tendo na ikitokea hawakuzipata, aibu hubaki pale pale.
Kwa kufahamu mikinzamo iliyopo kati ya akili na tiba ya nguvu za kiume na madhara yachipukayo imebainika kuwa, mtu anaweza kujitibu tatizo hilo kwa kutumia kanuni za kisaikolojia, badala ya dawa na mafaniko yasiyo na madhara yakapatikana.
Kimsingi kanuni ya ufanyaji mapenzi iko zaidi kwenye ubongo kuliko mwilini. Kinachotokea hadi mtu akapata msisimko wa kufanya mapenzi si mwitikio wa mwili, bali ni utambuzi wa akili juu ya kiwango cha mwanamke anayefaa kimapenzi.
Inaelezwa kuwa, akili ikishiba vigezo na kutuma taarifa zenye usahihi kwenye mwili viungo hupokea hisia na kuanza kusumbua. Kwa msingi huo kama tunataka kufika kileleni mapema au kuchelewa lazima tucheze zaidi na akili kuliko mwili.
Katika hali ya kawaida nguvu ya kupenda inayomwingia mtu huwa kubwa, lakini suala la kupunguza ukubwa wa hisia lazima lipewe kipaumbele. Jambo kubwa linalowasumbua wanaume wengi wenye tatizo la kufika kileleni mapema ni kuwa na PUPA ya kufanya ngono.
Wengi wao hupokea hisia zilizokuzwa na kwenda nazo katika ufanyaji wa tendo la ndoa. Wataalam wa saikolojia wanasema ili mwanaume achelewe kumaliza, lazima apunguze mhemko unaotokana na kuona, kuhisi na kupagawishwa na staili au chombezo toka kwa mwanamke.
Anachotakiwa kufanya ni kutumia zaidi ya dakika 20 kufanya maadalizi na mpenzi wake kabla ya kuanza tendo. Hii itasaidia kuufanya mhemko wake ushuke na kumuongezea muda wa kumaliza.
Aidha mbinu ya kuidanganya akili lazima itumike ili kuzima taarifa za juu za uzuri wa mwanamke, maumbile na raha ya starehe isipokelewe kwa nguvu kubwa mwilini. Hii ikiwa na maana kuwa kuna kipindi inabidi fikra za mwanume zisihamasike sana kwenye tendo badala yake iletwe mawazoni hali ya kawaida, si ile ya kuweweseka na kuhema hema hovyo. Yafuatayo ni maelekezo ya msingi ya kufanya, ili mtu asifike kileleni mapema:
Mume na mke wanapoingia katika uwanja wa mapenzi wakae kwanza kwa muda, huku wakiwa wamejiachia na mavazi mepesi. Pili wacheze michezo mingi kwa muda mrefu bila kuanza kazi yao. Wakiwa kwenye hamasa hizo wasiwe kimya bali wazungumze na kuulizana maswali ya kimahaba.
Baada ya hapo mbinu nyingine ya kuzuia mbegu za kiume zisitoke ni ile ya kujibana. Inashauriwa kuwa mwanaume akiona dalili za awali za kumaliza bila kujali ametumia muda gani anachotakiwa kufanya ni kukaza misuli ya miguu na kuzuia mbegu kwa mtindo atumiao kuzuia haja ndogo isitoke.
Kujibana huko kunatakiwa kuende sambamba na kuacha kucheza �shoo�. Pacha na hilo mwanaume anatakiwa kuidanganya akili kwa kuilazimisha iwaze jambo jingine hasa la kuhuzunisha ili kuharibu taarifa za raha zilizotumwa mwilini zisiendelee kufanyiwa kazi na hatimaye kumaliza tendo haraka.
Zoezi hili linaweza kuwa gumu katika hatua za kwanza kutokana na kukosea muda sahihi wa kujizuia, lakini mhusika akiendelea kujizoeza atajikuta anaweza na kupata uwezo wa kufanya mapenzi hata kwa saa nzima, hivyo kuondokana na tatizo hilo bila tiba wala madhara.
Njia 10 za kuimarisha kumbukumbu kichwani
Miongoni mwa hazina muhimu kwa mwanadamu ni kuwa na uwezo wa kukumbuka vitu kwa urahisi. Wanafunzi wengi hushindwa kufanya vizuri mitihani yao kwa sababu ya kukabiliwa na tatizo la usahaulifu, ambao huchochewa na mambo mengi ukiwemo ulevi wa pombe, utumiaji wa dawa za kulevya na msongo wa mawazo ya kimaisha.
Licha ya uwezo wa kumbukumbu kupungua kutokana na umri wa mtu, sayansi yaitegemei kijana mwenye umri wa chini ya miaka 28 kukabiliwa na tatizo hili kwa kiwango kikubwa, ingawa wale wenye miaka zaidi ya 40 wanatajwa kuzorota katika uwezo wa kukumbuka mambo.
Hata hivyo uchunguzi unaonesha kuwa watu ambao huzingatia suala la kanuzi za afya zikiwemo mbinu za kukuza kumbukumbu ya akili hupunguza kwa kiasi kikubwa mmeng�enyeko wa seli zinazojenga uwezo wa akili katika kutunza kumbukumbu. (Susan Tapert mwanasaikolojia kutoka Chuo cha California San Diego na kituo cha VA San Diego nchini Marekani anathibitisha haya pia).
Hivyo basi, ili mwanafunzi aweze kuwa na uwezo wa kutunza vema mambo anayosoma na kufundishwa na waalimu wake darasani lazima aweze kuiongezea akili yake uwezo wa kutunza kumbukumbu kwa kufanya yafuatayo:
1 . LISHE BORA
Ni wazi kuwa wengi wetu tunafahamu maana ya lishe bora, lakini kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo cha American Academy of Neurology kinachojihusisha na mambo ya neva, ulibaini kuwa machungwa, Spinachi, Karoti, brokoli (aina fulani ya mboga kama kabichi), viazi vitamu na mboga mboga huuongezea uhai ubongo na kumfanya mwanadamu asiweze kushambuliwa na magonjwa wa kupooza.
Aidha matunda na vyakula vyenye vitamini B, Foliki Asidi (folic acid), Niasini (niacin) Kalkumini (curcumin) husaidia kuufanya ubongo uwe na mawasiliano ya kutosha na viungo vingine vya mwili na kupunguza kwa asilimia 11 uhalibifu wa seli ndani ya ubongo. (Utafiti wa National Research Council nchini Milan, Italy unathibitisha kuwa vyakula vyenye Vitamini C na E hupunguza kiwango cha usahaulifu)
2. MAZOEZI YA MWILI
Ufanyaji wa mazoezi ya mwili huimarisha misuli na kusaidia akili kuweza kufanya kazi vema, hii inatokana na ukweli kwamba tunapofanya mazoezi tunakuwa tunaongeza msukumo wa damu mwilini na hivyo kuufanya ubongo kufikiwa na damu ya kutosha ambayo ni muhimu kwa uimara wa kumbukumbu.
Mara nyingi, mazoezi yanayofaa zaidi kwa afya ya mwili na uimarisha wa ubongo ni yale ya asubuhi na jioni. Kuhusu aina ya mazoezi inategemea na umbo la mtu, lakini kukimbia, kuruka kamba, kucheza mpira na hata kuinua vitu vizito vinavyolingana na uwezo wa mtu ni bora kwa afya. Mazoezi ya aina hii yakifanywa na wanafunzi yanaweza kuwasaidia pia kutunza kumbukumbu za masomo wanayofundishwa.
3 : MAZOEZI YA AKILI
Ni muhimu kwa mwanafunzi kuwa na mazoea ya kuifanyisha akili yake mazoezi ya kutunza kumbukumbu kwa kuingiza kichwani mambo ambayo hakuyazoea na kuyafanyia mazoezi ya kuyakumbuka. Kwa mfano mwanafunzi anaweza kundika namba zisizopungua 14 na kuanza kuzitaja kwa kufuta mpangilio aliojiwekea.
Namba zinatakiwa ziandikwe kwa kuchanganywa si kwa kuzifuatanisha kwa mtindo wa kuhesabu. Mfano, 23938393835575, baada ya kuziandika kwa mfumo huo mwanafunzi atatakiwa kuzikariri kwa dakika tano kisha kufumba macho au kutazama pembeni na kuanza kuzisoma kwa kufuata mfululizo huo, huku akihakikiwa na mtu mwingine. Mazoezi haya yatamsaidia kuondoa tatizo la kusahau na kumpa kipimo ni kwa kiwango gani hana uwezo wa kukumbuka.
Endapo mwanafunzi atashindwa kufikia kiwango cha zaidi ya nusu ya namba alizojiwekea afahamu kuwa ana uwezo mdogo wa kutunza kumbukumbu hivyo anatakiwa kuongeza juhudi za kujiimarisha.
Njia nyingine ya kuifanyisha mazoezi akili ni kujifunza mara kwa mara mambo mapya, ikiwa ni pamoja na kuimba nyimbo kwa lugha ya kigeni, kujifunza lugha za makabila mengine, kutembelea mitandao mbalimbali ya intaneti na kusoma, kucheza michezo ya kwenye simu na kompyuta.
Aidha usomaji wa vitabu, urudiaji wa mara kwa mara wa notisi za darasani, husaidia kuongeza msukumo wa akili katika kutunza kumbukumbu kichwani. Hata hivyo tafiti nyingi zinaonesha kuwa uhudhuriaji wa majadala na uongeaji wa mambo ya msingi mbele ya watu wengi huimarisha uwezo wa mtu kukumbuka mambo kwa urahisi.
4. UTUMIAJI WA VINYWAJI
Vinywaji kama kahawa, chai nyeusi navyo huchangia kuongeza uwezo wa ubongo kutunza kumbukumbu. Inashauriwa kwa mwanadamu kutumia walau kikombe kimoja cha vinywaji hivyo ili kuongeza enzymes ambazo ni muhimu kwa kuuongezea nguvu ubongo ili uweze kutunza kumbukumbu. Hata hivyo vinywaji vikali kama pombe haviruhusiwi kwani huchangia kudumaza uwezo wa kukumbuka.
5. PUNGUZA MSONGO WA MAWAZO
Ubongo unaweza kushindwa kutunza kumbukumbu endapo mtu husika atakuwa na msongo wa mawazo yatokanayo na shida za kidunia. Endapo mwanafunzi atakuwa mtu mwenye kuutumikisha ubongo wake katika mawazo yenye kuumiza kila wakati, hawezi kuwa na uwezo wa kukumbuka anayofundishwa.
Hivyo ni vema kupunguza mawazo kwa kuwashirikisha wengine magumu unayokutana nayo maishani na kukubali kuyaacha yapite ili yakupe nafasi ya kuishi kama wewe. Hatari ya msongo wa mawazo ni kuongeza kiwango cha seli za cortisol ambayo huharibu ubongo wa kati ambao ni muhimu kwa kutunza kumbukumbu.
6. KULALA
Watu wengi wakiwemo wanafunzi wamekuwa wakipuuza usingizi kwa kusoma sana usiku na kuacha kupumzisha miili yao kwa kulala, jambo ambalo hili ni hatari kwa utunzaji wa kumbukumbu kichwani.
Ifahamike kuwa usingizi ni kama chujio la akili ya mwanadamu, ambapo mtu anapolala mchakato hufanyika akilini kwa kuyachambua mamilioni ya mambo ambayo mhusika aliyaona, kuyasikia, kuhisi na pengine kuyatenda. Mchakato huo huweza kuchuja mambo mabaya na kuyatupa na mema huhifadhiwa kwenye kumbukumbu.
Hivyo, kama mwanafunzi hatolala, mambo yote yakiwemo ya kipuuzi aliyofanya mchana yatabaki kwenye akili yake na kama mtindo huo wa kutolala utaendelea unaweza kuufanya ubongo uchoke na kupoteza kumbukumbu ya mambo muhimu yakiwemo ya shuleni.
Utafiti uliofanywa mwaka 2008 na Chuo cha Pennsylvania ulionesha kuwa wanafunzi wanaolala kwa saa 6 kwa siku huwa na kumbukumbu nzuri zaidi ya wale wanaolala kwa kiwango cha chini ya saa hizo. Utafiti wa aina hii ulifanywa pia na Chuo Cha Luebeck na kubainisha kuwa akili huongezewa uwezo mara tufu kwa kutunza kumbukumbu pale mtu anapokuwa analala usingizi mnono.
7. TUMIA MUZIKI
Muziki unatajwa kuwa na faida katika kumsaidia mtu kukumbuka mambo yaliyopita, inawezekana kabisa kwa kupita wimbo ukakumbuka mambo ambayo uliyafanya siku za nyuma. Hivyo kuufurahisha mwili kwa kucheza muziki, kusikiliza nyimbo, kunaweza kuongeza uwezo wa mtu kukumbuka mambo. Hata hivyo kujifunza lugha au jambo fulani kwa njia ya wimbo ni rahisi kukumbuka kuliko kuhifadhi maneno yenyewe.
8. KUANDIKA
Ni muhimu kwa mwanafunzi kuwa na kumbukumbu za pembeni nikiwa na maana ya maandishi ya mkono. Ni muhimu kuorodhesha mambo ambayo umekusudia kuyafanya au yalikutokea kwa kuyaandika kwenye kitabu kidogo cha kumbukumbu. Mfano, unaweza kuandika siku uliyoanza shule, uliyozaliwa, tarehe uliyomaliza darasa la saba n.k.
9. ONDOA HOFU
Kuna wanafunzi wengine hushindwa kukumbuka mambo si kwa sababu akili imesahau, bali wanajichanganya kwa hofu na kutojiamini kwamba wanachokumbushwa na akili kwa wakati huo kiko sahihi. Hivyo ni wajibu wa mtu kujiamini na kutupilia mbali wasi wasi wote unaojitokeza wa kuhofu kuchekwa au kutofanya vizuri katika jambo lililopo mbele yake.
10. AFYA
Jambo la mwisho ambalo ni muhimu katika uimarishaji kumbukumbu za kichwani ni mtu kuwa na afya kwa maana ya kuhakikisha kuwa anatibiwa magonjwa yake na anakuwa mfuasi mzuri wa huduma za kitabibu kwa ajili ya kuuwesha mwili wake ufanye kazi kama unavyokusudia.
NAMNA YA KULIONDOA TATIZO LA KUWAHI KUMALIZA KATIKA TENDO LA NDOA
Miongoni mwa matatizo makubwa kabisa yanayowakabili wanaume katika suala la kujamiiana ni kufika kileleni mapema. Takwimu zisizo rasmi zinaonesha kuwa, wanaume saba kati ya kumi wanakasoro hii.
Malalamiko yanayotolewa na baadhi yao yanakariri kwamba, muda wa kumaliza tendo huwa kati ya nusu dakika na dakika tatu kwa tendo la kwanza, huku wengine wakimaliza hamu katika hatua za awali tu za hamasa ya kimahaba.
Hata hivyo kumetolewa maelezo na nafuu ya ongezeko la muda katika tendo la pili na kuendelea, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla ya mwanamke limekuwa likiwahuzunisha wanaume walio wengi.
Ndoa na wapenzi wengi wameachana kwa kasoro hii waliyonayo wanaume. Karibu kila kona kunasikika vilio toka kwa wanaume wakilalamika kukabiliwa na tatizo la ufikaji kileleni mapema, ambalo limewafanya waonekane si �keki� kwa wapenzi wao.
Ni ukweli usio pingika kuwa mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya mwenzake humsababishia kero mwanamke anayeshiriki naye tendo, kwani humwacha njia panda pasipokuwa na hitimisho la raha ya kujamiiana.
Hali hii inatokana na maumbile ya mwanaume yanayomlazimisha kusinyaa uume mara baada ya kuhitimisha mbio zake, ingawa kwa mwanamke kuwahi si tatizo, kwani hakumfanyi ashindwe kumsindikiza mwenzake hadi kileleni.
Pengine utofauti huu ndiyo unaowafanya wanaume wahuzunike zaidi wanapokabiliwa na janga hilo kiasi cha kufikia hatua ya kwenda kwa waganga kutafuta tiba ya miti shamba ili iwasaidie kuepuka balaa ya kutoka uwanjani na aibu.
Ingawa kumekuwa na mafanikio katika tiba asili, lakini bado wanaume wameshindwa kupata ukombozi wa kudumu wa tatizo hili. Wengi wamejikuta wakijiongezea mzigo wa fikra kwa kuzitumaini zaidi dawa, jambo ambalo huwalazimisha kuzitumia kila wanapofanya tendo na ikitokea hawakuzipata, aibu hubaki pale pale.
Kwa kufahamu mikinzamo iliyopo kati ya akili na tiba ya nguvu za kiume na madhara yachipukayo imebainika kuwa, mtu anaweza kujitibu tatizo hilo kwa kutumia kanuni za kisaikolojia, badala ya dawa na mafaniko yasiyo na madhara yakapatikana.
Kimsingi kanuni ya ufanyaji mapenzi iko zaidi kwenye ubongo kuliko mwilini. Kinachotokea hadi mtu akapata msisimko wa kufanya mapenzi si mwitikio wa mwili, bali ni utambuzi wa akili juu ya kiwango cha mwanamke anayefaa kimapenzi.
Inaelezwa kuwa, akili ikishiba vigezo na kutuma taarifa zenye usahihi kwenye mwili viungo hupokea hisia na kuanza kusumbua. Kwa msingi huo kama tunataka kufika kileleni mapema au kuchelewa lazima tucheze zaidi na akili kuliko mwili.
Katika hali ya kawaida nguvu ya kupenda inayomwingia mtu huwa kubwa, lakini suala la kupunguza ukubwa wa hisia lazima lipewe kipaumbele. Jambo kubwa linalowasumbua wanaume wengi wenye tatizo la kufika kileleni mapema ni kuwa na PUPA ya kufanya ngono.
Wengi wao hupokea hisia zilizokuzwa na kwenda nazo katika ufanyaji wa tendo la ndoa. Wataalam wa saikolojia wanasema ili mwanaume achelewe kumaliza, lazima apunguze mhemko unaotokana na kuona, kuhisi na kupagawishwa na staili au chombezo toka kwa mwanamke.
Anachotakiwa kufanya ni kutumia zaidi ya dakika 20 kufanya maadalizi na mpenzi wake kabla ya kuanza tendo. Hii itasaidia kuufanya mhemko wake ushuke na kumuongezea muda wa kumaliza.
Aidha mbinu ya kuidanganya akili lazima itumike ili kuzima taarifa za juu za uzuri wa mwanamke, maumbile na raha ya starehe isipokelewe kwa nguvu kubwa mwilini. Hii ikiwa na maana kuwa kuna kipindi inabidi fikra za mwanume zisihamasike sana kwenye tendo badala yake iletwe mawazoni hali ya kawaida, si ile ya kuweweseka na kuhema hema hovyo. Yafuatayo ni maelekezo ya msingi ya kufanya, ili mtu asifike kileleni mapema:
Mume na mke wanapoingia katika uwanja wa mapenzi wakae kwanza kwa muda, huku wakiwa wamejiachia na mavazi mepesi. Pili wacheze michezo mingi kwa muda mrefu bila kuanza kazi yao. Wakiwa kwenye hamasa hizo wasiwe kimya bali wazungumze na kuulizana maswali ya kimahaba.
Baada ya hapo mbinu nyingine ya kuzuia mbegu za kiume zisitoke ni ile ya kujibana. Inashauriwa kuwa mwanaume akiona dalili za awali za kumaliza bila kujali ametumia muda gani anachotakiwa kufanya ni kukaza misuli ya miguu na kuzuia mbegu kwa mtindo atumiao kuzuia haja ndogo isitoke.
Kujibana huko kunatakiwa kuende sambamba na kuacha kucheza �shoo�. Pacha na hilo mwanaume anatakiwa kuidanganya akili kwa kuilazimisha iwaze jambo jingine hasa la kuhuzunisha ili kuharibu taarifa za raha zilizotumwa mwilini zisiendelee kufanyiwa kazi na hatimaye kumaliza tendo haraka.
Zoezi hili linaweza kuwa gumu katika hatua za kwanza kutokana na kukosea muda sahihi wa kujizuia, lakini mhusika akiendelea kujizoeza atajikuta anaweza na kupata uwezo wa kufanya mapenzi hata kwa saa nzima, hivyo kuondokana na tatizo hilo bila tiba wala madhara.
Njia za kutafuta na kupata furaha
Miongoni mwa vitu muhimu katika maisha ya mwanadamu ni kupata furaha. Watu wengi wamekuwa na harakati nyingi za kuhakikisha kuwa wanafurahika katika kuishi kwao. Kuna wanaotafuta furaha kupitia kwa rafiki, wapenzi, ndoa zao na hata jamii zao. Ni wazi kwamba kila afanyalo mwanadamu kupitia maamuzi yake, msingi wake huwa ni kutafua furaha, hii haijalishi kama atafanya jambo mbaya au zuri kwa mtazamo wa watu.
Ifahamike, watu wanavuja jasho katika kufanya kazi kwa sababu wanahitaji mshahara au pato ambalo baadaye hulitumia katika kufurahi. Wasomi, wafanyabiashara nao wanapohangaka katika hili na lile ukichunguza utakuta nyuma yao kuna kiu ya furaha.
Hii ina maana kuwa, furaha ndiyo jambo pekee ambalo watu hulitafuta zaidi. Ni nadra au pengine hakuna mtu ambaye kwa akili timamu ana kiu ya kupata mabaya na kuhangaika kuyatafuta. Mara nyingi yakimtokea basi huwa yamejitokeza tu katika safari yake ya kutafuta furaha. Wezi, majambazi, wazinifu hata watukanaji wote kwa pamoja wanapofanya hivyo huwa nyuma yao kuna hitaji la kupata furaha.
Pamoja na shabaha ya binadamu kuwa katika kutafuta furaha, wengi wao wamekuwa hawaipati kwa sababu hawajui njia za kuipata. Kuna watu wanahangaikia utajiri, wakidhani wakiupata, basi watakuwa na furaha, lakini baada ya kupata utajiri huo hujikuta hawana furaha. Wengine huamua kuoa, kuwa na wapenzi na marafiki lakini nao matokeo huwa tofauti na malengo.
Ingawa kuna matatizo mengi ambayo yanajitokeza katika maisha ya watu kila siku ambayo huondoa furaha, lakini si sababu ya moja kwa moja ya kumfanya mtu ahuzunike, eti tu kwa maana kafikwa na tatizo. Ukichunguza kwa makini utafahamu kuwa furaha si kitu ambacho mtu anaweza kukipata na kikamtosha. Unaweza kupata kila kitu lakini ukawa huna furaha.
Ukisema pesa ndiyo furaha, unaweza kuzipata lakini usifurahike na ukashangaa watu ambao ni masikini wakawa na furaha tele. Hivyo basi msingi wa furaha ni uelewa wa namna ya kuitafuta na kuipata. Swali, furaha inapaika wapi na katika vitu gani? Nibu ni kuishi kwa kuzingatia muongozo ufuatao:
Unaitafutaje furaha?
Watu wengi wanapopata matatizo huwa hawakubali kuyapokea. Kuna mfano wa mtu mmoja ambaye alikuwa bosi katika kampuni, siku moja uongozi wa juu uliamua kumshusha cheo kutoka ukurugenzi hadi mpokea wageni. Bosi huyo alipotelemshwa cheo kwa kiwango hicho hakujiona duni kwa wafanyakazi wenzake, badala yake alichofikiri yeye ni kwamba watu wote wanamuunga mkono na kumsikitikia kwa unyama huo wa kushushwa cheo kupitiliza.
Zile fikra za kuhurumiwa na watu zilimfanya awe na furaha na akawa mtu wa kuwahi kazini kila siku ili watu wakamuone na kumsikitia, jambo ambalo aliamini kuwa uongozi uliomshusha cheo ndiyo unaopata aibu mbele ya jamii na wala sio yeye. Kitendo hicho cha kuwahi kazini na kuonekasna ni mtu mwenye furaha kilimfanya awe mtu wa pekee kwenye jamii, aliweza kutengeneza maswali mengi kwa watu na hatimaye minong’ono ya kuonewa ilianza kusikika.
Kilichotokea hatimaye, kampuni moja kubwa ilipata habari ya kuwepo kwa mtu wa aina hiyo, ikafanya mawasiliano naye na kumwajiri, bila kujali kashfa zilizokuwa zimemwengua katika wadhifa wake wa kwanza. Jamaa huyo alipopata ajira mpya alijirekebisha makosa yake ya kugushi na wizi kwa vile alikuwa amejifunza kilichokuwa kimempata. Bosi huyo aliweza kuendesha kampuni hiyo kwa mafanikio makubwa, jambo lililowafanya wakuu wake wa zamani wajute kumuondolea wadhifa.
Hapa tunajifunza kuwa tunapopata matatizo kinachotufanya tupoteze furaha ni fikra zetu, lakini tukijua kucheza nazo na kuzielekeza katika mlango wa pili, tunaweza kuyatumia matatizo yetu kupata furaha pia. Lazima kila mmoja wetu atambue kuwa matatizo ni shule, tunapoyapata tunajifunza. Lakini hatuwezi kujifunza tukiwa na msongo wa mawazo, lazima tufanye unafiki fulani wa kimawazo kama alioufanya bosi aliyeshushwa cheo, yeye hakuangalia wadhifa wake wa zamani, wala namna gani watu wanamtazama katika kazi yake mpya. Mawazo yanawezaje kutuletea furaha?
Katika hali ya kawaida hakuna mtu hata mmoja anayeweza kumwambia mwenzake lia naye akafanya hivyo. Kila siku tunaona na kusikia mengi kutoka kwa ndugu, rafiki, waalimu wahubiri, wachungaji mapadri wetu na hata kwenye vyombo ya habari, lakini kusikia huko hakuna maana kuwa ni lazima kutuondolee furaha, kwani ndani ya akili zetu kuna kitu muhimu ambacho ni maamuzi yetu.
Utawala wa mawazo yetu ni kazi ya kila siku na uamauzi wa nini ha kufikiri ni suala ambalo lipo kwenye uwezo wa mwanadamu mwenyewe. Ingekuwa ni lazima kila wazo baya tunaloliona na kulisikia lazima lituhuzunishe basi tusingekuwa na furaha hata kidogo katika maisha yetu, kwani hakuna siku ambayo itapita bila kuona, kusikia au kutendewa jambo baya na mtu mwengine.
Ajali zinatokea kila siku, watu wanakufa, wanaugua, wanateseka, wanalia, wanaomboleza na kufanyiana hila, lakini kwa nini hatuyachukulii matukio yote kwa uzito sawa kiasi ha kulia? Ni kwa sababu tuna uhuru wa kuchagua tulie kwa sababu ya nani na kwa nina? Na hii ndiyo silaha pekee ya kuyatumia mawazo kutuletea furaha. Yaani kuchagua lipi la kutuliza na lipi la kutufurahisha na mwisho wa yote tuna uwezo wa kuyatumia mawazo yetu kuchagua mambo ya kufurahisha na kuyapa kipaumbele, bila kujali ni mema au mabaya. (Kumbuka mfano wa bosi aliyeshushwa cheo).
Hivyo ni vema wakati tunapokuwa na mawazo ndani yetu tukazingatia misingi ifuatayo ambayo inaweza kutusaidia kufikia uamuzi sahihi juu ya kila tunaloona na kulisikia, ili mawazo yasitufanye tuhuzunike na badala yake tufurahi. Kwanza ni kujipenda wenyewe. Tukijipenda hatutajihukumu na kujiona duni mbele ya wenzetu na hivyo kutopoteza furaha. Pili ni kujiamini, kuamini huku kutatuwezesha kuwa na msimamo juu ya maamuzi ya kila tunachoshibishwa ndani ya mawazo yetu kupitia mawasilia ya sauti na yasiyo na sauti.
Tatu, kumiliki mawazo yetu yasichukuliwe na ukubwa au udogo wa tatizo. Udhibiti huu lazima uyaone mambo yote yanayoingia kichwani kuwa ni ya kawaida kwa vile yapo duniani na yanawakuta watu kama sehemu ya changamoto za kimaisha. Katika hali ya kawaida ukubwa au udogo wa tatizo unatokana na mawazo ya mtu husika. Nne, kuwa na uvumilivu juu ya kila jambo kwa imani kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Tano na mwisho ni kuhakiki maamuzi yetu kama yako sahihi kabla na baada ya kutenda jambo.
Kutojiheshimu kunavyohatarisha furaha yetu?
Ni muhimu kila mtu akaishi kama yeye alivyo, lakini linapokuja suala la kuchangamana na ulimwengu, lazima kuwe na kitu cha kujifunza kwa sababu huwezi kuishi nje ya familia na watu wengine.
Kwa msingi huo ili mtu aweze kupata furaha lazima afahamu namna atakavyoweza kujisahihisha tabia yake kwa kujiheshimu yeye na kuwaheshimu wengine anaoishi nao. Kwa maana kuishi kama mtu anatakavyo bila kutazama wengine ni jambo baya. Hivyo dokezo zifuatazo ni muhimu kwa kila mtu kuzifahamu ili kuondoa mkwaruzano kati ya mtu na mtu.
A –Wafanyie wengine mema
Furaha haiwezi kuja kama mtu hajiheshimu mwenyewe na kuwafanyia wengine mema ambayo angependa atendewe. Watu wengi wamekuwa hodari kutembea na wake za watu, kuiba, kudhuru, kutukana, kudharau wengine na hata kunyanyasa, bila kugeuza upande wapili wa shilingi na kufikiri endapo wangefanyiwa wao hali ingekuwaje, si wangepoteza furaha? Sasa kama jibu ni ndiyo kwa nini wao wawe mahodari kuwaumiza wengine? Ni wazi kwamba kila mwanadamu angekuwa makini kufanya yale ambayo angependa kufanyiwa, kiwango ha huzuni kingepungua, na hii ndiyo changamoto kubwa kwa mtu atakaye kupata furaha lazima awafanyie wengine wema kwanza kabla ya yeye kufanyiwa.
B – Kuwa kiongozi
Katika maisha kuna watu ambao hawaelewi kuhusu matumizi ya mawazo na namna ya kutenda kama binadamu, hivyo kwa wale ambao wanaelewa nini maana ya maisha ni vema wakawa viongozi kwa wengine, viongozi katika kusamehe, kukubali kosa, kutenda haki na kusimamia ukweli.
C- Kushukuru
Ni watu wachache sana ambao hushukuru wafanyiwapo mabaya, lakini inashauriliwa kwamba ili kuuita furaha na kupunguza nguvu ya huzuni ni bora mtu akajifunza kushukuru hata kama amefanyiwa jambo baya.
D - Kuwa na juhudi
Mambo yote tunayoyafanya lazima yaambatane na juhudi. Ikiwa tunatafuta majibu ya nini tunataka kifanyeke katika kupata furaha lazima tuwe na bidii, tusifanye vitu kwa uzembe kwani matokeo yake ni kushindwa ambako kutatuingiza katika shida ambazo zitatuhuzunisha. Umeolewa jitahidi kulinda ndoa yako, jitahidi katika kazi na kila jambo ili usikwame.
E- Kuchunga ulimi
Kuna watu wengi ambao wanapoteza furaha kwa kutojua namna ya kutumia ndimi zao. Utakuta mtu yuko katika kati ya watu, anatukana na wakati mwingine kutamka maneno ambayo wenzake hayawapendezi. Kujiheshimu ni pamoja na kuchuja maneno ya kusema mbele za watu kulingana na mahitaji yaliyopo, kuropoka ropoka kuna madhara. Kabla hujasema kitu tafakari kama usemecho kitaleta furaha au huzuni.
Kanuni za kuifikia furaha ya kweli
Wakati wa kutafuta furaha ya kweli lazima kujiuliza baadhi ya kanuni za kimaisha kama unazifuata kwa ufasaha, vinginevyo unaweza kuwa mtafuta furaha lakini usiwe miongoni mwa wanaoipata. Kama nilivyosema awali kuwa, kuna watu hutafuta furaha kupitia kwa wake/waume zao, rafiki, wapenzi na hata kwenye mali, lakini mwisho wa siku wanapokuja kutafakari zaidi hujikuta hawana furaha waliyoitaraji wakati wakihangaikia njia za kuipata.
Kuna watu ambao mawazo yao yanatamani sana kupata mtoto na wengine wameapa kabisa kwamba wakifanikiwa kushika ujauzito watakuwa na furaha, lakini bado kama hawatakuwa makini wao wenyewe watajikuta wanapata furaha ya muda na hatimaye kutoweka na kuanza kujutia harakati zao, huku wakianza safari mpya za kufuata furaha kupitia jambo jingine. Hebu tujiulize maswali haya.
A-Je tunapokuwa tunatafuta furaha tunatumia uwezo wetu wote au kwa kiwango kidogo? Kama tunatumia kiwango kidogo basi tujue kuwa hata kama tutapata kitu tunachodhani kitatufurahisha utajikuta hatufurahi, kwa sababu hatutafanikiwa au tutakuwa na furaha ya muda tu kwa vile nia yetu hatukuijaza kikamilifu ili tuweze kupata furaha timilifu
B- Je tunafanya sawa katika maamuzi au tunabahatisha tu? Endapo tutakuwa tunafanya mambo ya kubahatisha ambayo hatujayahakiki, huzuni yetu itakuwa kwenye makosa na kamwe hatuwezi kufanikiwa kupata yale tunayotaraji yatufurahishe. Kuna watu wanatafuta watoto lakini hawazingatii kalenda za mimba na wengine wanatafuta mali, elimu kubwa, mke mwema, lakini hawako makini katika kufanya maamuzi kwa usahihi. Ni vema tukathibitisha uchaguzi wa mambo ili tufanikiwe kupata yatakayotufurahisha.
C- Je tunatimiza wajibu wetu au tunadanganya? Wapo watu ambao walitamani kuoa ili wapate furaha, lakini walipofanikiwa katika hilo hawakutimiza majukumu yao wakajikuta wanageukwa na wake/waume zao na kujutia uamuzi wao. Msomaji wangu, unapokuwa katika safari ya kutafuta furaha kupitia utajiri, elimu, uongozi ni vema ukatimiza wajibu wako, ili upate matokeo mazuri. Maana kama utakuwa unatamani kufaulu mtihani wako halafu husomi kwa bidii, sina shaka majibu utakayopata yatakuhuzunisha kwa sababu lazima ufeli na furaha uliyotaka haitapatikana.
D- Je tunafuata muongozo, au tunakiuka? Kila jambo tunalotaka kulifanya lina kanuni zake, ukitaka kupika ugali upo muongozo ambao unakutaka uwe na vifaa, uache maji yachemke na hata kutoharakisha upishi wenyewe, lengo ni kupata matoke mazuri. Sasa kama tutakuwa kupata furaha ya kudumu kupitia mambo fulani ni lazima tuyafanye kwa kufuata muongozi na si kwa kukurupuka. Biashara, elimu, kazi, zote hizi zinamiongozo ambayo lazima kuifuata kwa matokeo mazuri.
E- Tunatumia tulivyopata au tunavitelekeza? Wapo watu ambao hutamani kupata kazi, lakini wanapopata hawazitumii, kazi hizo kwa ukamilifu, badala yake wanakuwa watu wa kufanya ujanja ujanja ujanja kwa kutoroka na wakati mwingine kutojihusisha na shughuli nyingine kwa lengo lile lile la kutafuta furaha. Kusema kweli mtu wa namna hii hawezi kuwa na furaha kwa sababu anayolenga yamfurahishe hayatumii kufurahika na badala yake anatafuta jambo jingine. Fikiria kuhusu mume, anaoa lakini anaacha kumtumie mke wake wake anakwenda kwa hawara! Hili si jambo jema na kamwe haliwezi kuleta furaha kupitia mambo tunayoyatafua. Soma vifungu hivi ndani ya kitabu cha Biblia: “Vitu vyote ni halila, bali si vitu vyote ifaavyo. (1 Wakorintho 10:23).” “ Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi (Yakobo 4:17)”
VYANZO VITANO VYA BAHATI MBAYA
“Alikuwa anavuka barabara, lakini kwa bahati mbaya akagongwa na gari.” “Nimemaliza masomo yangu mwaka jana, lakini kwa bahati mbaya nikafeli.” Kwa bahati mbaya biashara yangu ilisambaratika.” “Kwa bahati mbaya alifukuzwa kazi.” Imetokea kwa bahati mbaya” Nimebata bahati mbaya Mume wangu hanifai hata kidogo.” “Kwa bahati mbaya alijifungua mtoto aliyekufa”
Hizi ni baadhi kauli za baadhi ya watu ambao ni wafuasi wakubwa wa kitu kinachoitwa bahati mbaya katika maisha yetu ya kila siku. Hebu tujifunze vyanzo vya bahati mbaya na namna ya kuepukana nayo, ili tusijikute kila siku tunalaumu kupatwa na bahati mbaya kumbe makosa ni yetu na kwamba hatukuwa makini katika kuishi kwetu.
UZEMBE WA KUFIKIRI
Watu wengi wanaoamini kuwepo kwa matukio ya bahati mbaya katika maisha wanaelezwa na wataalamu kuwa na kasoro katika upeo wa kufikiri vyanzo vya mambo. Inasemwa na watafiti wengi kuwa matukio mabaya yaliyopata kuripotiwa ulimwenguni ni matokeo ya uzembe wa kufikiri na kuamua. Kwa maana hivyo inashauriwa kuwa mtu anayetaka kuepukana na bahati mbaya lazima awe hai katika fikra, hasa upataji wa jibu la mapema juu ya nini kitatokea katika kutenda kwake.
Inampasa mvuka barabara kwa mfano, ajiuliuze matokeo ya kuvuka kwake na apate majibu chanya na hasi na ahakiki matokeo hasi ambayo kwa kawaida ndiyo yenye madhara. Vivyo hivyo kwa dereva anayeendesha chombo cha moto, msichana anayetaka kuolewa, mfanyabiashara, mfanyakazi, anayefanya mapenzi, anayesoma, wote kwa ujumla wao lazima wawe na majibu ya kwa nini wanataka/ wanafanya hayo, kisha wajadili akilini matokeo mabaya ambayo yapo na kuyatafutie njia ya kuepukana nayo.
KUTOTUMIA UWEZO WOTE
Mwanadamu natajwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo kuliko wengi wao wanavyodhani. Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kuwa asilimia 70 ya watu ulimwenguni, hasa wale wa dunia ya tatu wanaishi chini ya uwezo na vipaji walivyonavyona. Kwa kuzingatia hilo wahanga wengi wa bahati mbaya ni wale ambao hawatumii uwezo wao wote au zaidi ya nusu ya vipaji vyao katika kupambana na matokeo mabaya.
Wanafunzi wengi hawasomi kwa uwezo wao wote, wataalamu, wanasiasa, viongozi, watendaji hawatumii uwezo wao wote kufanya kazi na majukumu waliyonayo, matokeo yake wanalipua kazi na baadaye kuleta matokeo mabaya kisha kuyapa jina la BAHATI MBAYA. Inasemwa kuwa kila mahali palipo na janga msingi wa kwanza kutazamwa kwa watu wenye uelewa ni UZEMBE na kutotumika kwa uwezo halisi wa wahusika katika kukinga matokeo mabaya.
KUAMINI VIASHIRIA VYA KUSHINDWA
Kuna watu ambao hupatwa na matokeo ya bahati mbaya baada ya kuamini viashiria vya kushindwa na kuacha kujizatiti katika nguvu za ushindi. Kwa mfano timu ya mpira inaweza kufungwa magoli 3 kipindi cha kwanza, matokeo hayo yakiaminiwa na wachezaji yanaweza kunyonya nguvu ya ushindani na kuikaribisha bahati mbaya, kumbe wangepuuza viashiria hivyo vya kushindwa mapema wakaongeza nguvu wangeweza kurudisha na pengine kushinda mchezo.
Vivyo hivyo, tunapokuwa tunafanya jambo fulani, kuna viashiria vinaweza kujitokeza kututia hofu kwamba tutashindwa, tunashauriwa kutokata tamaa. Kama wewe ni muuguzi umemuona mgonjwa wako anashindwa kupumua usipunguze harakati za kumtibu kwa kuamini viashiria kwamba anakufa muda mfupi ujao, badala yake zidisha juhudi za kumuokoa. Mfanyabiasha pia ukiona biashara inayumba usikate tamaa, ongeza bidii kwa kufanya hivyo utakuwa unapambana na bahati mbaya na kwa mujibu wa wanasaikolojia utakuwa umenyonya nguvu za mabaya na hivyo kutokukupata.
KUYUMBA KATIKA MAAMUZI
Kuna watu ambao kwa hakika kabisa wanaweza kuwa wamefikiri vema, wametumia uwezo wao wote, hawakuamini viashiria, lakini wakajikuta wanapatwa na bahati mbaya kwa kuyumba katika maamuzi, hasa wakati wa kuhitimisha jambo fulani.
Kwa mfano mtu anaweza kuwa ametafuta mchumba, akamhakiki kama nilivyosema, lakini likatokea neno la umbea fulani likamyumbisha na akajikuta amemwacha mchumba wake na kuchukua mwingine ambaye hakumhakiki katika fikra. Inashauri kwamba mtu asiyumbe katika maamuzi sahihi aliyoyathibitisha.
KUMBUKUMBU MBAYA
Katika maisha yetu kuna watu wengi ambao wanasogeza bahati mbaya kwa kujaza kumbukumbu mbaya za matukio hasi kwenye akili zao. Wapo mahodari wa kukumbuka mahali zilipotokea ajali za magari, yaani wakifika hapo tu mioyo inakwenda mbio. Kuna wanaokumbuka rafiki zao waliokufa wakati wanajifungua na wengine wana historia za nani alipatwa na mabaya baada ya kufanya jambo fulani na wengine wanawafahamu kwa majina waliokufa bila kuzaa, yote hayo ni kujitia hofu tupu.
Kuishi na wingi wa kumbukumbu mbaya ni kosa kubwa kwani hutengeneza uzembe wa mwili ambao huleta matokeo mabaya bila mhusika kujijua. Ndiyo maana unaweza kukuta ajali nyingi hutokea zaidi eneo moja kutokana na madereva wapitao hapo kujaza kumbukumbu mbaya ambazo huwaondolea umakini. Hivyo kama tunataka kuepukana na bahati mbaya ni vema tukaondoa kumbukumbu mbaya zinazotia hofu na hata kama tutakumbuka iwe kwa ajili ya kuongeza umakini na isiwe kwa kupata woga wa kuvuka salama eneo au tukio hilo.
TIBA MBADALA YA MAGONJWA SUGU
Kama inavyofahamika katika jamii yetu kuna watu wengi ambao wamekumbwa na magonjwa yanayotajwa kuwa hayana tiba na wengine wapo njiani kuambukizwa maradhi ya aina hiyo.
Inakuwaje pale unapokwenda hospitali na kukutana na jibu la dokta likikufahamisha kuwa wewe ni muathirika wa Ukimwi au unakabiliwa na kansa au kisukari.
Utawaza nini ukisikia mumeo ana uvimbe kwenye ini?. Utamjibu nini rafiki yako atakapokutaka umshauri kuhusu uvimbe wa hatari uliogundulika katika ubongo wake?
Bila shaka maneno na mawazo lazima yatatofautiana sana. Kwa anayeumwa kauli ya kujipa moyo kuwa atapona inaweza kutoka kinywani lakini mawazo yakabaki na jawabu la kifo kwa asilimia 80 au pengine hata zaidi ya hapo. Hivyo basi, kipimo cha kufa katika mawazo kitakuwa juu ya kile cha kupona.
Kwa maana hiyo, mawazo ya kufa yanaposhinda maradufu zaidi ya ya yale ya kupona, yanazalisha nguvu za kutimiza kile ambacho mwili unapewa taarifa kutoka katika ubongo ambao ndiyo muongozo na chaji ya vitendo vyote vinavyofanywa na viungo vya mwili wa mwanadamu.
Kanuni ya kisaikolojia inayosema kuupa mwili hisia za kifo ni sawa na kupanda umauti ambao mhusika atake asitake atavuna kifo.
Kinachotajwa hapa ni kwamba, kutafuta tiba ya ugonjwa wa kansa ambao mwanadamu ameshaamini kwa mawazo kuwa hauponyeki na kifo ndiyo suluhisho ni kuhangaika bure kumeza dawa ambazo kimsingi hazitafanya kazi inayokusudiwa na matabibu.
Labda kabla haujazama ndani ya mada hii naomba niseme wazi kuwa mimi sina lengo la kupinga watu wasiende hospitali, isipokuwa nataka jamii yenye magonjwa sugu ifahamu tatizo la kwanza kutibiwa si
kansa, Ukimwi, kisukari, pumu na BP, bali tiba ya kwanza lazima ihusishe namna akili inavyoweza kutafsiri magonjwa hayo.
Kabla mgonjwa hajaamua kwenda hospitalini au kumeza vidonge, anatakiwa kuyaondoa mawazo yake kutoka kwenye mfereji wa kifo hadi kwenye matumani ya kuishi licha ya kuambukizwa Ukimwi.
Akishafanya hivyo na kutoshtushwa na hofu ya kufa, atakuwa anaufanya mwili wake kuimarisha kinga zaidi ya kupambana na ugonjwa wake hata kabla ya kuanza kutumia madawa.
Katika utafiti wa hivi karibuni ulioripotiwa katika jarida la New England la Marekani umethibitisha kuwa, watu wenye hofu na kukata tamaa wana hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa kwa uwiano wa 2-1 ukilinganisha na watu ambao wanaishi kwa imani.
Pia utafiti mwingine uliofanyika hivi karibuni nchini Marekani uliowahusisha panya waliofungiwa chombo cha kuwafanya wakate tamaa na wengine kuachwa katika hali yao ya kawaida na baadaye kupandikizwa saratani, waliofungiwa chombo cha hofu walibainika kuambukizwa mara mbili zaidi ya wale ambao hawakuwa na hofu.
Ukweli uko hivi, kinachochangia vifo vya watu wengi sio magonjwa yenyewe bali ni hali za wagonjwa kukata tamaa, jambo ambalo husababisha kinga za mwili kumeng’enywa kwa kiwango kikubwa na kumfanya mgonjwa adhoofike haraka na kuzifanya dawa anazomeza kushindwa kufanya kazi katika kiwango kilichokusudiwa na hatimaye mgonjwa kupoteza maisha yake.
Kutokukata tamaa ni tiba ya kwanza na yenye nguvu zaidi ambayo inaweza kumfanya mgonjwa aishi hata kama amepata maambukizi ya magonjwa ya hatari. Nasema hivi kwa sababu mwenendo wa dunia una nguvu asili ambayo hushughulika kuwaondoa watu waliokata tamaa na kuwaacha watu imara wenye kuamini katika kuishi kwao.
Kwa maana hiyo ili mwenye ugonjwa usiokuwa na tiba aishi muda mrefu lazima kwanza aondokane na hali ya kukata tamaa.
Ni suala la lazima kufuta uongo wa kimawazo kwamba Ukimwi, kansa kisukari ni magonjwa ya kifo, ingekuwa ndivyo watu wasingekufa kwa ajali, badala yake wangesubiri wapate kansa ndiyo wafe. Kifo hakina ubia na magonjwa hayo kwani hata wazima wanakufa.
Jambo jingine kubwa kabisa ambalo watu wengi hawalifahamu ni kuhusu watu wanaotakiwa kuwa karibu na mgonjwa. Imebainika kuwa mara nyingi wagonjwa huwa hawajifahamu hali zao pale wanapokuwa wanaumwa. Kwa maana hiyo majibu ya hali zao huyapata kutoka kwa watu wanaowauguza au wale wanaofika kuwatazama.
Mgonjwa anapotazamana na rafiki yake aliyepo kitandani kwake na akakutana na maneno ya kusikitikia hali yake kutoka kwa wanaomtazama, kwa mfano: “Oooh pole sana ndugu yangu yaani umekwisha kwa muda mfupi hivi, ama kweli ugonjwa wa TB si wa kuchezea” tayari kwa maneno hayo mgonjwa aliyeko kitandani ambaye hafahamu madhara ya ugonjwa wake huingiwa na hofu.
Tangu hapo ataanza kuhisi kuwa ni mtu aliyekonda sana, hisia ambazo zitazidi kumuongoza katika mawazo ya kujiona yu karibu na mlango wa kuzimu. Kwa mantiki hiyo watu wanaowaguza au kuwajulia hali wagonjwa wanatakiwa kuwa na maneno yenye faraja hata pale hali ya mgonjwa inapoonekana kuwa ni ya kukatisha tamaa.
Mgonjwa anatakiwa kuwekwa mbali na mazungumzo yanayoelezea ukubwa wa maradhi yake na jinsi watu wanavyokufa kutokana na ugonjwa wa aina yake. Maneno ya kumkejeri na pengine kumbagua kimaisha ni mambo yanayotakiwa kuepukwa na wauguzaji.
Lengo la kufanya hivi ni kumtibu mgonjwa kiakili na kumfanya ajione ni wa kupona, licha ya kuugua kwa muda mrefu.
Pamoja na hayo inashauriwa kwamba watazama wagonjwa na wahudumu wawe na maneno yenye mzaha utakaofanya mgonjwa awe na fursa ya kucheka au kutabasamu kwa furaha. Hii itamsaidia mgonjwa kupunguza kiwango cha sumu inayozalishwa mwilini mwake.
Ni vizuri pia watu wakafahamu kuwa mazoezi kwa wagonjwa na lishe ni vitu muhimu sana kuliko hata vidonge. Ni vema wagonjwa wakapewa mazoezi kulingana na ushauri wa matabibu na muda mwingi wafarijiwe kwa kupewa vitabu, kutazama video, kusoma majarida na katuni za kuwapotezea mawazo ya kuugua kwao. Kwa wale ambao hawana nguvu wanaweza kubembelezwa kwa maneno ya faraja.
Hayo yote yakifanyika mgonjwa atakuwa na nafasi ya kupona na kuishi kwa muda mrefu hata kama atakuwa na maradhi sugu yasiyokuwa na tiba. Watu wanaokwenda makanisani kuombewa (kwa mfano) hawapewi dawa ila wanatiwa imani ya kwamba watapona.
Tiba ya faraja imekuwa ikitumika zaidi nchini Marekani na Uingereza na imeonesha mafanikio makubwa. Hospitari nyingi hasa wa watoto zimekuwa zikifungwa televisheni zinazoonesha michezo ya kuchekesha eneo la mapokezi na madaktari wamekiri kuwa watoto hupata nafuu hata kabla ya kuingia kwenye chumba cha Daktari.
Ushauri wa mwisho kwa wagonjwa wote wenye magonjwa sugu ni kuacha woga wa kufa badala yake wayapokee matatizo yao na kuyashughulikia kwa imani kuwa yanawezekana kutatuliwa. Ulimwenguni kuna watu wengi ambao wameishi miaka mingi wakiwa na UKIMWI, KANSA, KISUKARI, MOYO na mpaka leo hawana dalili za kufa.
Kinachowaua wengi kama nilivyosema ni hofu si magonjwa husika. Uchunguzi unaonyeha kuwa hata wanaodhurika mapema na virusi vya ukimwi ni wale waliopokea majibu yako na kukata tamaa ya kuishi.
N
Mbinu za kuacha uvutaji wa sigara
Miongoni mwa mambo magumu kabisa katika ufanikishaji wake ni mtu kuachana na uvutaji wa sigara. Watu wengi wamekuwa wakionywa kuachana na uvutaji wa sigara kwa sababu ya madhara yake, lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukolewa na kiwango cha Nikotini inayopatikana katika tumbaku.
Vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika uvutaji kwa kufuata mkumbo, lakini baadaye wanapokuja kutambua kuwa wako katika hatari ya kuambukizwa au pengine wana ugonjwa wa kifua kikuu, wanakuwa katika wakati mgumu wa kuachana na uvutaji huo. Wengi wao wamekufa huku makundi kwa makundi wakitangatanga kutafuta suluhu ya kuchana na uvutaji, si tu kwa sababu ya kuhofia ugonjwa, bali hata kukosa uwezo wa kununua bidhaa hiyo.
Hata hivyo idadi kubwa ya wanaojaribu kuacha wamejikuta wakipata majibu ya kutoweza, kutokana na kusumbuliwa na hamu ya uvutaji, umbumbu wa mawazo pindi wanapokaa muda mrefu bila kuvuta, kuumwa na kichwa na hata udhaifu katika kukumbuka vitu au mambo waliyofanya au waliyopanga kuyatenda.
Pamoja na yote hayo watalaam na washauri wa masuala uvuaji wa sigara wanasema wanaopatwa na hayo wamekosa mbinu na muongozo wa kuwasaidia waachane na uvutaji wa sigara bila kupata madhara.
Kwa ufupi somo hili limehusisha uchunguzi wa kina pamoja na kumbukumbu za kitaalamu kutoka kwa washauri kama Anderson JE, Jorenby DE, Scott WJ, Fiore MC, Bailey WC, Cohen SJ, ambao wote kwa pamoja kupitia vituo vyao kikiwemo cha US Department of Health and Human Services na Public Health Service walishawahiwa kueleza mbinu salama za kuachana na uvuaji wa sigara. Zifuatazo ni dondoo kadhaa za kufuata ili mvutaji aache sigara kwa usalama.
* Mvutaji lazima afahamu ni muda gani ambao huwa anavuta sigara kwa wingi, je ni wakati akiwa amelewa au akiwa na mawazo mengi ya kimaisha? Akishafahamu hilo ajiulize ni kiwango gani cha sigara ambacho huwa unavuta kwa siku?
*Baada ya hapo achukua kitabu chake cha kumbukumbu na aandike muda huo ambao yeye huvuta sigara kwa wingi. Ajiulize kwa nini huwa unavuta, atathimini madhara ya uvutaji wa sigara kwake binafsi na kwa familia yako.
* Kaa chini upitie kwa makini kumbukumbu zako za muda na kiwango cha sigara unazovuta kwa nyakati hizo, kisha panga utaratibu mpya. Kwa mfano kama unavuta sana wakati ukiwa kwenye mawazo hakikisha kuwa unapoanza kufikiria juu ya jambo fulani uwe na kitu mbadala kitachukua nafasi ya sigara. Mfano kahawa au chai? Hakikisha kila penye hamu ya uvutaji unaweka kitu kingine mbadala cha kufanya zaidi ya kuvuta sigara.
*Ondoa masalio ya sigara katika sehemu ambazo unaishi, fua nguo zote na vitambaa ili kuondoa harufu ya sigara katika eneo unalokuwepo. Usikae karibu na mtu anayevuta, usikubali kuwa mshirika wa mvutaji na usiwe mtu wa kuendekeza sana msukumo wa mwili unaotaka uvute, bali kila unapowaza juu ya kuvuta fikiria madhara na nia yako ya kuacha.
*Wafahamishe rafiki zako kuwa umeamua kuachana na uvutaji, ili upate watu wa kuwaonea aibu pale utakapoanguka na kurudia uvutaji wa sigara. Panga tarehe ya kuacha na iwe kwenye kumbukumbu.
*Wakati ukiiendea tarehe hiyo ya kuacha hakikisha unapunguza kiwango cha uvutaji kadiri unavyoisogea siku hiyo. Jipangie muda mrefu zaidi ya kuvuta kulingana na kiwango chako cha uvutaji na kuendelea kuuongeza kila siku ili uzoee kukaa saa nyingi bila kuvuta.
*Fuata ratiba mbadala uliyojiwekea kuziba pengo la uvutaji, kama umepanga kutumia kahawa kila unapokuwa mpweke sebuleni hakikisha unajizoeza ili ikifika tarehe yako ya kuacha usiwe mtu wa kujiuliza cha kufanya nyakati ambazo utakuwa na hamu ya sigara.
*Lengo lako liwe ni kufanikiwa na usikate tamaa utakaposhindwa kufanikisha lengo lako kwa wakati uliojipangia. Mara kwa mara nenda kamuone daktari mshauri ili akupe muongozo zaidi wa kukusaidia na ikiwezekana akupe nafasi ya kuwatembelea wagonjwa waliopata ugonjwa wa kifua kwa sababu ya kuvuta sigara.
Kwa kifupi hizo ni dondoo chache tu za kukusaidia kuachana na uvutaji wa sigara, lakini mara nyingi kinachoweka nguvu za kufanikisha uachaji wa sigara ni utashi wa mtu ambao hutokana na tathimin ya kina ya muhusika na mtazamo wake juu ya sababu za kuacha. Mara nyingi wanaoshindwa ni wale ambao hawakuzitia nguvu sababu za kuacha kwao.
Siku zote mwanadamu anaongozwa na utashi na kila mwenye kutaka hufanikiwa. Hii ina maana kuwa kama mwanadamu atasema hawezi kuacha kitu fulani, haina maana kama hawezi kwa sababu ameshindwa kujizuia bali ameamua kutokutaka na kinachomshinda ni matokeo ya ya maamuzi yake. Kila anayetaka jambo hufanikiwa na hata wavutao sigara wanaweza kuacha kama wakitaka kufanya hivyo.
Hatua 10 za kujiandaa na mitihani
Katika uchunguzi wangu nimebaini kuwa ni wanafunzi wachache ambao hutoka katika vyumba vya mtihani na jibu la uhakika kuwa wamefaulu au wamefeli mitihani yao, hii ikiwa na maana kuwa wengi wao huwa hawafahamu kama majibu walioandika ni sahihi au la, na hivyo kudhani kuwa wasahihishaji wanaweza kuwa na jipya zaidi ya kuwapa mavuno ya kile walichopanda.
Kutapatapa huku kwa majibu hakuna maana nyingine zaidi ya kuutambulisha uwezo duni wa mwanafunzi husika kuwa alipoingia hadi anatoka kwenye chumba cha mtihani hakuwa anajua alichojifunza kabla, alicholetewa kwenye mtihani na alichojibu, ndiyo maana amekosa jibu la uhakika.
Lakini kama angefahamu alichojifunza, kilichotokea na alichojibu, moja kwa moja angeweza kuwaambia wazazi na walezi wake kuwa hakufanya vizuri mtihani wake na hivyo kutupilia mbali subira ya bahati, ambayo katika masomo haipo kwa vile apandacho mtu ndicho avunacho.
Baada ya kusema haya ni vema sasa tukajifunza mbinu za kufanya ili mwanafunzi aweze kufanya mtihani wake vema na kufaulu kwa alama za juu.
Kwanza ni muda, wanafunzi wengi huwa hawafahamu matayarisho ya mitihani yanahitaji muda gani kuyakamilisha, hivyo hukurupuka wakati mitihani ikiwa karibu au kujisumbua kwa muda usiotimilifu na kujikuta wamepoteza shauku na kukata tamaa.
Kifupi mwanzo wa mwanafunzi kufanya vibaya kwenye mitihani yake huanzia kwenye kupanga muda wake na kuutumia.
Kwenye kipengele hiki kuna makundi matatu ambayo ni ya wale wanaouchezea muda wote, wanaoutumia kwa kuwahi na wanaoutumia kwa kuchelewa huku kiini kikubwa cha tatizo kikiwa ni kwa mwanafunzi kutokujitambua uwezo wake.
Kujitambua uwezo ni suala muhimu, ambalo linaweza kumfanya mwanafunzi akaamua ni muda gani anaohitaji kufanya maandalizi ya mitihani wake. Hii ikiwa na maana kuwa si wanafunzi wote wanahitaji muda mwingi kujiandaa kutokana na wepesi wao wa kumbukumbu, vilevile si wote wanaohitaji muda mchache kwa maana ile ile ya uwezo wao binafsi.
Hivyo basi, ni wajibu wa mwanafunzi kujiuliza anahitaji muda gani kukamilisha maandalizi yake kabla hajaingia kwenye chumba cha mtihani?
Swali hili lazima liende sambamba na vitu gani ambavyo anadhani ni muhimu kuvisoma, kuvielewa kabla ya siku yake ya kutahiniwa.
Ikiwa ni topic, lazima mwanafunzi ajiulize ni ngapi ambazo hajazielewa, na je itamchukua muda gani kuzimaliza? Ikiwa jibu atakalopata litakuwa ni miezi sita, muda huo lazima utumike kwa kukamilisha malengo ya kuzielewa topic hizo bila kukwama.
Kama muda utamalizika bila mipango kutimizwa, kuna hatari kwa mwanafunzi kuingia kwenye chumba cha mtihani akiwa na viporo vya mada asizozifahamu, jambo ambalo ni muhari kwake endapo atakutana na maswali kutoka kwenye mada hizo.
Mbali na hayo mwanafunzi ambaye anataka kupata alama za juu katika mtihani wake lazima awe mtu wa kujiandaa kila siku kwa kutumia dondoo zifuatazo ili kujihakikishia uwezo wa kufaulu na kuepukana na dhana ya kuishi kwa kutegemea bahati.
KWANZA: Kama nilivyosema hapo juu jambo la kwanza ni kuzingatia muda, si vema kukurupuka na kukimbizana nao na kujinyima usingizi wakati ratiba ya mtihani ilikuwa inafahamika na muhusika alikuwa na uwezo wa kujiandaa taratibu kuelekea kwenye siku ya kutahiniwa kwake.
PILI: Jindae mwenyewe kwa kutafuta na kufanya mitihani iliyopita, huku ukinakili maswali ambayo watunzi wamekuwa wakiyarudia rudia kila mwaka.
Njia hii itakuwezesha kujiandaa kwa kuzingatia shabaha na mahitaji halisi ya maswali yatokayo mara nyingi kwenye mitihani. Hakikisha unapata mitihani ya nyuma ya ngazi uliyopo isiyopungua kumi au zaidi na uifanye huku ukihakikisha hakuna swali hata moja ambalo linakushinda.
Pamoja na ukweli kwamba ubahatishaji wa vitu si njia sahihi sana, lakini umeonekana kuwasaidia wale ambao ubahatishaji wao huambatana na umakini, hivyo mwanafunzi anatakiwa kuwa na tabia ya kubahatisha maswali ambayo anadhani mwalimu wake anaweza kuyatoa kutoka kwenye daftari lake na hivyo kujiandaa.
Ubaharishaji huu, lazima uambane na kile nilichosema awali, yaani kuwa na kumbukumbu ya mitihani iliyopita. Wanasema watalaamu kuwa ulimwengu una tabia ya kurudia matukio, hivyo hata kwenye maswali kuna tabia hii ya kujirudia rudia.
TATU: Orodhesha maeneo yote ambayo huyaelewi kwenye mtihani hiyo ya nyuma na uyafanyie mazoezi kwa kupata ushauri kwa waalimu wako. Kama kuna mada ambazo hujazielewa kwenye daftari lako hakikisha muda uliojiwekea utatosha kuzielewa.
NNE: Hakikisha unajizoeza kufanya mitihani ya majaribio mara kwa mara, ambayo utaifanya kwa kuzingatia muda na masharti yote ambayo hutolewa siku ya kufanya mtihani halisi. Haifai mwanafunzi kukimbia majaribio yanayotolewa darasani na mwalimu wake, kwani hayo ndiyo yatamuwezesha kufahamu kama amekamilika kwa kutahiniwa au bado kuna eneo linamtatiza.
TANO: Hakikisha kuwa kumbukumbu zako kichwani zinaongezeka kadiri unavyojifunza, usiwe mtu wa kusahau sahau uliyojifunza na ikiwezekana eneo ambalo unaonekana kulisahau ndilo ulipe kipaumbele cha kujikumbusha, ikibidi hata kila siku.
SITA: Angalia kwa makini alama zako za mitihani ya majaribio, ikiwa unapata alama za chini ujue kuna mahali panahitaji nguvu za ziada, shauriana na mwalimu wako maeneo yote unayokosa au yanayokusumbua kabla ya siku ya mtihani.
SABA: Ili mwanafunzi awe na uhakika wa kufanya vema mtihani wake anatakiwa kuzingatia dondoo zote zilizotolewa kwenye kipengele cha kuimarisha kumbukumbu kichwani, ambazo zimo ndani ya kitabu hiki.
NANE: Wakati mwingine ni vema ukausikiliza mwili, si vema kuulazimisha kusoma hata kama unaona kuna udhaifu, baadhi ya wanafunzi hukesha wiki mbili mfululizo wakisoma, matokeo yake mwili na akili huchoka na kushindwa kupokea masomo vizuri. Muda wa kupumzika unahitajika.
TISA: Kabla mwanafunzi hajaingia katika chumba cha mtihani anatakiwa kujiamini kwa kushinda hofu. Eneo hili ni muhimu sana kwani kuna wanafunzi hufeli si kwa sababu hawakujiandaa, bali hukumbwa na hofu muda mfupi kabla ya kuanza mtihani. Hivyo ni muhimu mwanafunzi akaandaliwa kisaikolojia na waalimu pamoja na wazazi wake jinsi atakavyoweza kufanya mtihani bila hofu.
KUMI: Imani ni hitimisho la mafanikio ya mwanafunzi, haifai kuingia katika chumba cha mtihani ukiwa na mawazo hasi. Kinachotakiwa ni ari ya ushindi au kwa lugha nyingine ni mawazo chanya. “LAZIMA NIFAULU MTIHANI HUU” Imani hii inaweza kujengwa na mtu kupitia kujiamini mwenyewe au kuamini kwa msaada wa nguvu za imani yake ya dini.
Mbinu za kusoma na kuelewa
Tunapozungumzia uelewa wa wanafunzi darasani tunakuwa tumeingia katika msitu mpana zaidi wa majibu, lakini ukweli unabaki kuwa ndani ya darasa linalofundiswa na mwalimu mmoja hutokea wanafunzi wengine wakaelewa zaidi na wengine wasielewe kabisa.
Kuna wanafunzi na baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kuna binadamu huzaliwa na uwezo mkubwa wa kuelewa zaidi ya wenzao, huu ni ukweli lakini si wa kuamini sana kwani kipimo cha kuhakikisha kuwa huyu ameumbwa hivyo hakuna zaidi ya kuangali tu yale ambayo yanatendwa na huyo anayeitwa ana akili za ziada au za kuzaliwa.
Lakini wakati huo huo kuangalia ayatendayo mtu au kuangalia uelewa wake darasani hakutoshi kumpa sifa za kuwa na sababu ya kuwazidi wenzake ambao wameamua tu kutokusoma, kutomsikiliza mwalimu, kutozingatia wanachoelekezwa au wameharibiwa na masumufu ya dunia yakiwemo masuala ya mapenzi.
Kwa maana hiyo, hawa ambao hawaelewi kwa sababu wanasoma huku wanawaza mambo ya kimapenzi au wanafikiria kwenda muziki au kucheza, hawawezi kuwekwa kwenye kundi la watu ambao hawakuzaliwa na akili bali waliojiharibu kwa kukosa kuufahamu ukweli.
Hivyo basi, kuna kila sababu kwa mwanafunzi kupuuza fikra za kizembe zinazomfanya ajione kuwa anazidiwa na wenzake darasani kwa sababu yeye hakuzaliwa na akili nyingi. Kila binadamu mwenye akili timamu kwa mujibu wa tafiti za watalaamu wa masuala ya ufahamu ana uwezo mkubwa mara 1000 kuliko ule anaoutumia.
Hii ina maana kuwa kama kuna mwanafunzi anaongoza darasa lenye watu 100, uwezo huo wa kuongoza anaweza kusonga nao mpaka akafikia kwa watu 1,000 na akifika hapo anaongeza mara 1,000 tena na tena. Huu ni uwezo wa ajabu sana alionao mwanadamu. Lakini wengi kati yetu tumeshindwa kusonga mbele mara elfu toka tulipo kwa sababu tumeshindwa kutumia kipawa chetu na tumeamini uongo kuwa kuna waliopendelewa tangu wanaumbwa.
Ben Carson mwandishi mashuhuri na daktari bingwa wa magonjwa ya akili ambaye awali alikuwa akiburuza mkia darasani aliambiwa na mama yake aitwaye Sanya Carson maneno haya: �you can do anything they can do, only you can do it better� (Nukuu inapatikana ndani ya kitabu kiitwacho THINK BIG cha Ben Carson ukurasa wa 7) kwa tafsiri isiyo rasimi Ben aliambiwa na mama yake kuwa �unaweza kufanya wayafanyayo, lakini wewe unaweza kufanya zaidi yao�
Mwanamke huyu alidumu kumwambia mwanae kuwa ni bora zaidi ya wengine na kumtaka aongeze bidii kila siku ili afikie lengo. Ben aliaamini aliyokuwa akiambiwa na kwa makusudi aliamua kujibidisha na hatimaye kufikia kiwango cha kuwa msomi mwenye kuheshimika ulimwenguni.
Kimsingi kuna watu wengi ambao walipuuza kauli za kujiona duni na kufanikiwa katika mambo waliyokusudia kuyafanya. Huu ni ushahidi kuwa hajaumbwa mwanadamu kuwa wa mwisho darasani bali matokeo ya kushindwa ni lazima yapewe kwanza sababu za uzembe na maumbile yawe ni ya mwisho kufikiriwa. Ufuatao ni muongozo wa kumuwezesha mwanafunzi kusoma na kuelewa vema.
-Kumzingatia mwalimu
Wanafunzi wengi wanashindwa kufikia uelewa wa juu kwenye masomo yao kwa sababu hawawi makini wanapofundishwa darasani na waalimu wao. Kitendo cha kuweka mawazo nusu darasani na nusu nje ni kujiwekea kizingiti cha kuelewa kinachofundishwa.
Ni muhimu kwa mwanafunzi kama nilivyosema awali kwamba ampende mwalimu wake na aone furaha kumsikiliza anapofundisha. Itakuwa vigumu kwa mwanafunzi kuelewa anachofundishwa kama anayemfundisha anamchukia eti tu kwa sababu jana alimwadhibu au alimfokea.
Ifahamike kuwa, msingi mkubwa kabisa wa mwanafunzi kuelewa somo lo lote ni kuelewa anachofundiswa moja kwa moja toka kwa mwalimu wake. Kitendo cha kutoka darasani bila kujua kilichofundishwa ni jambo la hatari kwa maendeleo ya mwanafunzi kimasomo.
Inashauri kuwa mwanafunzi anapoingia darasani anatakiwa kuwa makini na kufuata anachoongea mwalimu wake neno kwa neno, huku akinoti anachoelewa na asichoelewa, ili kama ni msaada wa kueleweshwa aombe muda mfupi baada ya mwalimu kumaliza kufundisha.
Kurudia notisi
Mara baada ya mwanafunzi kufundishwa na kuelewa, anatakiwa akifika nyumbani siku hiyo hiyo arudia yale aliyosoma kwa kujikumbusha alichosema mwalimu wake. Hii itamsaidia zaidi kuifanya akili itunze kumbukumbu ya somo alilofundishwa na hivyo kumfanya mwanafunzi kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kujikumbusha au kukumbuka atakapokuwa akifanya mtihani.
Haifai kwa mwanafunzi kurejea nyumbani na kufunika madaftari bila kujikumbusha au kurudia siku mbili baada ya kufundishwa, kufanya hivyo kunaweza kutoa nafasi kwa akili kuyatupa aliyofundishwa kutokana na wingi wa masomo au mambo aliyoelekezwa kwa siku mbili au wiki nzima.
-Kufanya uchambuzi
Ni wajibu wa mwanafunzi kufanya uchambuzi wa notisi zake za shule kwa kuandika mchanganuo wenye maneno machache ya msingi kwenye daftari jingine au karatasi. Kufanya hivi kutamsaidia kupunguza wingi wa maneno ya kuhifadhi akilini hasa kwa wanafunzi wa ngazi za chini ambao wengi wao hutumia mbinu za kukariri ambazo ni hatari kwa kusahau haraka.
Kwa mfano, wanafunzi anapofundishwa kuhusu ubadhilifu wa pesa ndani ya Benki Kuu ya Tanzania �BoT� kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje maarufu kama EPA na kupewa takwimu na mlolongo mzima ulivyokuwa, anachotakiwa kufanya yeye ni kunyambua mambo ya msingi ambayo yatamuongoza katika kujibu maswali, kama kuwajua wahusika, mwaka wa skendo, kiasi kilichoibwa na kilichorudiswa.
Mambo hayo machache akiyafahamu yatamfanya awe na uwezo wa kulielezea jambo hilo kwa kina mbele za watu na kuonekana mwenye ufahamu wa kutosha, lakini pia atajihakikishia uwezo wa kukabili jaribio au mtihani wo wote utakaokuja na swali la EPA.
-Kujipima uelewa
Kumsikiliza mwalimu, kurudia notisi na kufanya uchambuzi kunaweza kusitoe picha sahihi juu ya uelewa wa mwanafuzni katika yale anayosoma pamoja na uwezo wake wa kukumbuka aliyojifunza. Mwanafunzi ili ajipime kama akili yake imenakiri vema anatakiwa kutenga siku ndani ya wiki kwa kujitungia mitihani kutoka kwenye daftari zake, kuifanya na kujisahihisha mwenyewe.
Hii itampa mhusika ufahamu wa kujua ni eneo gani kaelewa zaidi ya jingine na hivyo kujituma zaidi sehemu ambayo hajaelewa kwa kuuliza tena kwa mwalimu au kwa wenzake ambao anadhani wana ufahamu mkubwa kuliko yeye. Ni vibaya kusoma bila kujipima uwezo. Itapendeza kama wanafunzi watakuwa wakifanya mitihani ya kujipima kwenye vikundi kila wiki.
-Kukuza ufahamu
Ziko njia nyingi za mwanafunzi kukuza ufahamu wake lakini muhimu zaidi ni kusoma vitabu, kusikiliza habari kupitia vyombo vya mbalimbali na kushiriki katika mijadala ya wazi yenye kujadili masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Mwanafunzi hawezi kukuza ufahamu kama hajui masuala ya jamii yake, siasa za ulimwengu na hali ya uchumi wa ndani na nje na hayo yote yanapatikana kwa kusoma. Jambo jingine la msingi ni kwa mwanafunzi kuepukana na aibu ya kujieleza mbele za watu. Njia pekee ya kuhifadhi kumbukumbu ya kile alichosoma na kuwa na tabia ya kuwaeleza wengine.
Kwa mfano, kama mwanafunzi atakuwa amefungua mtandao wa inteneti na kusoma habari za kupanda kwa uchumi wa Marekani anatakiwa awaeleze wenzake alichojifunza, vivyo hivyo atakaposoma vitabu au kutazama filamu. Kujua jambo na kutokulitenda ni ujinga sawa na mtu ambaye hajui kabisa. Aibu ya kuzungumza mbele za watu haifai ni vema mwanafunzi akajiamini na kujizoeza kueleza anachokifahamu mbele za watu.
Subscribe to:
Posts (Atom)