Sunday, November 25, 2012
Jinsia
insia ni suala linalohusu maendeleo kwa sababu kutokuwepo kwa uwiano na usawa kama ilivyo sasa katika jumuiya, kunaizuia jamii kutambua uwezo wake kamili katika shughuli zote zinazohusu maendeleo ya uchumi, jamii na maeneo ya siasa.
Serikali iko mbioni kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia yanaunganishwa katika kutayarisha mipango na bajeti ili kuimarisha uhusiano baina ya wanaume na wanawake ambao ndiyo unatoa msukumo kwa maendeleo. Kwa hiyo, pasikuwepo uhusiano imara kwa pande hizo mbili kasi ya maendeleo itapungua.
Dira ya Maendeleo ya 2025 ya Tanzania inalengo la kuwapatia watu wake hali ya juu ya maisha, kufanikiwa katika kupata utawala bora wa kuheshimu sheria pamoja na kuendeleza uchumi imara na wa ushindani. Ili kufanikiwa kuleta usawa wa jinsia na kuwapa uwezo wanawake katika maeneo ya jamii, uchumi, uhusiano wa siasa na utamaduni lazima yatiliwe maanani. Jinsia imewekewa kipaumbele katika masuala yote ya Maendeleo ili kukuza uchumi wa Taifa, masuala ya siasa na utamaduni lazima yaangaliwe. Jinsia ni mkondo mkuu ambao vipengele vyote vya maendeleo hupita ili kuimarisha uchumi wa Taifa, siasa na masuala ya jamii na utamaduni.
Nchini Tanzania inakadiriwa kwamba wanawake hasa wa vijijini wanatoa asilimia 80 ya wafanyakazi katika eneo la kijiji na hivyo kutoa asilimia 60 ya chakula kinachozalishwa. Ingawa wanawake ndiyo wazalishaji wakubwa wa mazao ya biashara, mazingira hayawaruhusu kumiliki mali zao. Wanawake hawana maamuzi juu ya masula ya uzazi, kwa mfano wanawake wengi hawana uwezo wa kuamua idadi ya watoto katika familia ingawa wao ndiyo wenye jukumu kubwa la kulea mtoto.
Jinsia katika mfumo wa ajira kwa shughuli za kilimo au zisizo za kilimo nchini Tanzania imebadilika katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kwani wanawake wengi zaidi wanajishughulisha na masuala ya biashara na wanawajibika zaidi katika kuchangia fedha kusaidia mahitaji ya nyumbani. Wanawake wako mstari wa mbele katika kupanua biashara ndogo ndogo ambazo hujulikana kama sekta isiyo rasmi.
Jinsia na Ajira
Wanawake na wanaume wameonekana kuajiriwa kwa njia mbalimbali, na kwa masharti tofauti siyo tu hapa Tanzania bali ulimwenguni kote. Tofauti zinaonekana katika wanawake na wanaume, pamoja na kati ya makundi tofauti ya wanawake (wa vijijini – mjini, tajiri – maskini, aliyesoma – hakusoma) na wanaume. Baadhi ya kazi zimepigwa chapa kwamba ni za “wanaume” au “wanawake”, kwa sababu ya taratibu za jamii katika mgawano wa kazi ambao unatamka majukumu mbalimbali ya wanaume na wanawake. Wanawake karibu wote wa vijijini kazi zao ni kubeba maji, kuni, kubeba kichwani mazao ya shamba, kutunza watoto, kupika na kulima.
Mambo yasiyothibitishwa ya kijinsia, lakini yanachangia katika mfumo ambapo wanawake wanapangiwa kulipwa mshahara ya chini hupangiwa kazi zisizo za ufundi au kazi ambazo ufundi wake hautambuliki katika sekta rasmi na zisizo rasmi za uchumi.
Masharti ambayo wanawake na wanaume hushindania kupata ajira ni matokeo ya mahusiano ya kijamii ikijumuisha maeneo ya utamaduni, uchumi na siasa. Maeneo hayo ni pamoja na imani potofu kwamba jukumu la kwanza la mwanamke ni kukaa nyumbani kutunza familia na kwamba kila mwanamke anamtegemea mwanaume kwa masuala ya mahitaji ya fedha.
Suala la ustadi mara nyingi linaamuliwa pasipo sheria wala kanuni na huhusisha mila na desturi. Ustadi unaohusishwa na wanawake mara nyingi hauthaminiwi na huwekwa daraja la chini, hata kama unahusisha masuala mazito kama ya kulea watoto, kilimo na kadhalika.
Uwezo wa kufahamu Sheria
Nchini Tanzania haki za sheria za wanawake na haki za binadamu ziliathiriwa na ufahamu pungufu wa sheria kati ya wanawake. Sababu kubwa ni kwamba mfumo wa sheria unaotumika hauwafikii wanawake wengi wanaoishi maeneo ya vijijini. Ziko pia sheria zinazobagua mfumo wa sheria ambao hautoi amri za kulinda, au kuzuia uchunguzi usiozingatia unyeti wa suala na mashtaka yanayohusu kesi za ukatili dhidi ya wanawake na watoto. kama ilivyo katika jamii nyingi katika Afrika mila na desturi zinawabagua wanawake katika masuala ya kurithi mali hasa ardhi pamoja na kuruhusu ukatili didi ya wanawake kwa mfano kupiga mke, kubaka, kutahiri wanawake pamoja na kuwepo kwa sheria nyingi, amri za kanisa na desturi na mila ambazo huenda zinagongana.
Ili kuondokana na hali hii, Serikali ya Muungano wa Tanzania imejizatiti kuboresha uwezo wa kufahamu haki za wanawake kwa mpango wa kutoa elimu, kampeni za kuwaelimisha wanawake na wanaume juu ya haki za wanawake kwa madhumuni ya kuongeza hadhi ya wanawake kwa kuzidisha upeo wao wa ufahamu kuhusu sheria na haki zao. Serikali pia imeweka katika mfumo wa sheria taratibu za kuwalinda wanawake na watoto.
Utaratibu huu unajumuisha kufundisha masuala ya haki za binadamu katika shule na katika mipango ya elimu ya watu wazima. Mkazo wa mafunzo ya sheria ya kuwawezesha wanawake kupata msaada zaidi mara wapatapo matatizo yanayohusu haki zao za Sheria, unatokana na sababu kwamba mfumo wa sasa wa Sheria hauwafikii wanawake wengi hasa waishio maeneo ya vijijini.
Serikali kwa kushirikiana na vyama visivyo vya kiserikali (NGO’S) ilikuwa inafanya kazi ya kuondoa vipengele vinavyobagua vilivyo katika sheria zinazotumika ambazo hazitoi haki na uhuru wa wanawake. Serikali imepanga kurekebisha sheria za mirathi, sheria ya ndoa na inaandaa mkutano juu ya haki za watoto. Serikali iko mbioni kuanzisha Tume ya Haki za Binadamu Tanzania. madhumuni ya kuanzisha tume ni kuunganisha mipango ya kuongeza njia za kupambana na vitendo jeuri vya haki za binadamu.
Serikali imepitisha sheria kadhaa katika kutoa upendeleo kwa wanawake kwa mfano “Sexual Offences Special Provision Act of 1998, Land Law Act of 1999 na Village Land Act of 1999. Sheria hiyo ya kwanza inawalinda wanawake, wasichana na watoto kutokana na kunyanyaswa kijinsia na matendo mabaya. Sheria mbili za mwisho zinahuisha na kufuta sheria za awali zinazohusu masuala ya adhi na hivyo kuwawezesha wanawake kufaidi haki sawa na wanaume za kuweza kupata, kumiliki na kudhibiti ardhi.
Ili kusaidia juhudi hizo zilizotajwa hapa juu, vyombo vya habari vilitumika katika kuhamasisha na kuweka bayana mfumo wa sheria kwa wananchi. Serikali na NGOS wameyachambua na kukemea maeneo ambayo haki za binadamu bado zinatendewa ufidhuli. Serikali na NGOS pia zimewahamasisha wananchi na wanawake kuhusu ukatili wa jinsia.
Hata hivyo serikali imepambana na matatizo kadhaa katika jitihada za kuongeza uelewa wa sheria kwa wanawake wa vijijini. Matatizo hayo ni pamoja na ufinyu wa fedha za kuwezesha kuwahamasisha wanawake wa kijijini juu ya haki zao na kuwapatia msaada wa kisheria mbele ya mahakama za sheria.
Kuwapa uwezo wa kiuchumi wanawake na kufuta umaskini
Katika Tanzania asilimia 60 ya wanawake nchini wanaishi katika umaskini unaokithiri. Hayo ni matokeo ya kuongezeka kwa umaskini kati ya wananchi wanaoishi vijijini na mijini, kuongezeka kwa pengo kati ya matajiri na maskini, kati ya wanawake na wanaume na kati ya wanawake wenyewe. Katika sekta ya vijiji na sekta ya vitongoji vya miji, wanawake wanabeba mizigo mizito zaidi kwa sababu ya mila na desturi, wanawake wanakosa haki ya kumiliki mali na pia wanakosa elimu ya kutosha ya kufahamu huduma zilizopo za kupata mikopo. Na kutokana kiwango chao cha elimu kuwa cha chini, maarifa na ufundi wa kuendesha kazi zao huwa pia wa chini. Wanawake wengi pia hutegemea teknolojia duni ambayo hutumia muda na nguvu zao nyingi.
Ili kukabiliana na tatizo hilo, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejizatiti kuongeza uwezo wa kiuchumi wa wanawake kwa kuweka huduma za mikopo ili zipatikane kwa wanawake wengi, pamoja na kujenga na kuwasaidia wanawake kupata maarifa ya biahsara, kuongeza uwezo wao wa kuongoza, kuongeza mafunzo na upatikananji wa teknolojia. NGO’S zinazotoa mikopo kwa wanawake zimeongezeka tangu kufanyika kwa mkutano wa 4 wa dunia wa wanawake mjini Beijing. NGOS nyingi na mashirika ya misaada yamejitahidi sana kutoa mikopo kwa wanawake kwenye ngazi za kijiji. Wanawake wamepewa mafunzo ya kushughulikia masuala ya mikopo. Juhudi hizo zimeongeza ushirikishwaji wa wanawake katika miradi ya kuongeza kipato.
Tatizo moja ni upatikanaji wa uwezo wa kufuatilia matumizi ya fedha. Tatizo lingine ni kujitokeza kwa idadi kuwa ya vikundi vinavyohitaji hudma hiyo ambayo fedha kintakiwa kufanywa ni kuziongezea uwezo NGO’s ili ziweze kutoa huduma za mikopo kwa walengwa wengi zaidi na papo hapo kuziwezehsa NGO’s kujiendesha zenyewe.
Serikali imeshauri na kuyahimiza mashirika binafsi ya fedha kutoa mikopo kwa wanaake. Nafasi zaid zimetolewa kwa mafunzo ya ustadi wa biashara na katika kutumia teknolojia rahisi kutengeneza chakula na nguo. Walengwa wengi wa mifuko ya mikopo wanaishi mijini na taratibu za kupatikana mikopo zinakumbua.
Serikali itaweka juhudi zaidi ili wanawake wengi zaidi wanashiriki katika shughuli za uzalishaji za kiuchumi kwa msaada wa mikopo. Seriali kwa mfano itaweka mkazo zaidi katika kuhamasisha wenye fedha binafsi kuwapa mikopo wanawake na Seriklai itakuwa mmoja ya wadhamini. Serikali pia itaongeza juhudi ya kutafuta masoko kwa bidhaa yatakazalishwa na wanawake. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na NGO’s iko katika harakati ya kuhakikisha kwamba jinsia inaingizwa katika kuandaa mipango na bajeti za sekta zote.
Zaidi ya hayo, Serikali itaongeza jitihada ya kuwahamasisha wanawake kushiriki katika maonyesho ya Biashara ili bidhaa zao ziweze kuonekana na watu wa aina zote. Idadi ya wanawake wanaoshiriki katika maonyesho ya kimataifa ya biashara imekuwa inaongezeka kutoka wanawake 100 katika mwaka 1996 hadi 200 katika mwaka 1999 na hata ubora wa bidhaa zao umeongezeka. Juhudi za kuwahimiza wanawake kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya biashara zimeendeshwa na Serikali, NGO’s zinazoshugulika na kupunguza umaskini na vyama vya wanawake wafanya biashara.
Lakini Serikali na NGO’s bado zinahitaji kuendesha mafunzo juu ya uzalishaji bidhaa zenye ubora na maarifa ya kuuza bidhaa; kuhamasisha wanawake kuwashawishi wanawake wenzao kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya biashara; kuanzisha maongyesho kwa ajili ya mazao ya kilimo na bidhaa za viwandani katika ngazi zote. Serikali inahitaji kufanya utafiti kuhusu nafasi za uwekezaji kwa wanawake na matatizo yaliyopo katika upatikanaji wa mikopo; kuendeleza uanzishaji wa benki ya wanawake ambayo itatoa kipaumbele kwa kuwapa mikopo wanawake wawekezaji. Serikali pia inahitaji kuwaelimisha wanawake juu ya upatikanaji wa huduma za mikopo, kuhimiza wanawake kushiriki katika mipango ya kuweka akiba, kuwashawishi wafanya biashara wanawake wa mijini kuwekeza katika mipango ya kupunguza umaskini vijijini pamoja na kutayarisha na kusambaza taarifa za mikopo kwa ajili ya wanawake walioko katika Sekta isiyo rasmi.
Katika kuteKELEZA makubaliano yaliyofikiwa Bejing, Serikali imefanya uchambuzi wa wafanya biashara wanawake kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya maarifa ya kufanya biashara na kuendesha biashara katika Sekta isiyo rasmi. Nia ya Serikali ilikuwa ni kutoa mafunzo kwa asilimia 20 ya wafanya biashara wanawake kila mwaka. Idadi ya wanawake hao wanaopata mafunzo imekuwa inaongezeka lakini haijafikia asilimia 20 iliyopangwa. Moja ya sababu ya kushindwa kufikia nia hiyo ni ukosefu wa taarifa kuhusu idadi ya wanawake wanaoshiriki katika mpango huu na hivyo kuwa vigumi kupata kipimo cha uhakika kuthibitisha jitihada hizo za Serikali. Lakini bado Serikali inahitaji kuongeza jitihada zake za kutoa mafunzo kwa wafanya biashara wanawake hadi kufikia asilimia 20 kama ilivyolenga. Serikali inahitaji kufanya utafiti ili kupata taarifa ya idadi ya wanawake wanaopata mafunzo na kufahamu jinsi gani imesaidia katika ustadi wao.
Kwa vile shughuli za kuongeza mapato zinazidisha msululu wa kazi za wanawake, watu binafsi na mashirika ya binafsi, yanahimizwa kuendeleza na kukuza teknolojia sahihi na nafuu ambayo itapunguza makali ya kazi za wanawake za nyumbani na za shamba.
Serikali imetumia mbinu mbalimbali za kuongeza uwezo wa wanawake kiuchumi. Mbinu ya kwanza ni kufungua milango kwa wanawake ili wao waweze kumiliki ipasavyo njia za uzalishaji wa bidhaa. Kwa hiyo Serilaii ilirekebisha sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 na kutunga Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, Sheria ya Vijiji ya 1999. Sheria hizo zinamwezesha mwanamke kumiliki mali ya ukoo na familia kama ilivyo kwa wanaume. Serikali kwa kushirikiana na NGO’s na mashirika ya kimataifa wamechukua hatua ya kuwaelimisha wanaume na wanawake juu ya umuhimu wa wanawake kumiliki ardhi na njia nyingne za uzalishaji. Majukumu ya wanawake na nchango wao kwa familia na jamii katika mtiririko wa maendeleo umesisitizwa. Tatizo lingine ambalo bado linatakiwa kushughulikiwa ni kuelimisha jamii kuhusu mabadiliko haya na jinsi gani wanawake wanaweza kufaidika kutokana na mabadiliko hayo.
Tatizo kubwa liko kwenye mazoea na utamaduni. Ni vigumu kubadilisha msimamo katika jamii. Msukumo mkubwa uliopo ni kuanzisha uhamasishaji wa masuala ya junsia kwa madhumuni ya kubadilisha msimamo wa jamii.
Serikali inapanga kufanya uchunguzi wenye madhumuni ya kuzitambua NGO’s na kuzisaidia kuimarisha uongozi wao na kuongeza upeo wa uwezo wao.
Kumekuwepo na msaada wa kiufundi katika kilimo. Serikali imewaomba na kuwahimiza wahisani kusaidia utafiti juu ya matumizi ya dawa za asili za kuulia wadudu.
Wanawake sasa wanajishughulisha zaidi katika biashar aza samaki na ufugaji wa nyuki na hivyo kupata mwanya wa kuingia kwenye eneo la maliasili.
Kikwanzo ni imani za kale kwamba wawake hawawezi kufanya kazi za biashara. Jitihada lazima bado ziongezwe kuwawezesha wanawake kupata nafasi nzuri zaidi kwenye maliasili. Ni jambo la maana kuwa wananchi wahamasishwe kijinsia kuhusu matumizi ya mali, miliki na uongozi ili kutokomeza umaskini.
Uwezo wa kisiasa wa wanawake na utoaji wa maamuzi
Kimila, nafasi ya mwanawake nchini Tanzania ni ya chini kulinganisha na wanaume. Wanawake walikuwa hawatarajiwi kuongoza katika kutoka maamuzi kutoka ngazi ya nyumbani hadi ya Taifa. Kwa desturi za familia, wanaume ndiyo wanotambuliwa kuwa wakuu wa nyumba. Desturi hizo zimeegemea sana katika muundo wa baba, ambao unawanyima wanawake nafasi ya kushawishi katika kupanga mgao wa mali za nyumbani, katika ngazi ya taifa, desturi zilizopo zinaongoza katika uchaguzi na kuteua wanawake katika nafasi za juu na hivyo kupunguza sauti za wanawake katika kuchangia kikamilifu katika taratibu za kutoa maamuzi na kuandaa mipango.
Serikali inatamba kwamba maendeleo na mafanikio ya wanawake katika kufanikisha usawa na jinsia ni suala la haki za binadamu na ni kigezo cha kuelekea kwenye haki ya jamii. Serikali ya Tanzania inatamka kwa uthabiti thamira ya kuendeleza haki za wanawake kwa ajili ya maendeleo ya taifa na dunia. Serikali imeweka saini makubalioano ya kikomesha aina yote ya ubaguzi dhidi ya wanawake (Convention on the Elimination of all forms of Discrimination Against Women) (CEDAW). Zaidi ya hapo, Serikali im eweka ahadi ya kushughulikia makubaliano yaliyofikiwa Beijing (Beijing Platform for Action) ambayo yamedhamiria kutokomeza kabisa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake na kuungana na vyombo vingine vya kimataifa vya haki za binadamu katika kuleta usawa wa jinsia. Kuwasidia wanawake waweze kushiriki katika siasa na kutoa maamuzi ni moja ya maeneo manne Tanzania inapambana nayo.
Serikali imerekebisha kanuni na imechukua hatua za dhati za kuwajumuisha wanawake katika utoaji wa maamuzi. Mwaka 2000 Bunge lilipitisha sheria ya viti vya wanawake. Katika mabaraza ya Serikali za mitaa wanawake wamehakikishiwa asilimia 33 ya viti wakati Bunge la muungano wamehakikishiwa asilimia 20 ya viti.
Ni mipango ya Serikali kwamba itaongeza ushirikishwaji wa wanawake katika siasa hadi kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2005. Katika uchaguzi wa mwaka 2000 wanawake walihamasishwa kugombea viti vya majimbo na viti maalum kwa wanawake ndani ya asilimia 30 vilivotengwa bungeni. Juhudi zaidi zilifanywa kuhakikisha kuwa idadi kubwa iwezekanavyo ya wanawake ijiandikishe kama wapiga kura na wagombea. Kampeni ya vyombo vya habari na mikutano ya hadhara ilikuwa moja ya mbinu zilizotumika kufanikisha mpango huu.
Mpango mwingine ulikuwa ni kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi za kutoa maamuzi kwa kuwateua wanawake kushika nafasi katika Serikali na Idara nyingine za Serikali. Uamuzi wa Baraza la Mawaziri namba 23 wa 1996 pamoja na mambo mengine uliidhinisha utekelezaji wa mpango wa kuongeza wanawake katika ngazi zote na kutoa maamuzi kwa mfano kama wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi, wakuu wa Mashirika, Makamishna na Wawakilishi wa Taifa. Mpango mwingine ni uzingatiaji wa masuala ya jinsia katika idara ya utumishi na kuunda kitengo cha kuweka taarifa za wanawake, na sifa zao kwa kutumiwa na mamlaka za ajira pale zinapohitajika.
Hatua mbalimbali zilichukuliwa ili kufanikisha upatikanaji wa asilimia 30 ya viongozi wanawake. Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuendesha kampeni kupitia vyombo vya habari warsha na semina kwa madhumuni ya kuwahamasisha wanawake kugombea nafasi za uongozi, kustawisha taarifa za wanawake na kuwa na idara ya maendeleo ya wanawake mikoani na wilayani ambavyo viko katika mfumo wa serikali. Aidha, hatua zilichukuliwa kufuatilia utekelezaji wa uamuzi wa Baraza la Mawaziri wa 1996 wa kuwateua wanawake katika nafasi za jinsia katika idara ya utumishi, na kurekebisha muhtasari wa masomo ya uraia katika ngazi zote za elimu ili kuunganisha elimu ya maendeleo ya ujuzi wa katika uongozi. Ujio wa vyama vingi nchini Tanzania wakati wa kipindi cha kutekeleza maamuzi ya Beijing Platform for Action pia kulichangia kuweka mazingira mazuri ya kuanzisha vyama vya uraia. Idadi kubwa ya vyama vya NGO’S na CBO’S vya wanawake vilianzishwa pamoja na matawi ya wanawake katika vyama vya siasa vilivyosajiliwa nchini. NGO’S hizo za wanawake na matawi ya wanawake katika vyama vya siasa vinatoa nafasi nzuri kwa wanawake kuzungumzia siyo tu masuala yahusuyo jamii na uchumi bali masuala ya siasa pia. Mazungumzo yanayoendelea kuhusu zoezi la kurekebisha Katiba pia yanatoa nafasi nyingine ya kujumuisha haki za wanawake katika Katiba ya nchi.
Aidha ujio wa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania uliongeza uwanja wa siasa na kutoa nafasi ya kuzungumzia marekebisho ya vipengele vilivyoko katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania unapotokea umuhimu wa kufanya hivyo.
Katiba inatambua uwezo na haki ya wanawake ya kushiriki katika siasa masuala ya jamii na uchumi wa kuleta uhai wa nchi. Haki ya kupiga kura na haki ya kugombea kiti katika uchaguzi ziko sawa kwa wanaume na wanawake. Hii ilidhihirisha wazi katika uchaguzi mkuu wa 2000. Na hii ni ishara tosha kwamba yako mazingira mazuri kwa wanawake kushiriki kwa uhuru na kwa usawa na wanaume katika siasa na katika kutoa maamuzi nchini Tanzania.
Kuendeleza nafasi za Wanawake katika Elimu Mafunzo na Ajira
Elimu ni ufungua wa ukombozi na chombo muhimu cha kupunguza matatizo ya jamii na uchumi. Wanawake wanapata vikwazo vingi kupata elimu na mafunzo katika ngazi zote. Vikwazo hivyo ni pamoja na mazingira yasiyo mema hasa katika kufundisha hisabati na masomo ya ufundi na sayansi ambayo yanahitaji ushindani na hali fulani ya kujiamini ambayo inakosekana kwa wasichana. Utoro, mimba, ugumu wa maisha na kufunga ndoa katika umri mdogo vinawazuia wasichana katika kukamilisha masomo yao. Desturi za jamii zilizopo zinapendelea na kuendeleza elimu kwa wavulana na kuonyesha kujali kidogo tu katika elimu ya wasichana.
Serikali imedhamiria kuongeza nafasi za elimu kwa wanawake ili kupunguza pengo baina ya wavulana na wasichana katika shule za msingi na sekondari. Kwa mfano wakati wasichana wanaoingia katika shule za msingi ni asilimia 50 katika shule za sekondari wanaoingia ni asilimia 46.
Idara ya wasichana wanaojiunga na vyuo vya juu inaendelea kupungua (katika ngazi ya Chuo Kikuu waliojiunga ni jumla ya asilimia 17). Moja ya vikwazo vinavyowazuia wanawake kupata kazi za maana ni elimu duni na kukosa ujuzi wa kutosha katika kazi za kiuchumi za kuzalisha bidhaa. Madhumuni ya Serikali ni kuongeza idadi ya wanawake katika elimu ya ufundi, elimu ya ngazi ya kati na elimu ya juu. Serikali pia imerekebisha elimu na mafunzo katika ngazi hii ili yahusishe upatikanaji wa kazi. Hatua zinazochukuliwa na serikali ni kama ifuatavyo:
¨ Kuanzisha vyuo na vituo vya mafunzo na shule za sekondari za ufundi za wasichana.
¨ Kuongeza wakufunzi wa kike katika vituo na vyuo vya ufundi.
¨ Kufanya utafiti juu ya ufundi wa kike katika vituo na vyuo vya ufundi.
¨ Kufanya utafiti juu ya ufundi na soko la kazi.
¨ Kuchambua na kuondoa maandishi katika vitabu na aina nyingine ya vifaa vya kufundishia vyenye kuonyesha ubaguzi wa jinsia.
¨ Kufundisha wakufunzi kuwa wenye kutambua jinsia.
¨ Kuwahamamisha wazazi kuwatia moyo na kuwawezesha wasichana kujiunga na vyuo vya ufundi.
¨ Kuwawezesha wasichana kukutana na wanawake wasomi waliofanikiwa ili wawe mifano kwao pamoja na kuwawezesha wasichana kwenda kwenye ziara za mafunzo.
¨ Kuanzisha kozi na mafunzo katika ufundi yatakaosaidia kuwapatia wanawake kazi zenye manufaa.
¨ Kuongeza huduma za bweni kwa wasichana.
¨ Kutengeneza mfumo wa mafunzo ambayo yatajumuisha aina nyingi za ustadi ufundi wa kuendesha biashara na masuala yanayoendana na mafunzo hayo.
¨ Kutumia mfumo wa mafunzo ambao unalenga kwa kuwasaidia wanawake na wasichana.
¨ Kuanzisha kozi fupi fupi, vyuo vya huria kwa wakati maalum na pahali panapokubalika na wote ili kukidhi mahitaji ya wanawake ambao wana matatizo ya muda wa kutosha.
¨ Kuanzisha vituo vya mafunzo na karakana ili kuwapa huduma zipasavyo wanawake.
¨ Kuanzisha mfuko wa mafunzo kwa wanawake ili kuongeza uwezo kao wa uongozi na wa kutoa maamuzi.
Ni kweli kwamba wasichana na wanawake hata wale waliomaliza shule na mafunzo hawapati nafasi sawa za kazi. Vikwazo vinakvyowakabili wanawake katika kazi ni ukosefu wa huduma za kulelea watoto wadogo na shule za chekechea pamoja na vifaa maalum vya afya na usalama viwandani vilivyotengenezwa maalum kwa mahitaji ya jinsia. Ili kupunguza matatizo haya. Serikali imepanga yafuatayo:-
¨ Kuendeleza na kusimamia masuala ya afya katika sehemu za kazi kwa kuzingatia jinsia.
¨ Kuanzisha na kusaidia kuendesha vituo vya kulelea watoto kwa wanawake wafanyakazi wenye watoto.
¨ Kuwashawishi waajiri kwenye sekta binafsi kuwapatia akina mama muda wa kunyonyesha watoto wao.
¨ Kuongeza juhudi za kuwahamasisha waajiri juu ya masuala ya maendeleo ya wanawake.
¨ Kuweka mkazo juu ya amri za usalama katika sehemu za kazi kwa ajili ya wanaume na wanawake.
¨ Kurekebisha sheria na amri zitumikazo ambazo ni vikwazo kwa wanawake wanaofanya kazi katika sekta binafsi.
¨ Kufanya utafiti kuhusu mitindo na tabia za kazi za wanawake katika sekta rasmi na zisizo rasmi pamoja na kukomesha taarifa zinazowadhalisha wanawake kazini.
¨ Kuwaelimisha watumishi wa serikali juu ya miundo ya utumishi, sheria au taratibu na jinsi ya kujiendeleza kazini.
Nafasi
Katika kushughulikia masuala ya jinsia ni muhimu kuwa macho na kuweka bayana masuala yanayosaidia na yale yasiyo na faida katika kuleta mazingira mazuri katika maeneo ya jamii, siasa na utamaduni wa taifa. Masuala manne yanayosaidia ni vyema yatamkwe.
Kwanza, Tanzania imeanzisha Tume ya kurekebisha Sheria (Legal Reform Commission) kuchunguza na kutoa ushauri kwa serikali juu ya sheria zinazogandamiza ili zifutwe au kurekebishwa. Pili, Tanzania imeweka mfumo wa Serikali ambao una ngazi za kitaifa, kimkoa, serikali za mitaa, wadi na ngazi za kijiji ambazo zinaweza kuhamasisha juu ya masuala ya jinsia.
Tatu, Tanzania hivi sasa inayo mazingira mazuri ya siasa ambayo yanatambua na kutekeleza usawa wa jinsia.
Mwisho, Tanzania ni mwanachama wa “Beijing Platform of Action” na “Convention on the Elimination of all forms of Discrimination Against Women (DECAW) na ni mtekelezaji halisi wa makubaliano hayo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment