Sunday, November 25, 2012

Umasikini

Mipaka na vipimo vya umaskini Nchini Tanzania vimejitokeza katika kipindi cha muda mrefu. Muda wa mabadiliko katika kufahamu mipaka yanatokana na tofauti zilizopo na muda na nafasi ya kueleza nini maana ya kuwa na hali njema. Maelezo ya awali yalilenga kwenye mahitaji muhimu ya msingi kwa ajili ya kumwezesha mtu kuishi katika kipimo cha chini. Gharama za chini za mahitaji ya lishe ndiyo kitu muhimu cha kipimo kiwango cha umaskini. Maelezo hayo ya kipimo cha umaskini vilijumuisha vigezo vya jamii na uchumi vinavyohusika na viwango vya juu vya magonjwa na vifo, kushamiri kwa lishe duni, kutoweza kusoma wala kuandika, hali ya juu ya vifo vya watoto na akina mama, umri mdogo wa kuishi, mahali duni pa kuishi, nguo duni, mapato ya chini na matumizi finyu na miundombinu mibovu (mawasiliano, usafirishaji, huduma za jamii n.k). vipimo vingine pamoja na uzazi wa mara kwa mara, kukosekana kwa huduma za msingi kama vile maji safi, ukosefu wa chakula na kuwa na teknolojia duni. Kwa ujumla, vipimo hivyo vinaweza kutumika kumtambua mtu na nyumba maskini, jamii na jumuiya maskini. Nyumba wanayoishi watu au jamii inayokabiliwa na baadhi au vipimo vyote hivyo inaweza kusemwa kwamba ni maskini. Masuala mengi yanayohusu vipimo vya umaskini vinaegemea zaidi kwenye hali ya uchumi. Hatimaye, vingi vya vigezo vyake vinaweza kupimwa. Hivi karibuni, maelezo ya umaskini yameweza kupamuliwa zaidi. Maelezo mapya yanajumuisha matatizo ya heshima binafsi, uwezekano wa kupatwa na hatari za ndani na nje, kutengwa kutoka mpango wa maendeleo na kukosekana kwa mtaji wa jamii. Nyongeza hizo mpya kwa maelezo ya umaskini zinagusa ubora wa hali njema ya jamii na uchumi. Mkusanyiko wa ubora na wingi wa vigezo vya umaskini vinatumika kutambua nani ni maskini, ukubwa wa umaskini wao, wapi wanaikoshi na wanajishguhulisha na kazi gani ili waweze kuishi. Maelezo ya vigezo hivyo pia vinasaidia kutayarisha sera kwa ajili ya kusaidia maskini kukuza uchumi, kupanga matumizi kwa ajili ya watu, mipango ya usalama na kutayarisha vifaa kwa ajili ya kutathmini matokeo ya mipango na miradi juu ya kupunguza umaskini. Kwa kawaida umaskini ni matokeo ya vitu vingi na mara nyingi vitu ambavyo vinaingiliana ambavyo vinajumuisha ukosefu wa rasilimali ya kuzalisha utajiri, kutojua kusoma wala kuandika, magonjwa maafa kama vile mafuriko, ukame na maafa yanayoletwa na binadamu, kama vile vita. Katika ngazi ya kimataifa, kukosekana kwa usawa katika kushirikiana kiuchumi na kisiasa kama inavyojionyesha katika masharti yasiyoridhisha ya biashara na shughuli nyingine yaliyopangwa kwa ajili ya nchi zinazoendelea pia ni moja ya sababu kubwa ya umaskini katika nchi zinazoendelea. Baadhi ya sababu za umaskini hazijionyeshi wazi wazi kama vile desturi na mila ambazo zinazuia matumizi ya rasilimali ipasavyo na kukosa kushirikishwa katika masuala ya kuongeza kipato. Tathmini ya kiwango na mwelekeo wa umaskini unatibuliwa na kukosekana kwa taarifa za mara kwa mra, kutopatikana kwa vigezo vinavyojulikana rasmi vya umaskini. Kutopatikana kwa vigezo vilivyo rasmi vya umaskini kumewafanya baadhi ya wachunguzi kuamua kutumia matokeo ya uchunguzi wao wenyewe. Hivyo, “vigezo vya chini” huonyesha mahitaji ya msingi ya chakula yasiyothibitishwa kwa mfano tabia za kula, mahitaji ya lishe na gharama, na “vigezo vya juu” vinahusu mahitaji ya chakula, pamoja na mahitaji mengine muhimu, kama nguo, nyumba, maji na afya. Zaidi ya hayo, kigezo kingine cha umaskini ni matumizi ya dola moja ya Marekani kwa siku kwa kulinganisha na nchi nyingine. Umaskini mikoani na kukuza Hali njema Umaskini na vigezo vya hali njema vinatumika hapa katika kupanga nafasi za mikoa 20 ya Tanzania. Uchambuzi huu ni wa awali, unahitajikaji kuchujwa zaidi, na hivyo utumike kwa hadhari. Kutokana na uchambuzi huu, Dodoma, Kagera, Lindi na Pwani ni mikoa inayoathirika zaidi na hali ya umaskini Mikoa ya Dar es Salaam, Ruvuma na Kilimanjaro inaathirika kidogo sana. Umaskini unazidi kubaki kuwa zaidi ni suala la vijijini, ingawa idadi ya watu maskini katika maeneo ya miji hasa wasio na kazi na wale waliopo kwenye sekta isiyo rasmi, idadi yao ya umaskini inaongezeka kwa kasi katika eneo hili katika maeneo yote ya mjini na vijijini. Maskini wanakosa mtaji na rasilimali aliyonayo mtu mwenyewe kwa mfano elimu duni, hali mbaya ya afya na familia kubwa. Hali ya umaskini inahatarishwa zaidi kwa kuzidi kuongezeka kwa magonjwa hasa kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa wa UKIMWI. Hatua zinazochukulwia kuondoa umaskini Tangu kupatikana kwa uhuru 1961 Serikali ya Tanzania iliweka suala la kuondoa umaskini kuwa moja ya malengo yake makuu. Moja ya mikakati iliyobuniwa ni kuanzisha na kutekeleza sera za jamii na uchumi ambazo zinahusika na suala la umaskini katika ngazi za taifa na ya mtu binafsi. Utaratibu huu unamaanisha kwamba serikali iingilie kati kusaidia katika masuala ya elimu na maeneo mengine ya ustawi wa jamii, pamoja na kujenga mazingira mazuri ya kumwezesha mwekezaji binafsi kuingia katika sekta za uzalishaji. Katika harakati za mipango ya kupunguza umaskini ambao umeenea kote, Tanzania ilitayarisha mwaka 1999 na kukubali kutumika kwa Dira ya Maendeleo 2025 na mpango wa Taifa wa kuondoa umaskini (NPES) hapo mwaka 1997, mipango inayofafanua dira kwa ajili ya jamii fukara na kustawisha hali ya jamii. Mpango wa Taifa wa kuondoa umaskini ambao ulianza kutumika 1997 ulilenga katika kutoa mwongozo kwa washika dau katika kuchambua, kutunga, kutekeleza na kutathmini umaskini wao. Lengo la mpango huu ilikuwa ni kutoa maelekezo ya kuongoza juhudi za kuangamiza umaskini kwa nia ya kuondoa kabisa umaskini ifikapo 2025. Ili kufanikisha malengo ya mpango wa Taifa wa kutokomeza umaskini serikali umezishirikisha sekta muhimu tano: ¨ Elimu ¨ Afya ¨ Maji ¨ Kilimo na ¨ Barabara za vijijini Mpango umechagua maeneo matatu ya kushughulikiwa, nayo ni yafuatayo:- maeneo yanayotengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kutokomeza umaskini, maeneo yanayojenga uwezo wa kupambana na umaskini na maeneo yanayotokomeza umaskini. Mpango huo pia umetamka majukumu yatakayotekelezwa na ngazi mbalimbali katika juhudi za kuondoa umaskini. Dira ya 2025 iko sambamba na mpango wa maendeleo wa kimataifa ambao unatumia dira kusaidia kupata taarifa za kazi zinazofanyika katika kuangamiza umaskini. Mwezi Juni, 1999 serikali ilitoa kijitabu cha vigezo vya kusimamia umaskini na hali njema ambacho kina nia ya kutoa msingi wa kusimamia utekelezaji na kutathmini msukumo wa mpango wa kutokomeza umaskini. Vigezo vilivyoko katika kijitabu hiki vitasaidia kutoa taaifa za uhakika za maendeleo kwa kufahamu hali ya umaskini na ustawi ili kuongoza shughuli za sera na mipango ya kupunguza umaskini. Mpango wa Taifa wa kuondoa umaskini (NPES) na kijitabu cha vigezo vya kusimamia umaskini na hali njema vilitayarishwa kwa kushirikiana na washika dau mbalimbali. Sambamba na NPES, serikali imechagua maeneo ya kupewa kipaumbele ya kutumia fedha za umma kwa utaratibu wa “The Medium Term Expenditure Framework” (MTEF) ambao utekelezaji wake unasimamiwa chini ya utaratibu wa mwaka wa Public Expenditure Review (PER) ambao pia unawahusisha washika dau. Utaratibu huu ndio uliokuwa unatumika kuongoza bajeti kwa miaka mitaktu sasa. Mfumo huu wa kuendesha bajeti utaingizwa katika mpango mzima wa maendeleo ambao unashirikisha msaada kutoka nje. Mfumo unajumuisha malengo yote mawili ya kuendeleza uchumi na jamii kwa kuzingatia sekta zilizopewa kipaumbele mkazo ukielekezwa kwa maeneo yakfuatayo: ¨ Kuimarisha zaidi sera ya mazingira na masoko yanayokubalika. Kujenga mfumo imara ambao ndiyo ufunguo wa kipimo cha kustawi na njia ya kupunguza umaskini kwa kiwango kikubwa. Lakini, ufunguo wa kupunguza umaskini kwa kiwango kikubwa katika Tanzania ni kuongeza kasi ya kustawi. Makadirio ya kuonyesha kupungua kwa umaskini yanaoenda sambamba na ustawishaji na kuonyesha kuwa ongezeko la kustawi kunaweza kupunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya mstari wa umaskini ambao kwa sasa ni asilimia 50 hadi kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2015. ¨ Kufanikiwa kwa lengo la kuongeza ustawishaji kutahitaji juhudi nzito za kuzidisha uzalishaji na kuongeza uwekezaji katika mtaji wa watu na mali. ¨ Kuongeza uwekezaji kwa kutumia nguvu na uwezo wa binadamu kunahitaji kuchukuliwa hatua za kuwaongezea wahusika motisha na kuongeza faida kwa shughuli hizo za uwekezaji na kuongeza msaada wa umma katika maeneo yaliyo nje ya mfumo kwa mfano msaada wa elimu ya msingi na afya. ¨ Marekebisho ya mfumo. ¨ Shughuli za kudhibiti ukimwi zinatakiwa kuwekwa ndani ya sera ya maendeleo na ihusishe sekta zote. ¨ Mpango wa muda mrefu unaoambatana na ukuaji wa kilimo nchini Tanzania unahitaji angalao hali ya uchumi uliotulia, utafiti unaofaa na upanuzi, miundombinu iliyoimarishwa na kuendeleza mfumo uliofungamana, uimarishaji wa asasi zinazosaidia mabadiliko ya kilimo na maendeleo ya vijiji kwa mapana zaidi. Mipango ya kuondoa umaskini Mpango huu unaangaliwa kama ni chombo cha kupitisha juhudi za taifa kuelekea mwenye madhumuni tuliyokubaliana pamoja na nyenzo zilizo dhahiri na matokeo kimsingi. Ufafanuzi na utekelezaji wa mpango ni utaratibu unaoendelea. Wakati maamuzi yanayohusu masuala mengi yalikwishaanzishwa, matayarisho ya mipango ya baadhi ya sekta kama vile kilimo na elimu bado hayajakamilika. Zaidi ya hayo, uamuzi wa utekelezaji wa mabadiliko yanayolenga kuhamasisha jukumu la kutunga kutekeleza na kusimamia upunguzaji wa umaskini kusimamiwa na wilaya, manispaa na jumuia katika ngazi za chini umeanza, lakini zoezi hilo litachukua muda kukamilika. Kwa hiyo mpango mzima wa kupunguza umaskini itabidi ushughulikiwe taratibu ili kuruhusu kujumuisha mipango na shughuli nyingine zitakazojitokeza kutokana na kazi zinazoendelea. Mpango wa kupunguza umaskini kwa kiwango kikubwa, ni sehemu ya mabadiliko makubwa ya uchumi na mfumo unaosaidiwa chini ya mpango wa “Poverty Reduction Growth Facility” unaogharamiwa na Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) na mpango wa Poverty Structural Adjustment Credit unaogharamiwa na Benki ya Dunia IWB). Wakati huo huo katika kuizumgumzia hoja hiyo ngumu ya umaskini Benki ya Dunia na shirika la Kimataifa la Fedha hapo mwaka 1999 walianzisha juhudi za mpango wa “Enhanced Highly Indebted Poor Countries”, (HIPC). Madhumuni ya kuanzisha mpango huu ni kutoa msamaha wa kodi kwa nchi zinazokabiliana na mzigo mkubwa wa kulipa madeni. Msamaha utakaopatikana kutokana na unafuu wa madeni utaiwezesha Tanzania kutumia rasilimali zake kuimarisha maendeleo na kupunguza umaskini na kuimarisha upatikanaji wa huduma za elimu na afya. Jumuiya ya wahisani kwa kupitia HIPC imetoa unafuu ambao umeiongezea Tanzania uwezo wa kupigana na umaskini na kutekeleza Sera zake za maendeleo. Silaha kuu zinazotumika katika kufanikisha mpango huu ni kutekeleza yaliyomo katika Poverty Reducation and Growth Facility ya IMF na Programmatic Structural Adjustment Credit ya WB na PRSP. PRSP ni sehemu ya mpango wa HIPC na unaolenga uhusiano katika kupunguza umaskini. PRSP inazingatia shughuli zinazohusu umaskini ambazo hazihitaji msaada wa fedha lakini ni muhimu katika upunguzaji wa umaskini. Kazi za PRSP imehusisha mazungumzo ya ushauriano baina ya washika dau kitu ambacho kimechangia kuweka msingi madhubuti wa kutekeleza madhumuni ya Sera za maendeleo ya nchi pamoja na mapngo wa wa kupunguza umaskini. Juhudi madhubuti kuelekea kwenye upunguzaji wa umaskini zinazohuchukuliwa na washirika wa kimataif bado zinatekelezwa nje ya mfumo wa bajeti ya Serikali kuu. Ili kuhakikisha kwamba maendeleo ya kiwango cha juu kinapatikana katika upunguzaji wa umaskini na fedha iliyoombwa kwa shughuli hiyo inapatikana, jitihada zitazidishwa na mipango kutekelezwa kulingana na umuhimu wake. PSRC, wakati inaweka mipango dhidi ya umaskini pia itashughulikia marekebisho ya mifumo, kuweka uchumi imara na kuendeleza kustawisha uchumi kufuatana na mpango wa dira ya Taifa wa maendeleo wa 2025 Aidha kufuatana na mpango wa muda mrefu wa kuondoa umaskini Serikali imeanzisha (kuanzia Julai 1998) Multilateral Debt Fund ambamo Nchi hisani zimekubali kuchangia jumla ya US$ 145.56 millioni. Hadi kufikia Desemba 1999, US$ 109.5 milioni zilikwisha changwa kati ya fedha zilizoahidiwa kwa ajili ya kulipia mipango inayohusika na aya na elimu. Wapo watendaji wengi wanao jushughulisha na usimamizi wa mipango ya PRSP ambao huhusika na ukusanyaji wa taarifa, uchanguzi na matumizi ya taarifa. Jukumu kuu la kusimamia suala la umaskini kitaifa liko chini ya ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ni chambo cha Serikali kilichopewa jukumu la kuratibu masula ya kuondoa umaskini kwa kuhakikisha kwamba washika dau wote wanaohusika wanashirikishwa katika masuala ya ufuatiliaji.

No comments:

Post a Comment