Sunday, November 25, 2012
Ufumbuzi wa kisaikolojia wa tatizo la ugumba
Ni ukweli usiopingika kuwa ndoa nyingi zimepoteza furaha kutokana na watoto kukoseka miongoni mwa wanandoa. Wanawake na wanaume wamejikuta wakiangukia katika mikono ya matapeli wanaojiita waganga na kufanyiwa mambo mengi ya ajabu, ikiwa ni pamoja na kufanya mapenzi na mizuka au na watu ambao hawakuwatarajia ili tu waweze kupata watoto.
Hakuna ubaya wa kutafuta tiba ya ugonjwa endapo upo, lakini kutafuta tiba ya ugonjwa ambao haupo ni kuchosha mwili na matokeo yake huwa ni mabaya zaidi. Uchunguzi uliohusisha matatibu kutoka hospitali na vituo vingi vya afya unaonesha kuwa wagumba wengi wanaosaka tiba hospitalini wamebainika kutokuwa na matatizo ya kibaiolojia. Ninaposema kibaiolojia nina maana kwamba wanandoa wengi wagumba wamekutwa wakiwa na uhai katika viungo vyao vya uzazi.
Katika ulimwengu wa leo idadi ya watu wanaokosa watoto bila kuwa na sababu ya msingi inatajwa kuwa ni kubwa na kila siku wasichana na wavulana wanaingia katika chumba hiki cha huzuni isiyojulikana chanzo chake. Kukosa uzazi bila sababu ni tatizo ambalo limekuwa likizisumbua akili za wahitaji watoto wengi na mwisho kuwagotesha katika mawazo ya kurogwa na sababu kubwa ikiwa ni kutojulikana kwa chanzo cha wazi cha kutokuzaa kwao.
Ukweli pekee ambao nimekusudia kuuzungumza leo kuhusiana na wasiokuwa na matatizo ya uzazi kutokuzaa ni ule ambao umeshawekewa misingi na watafiti walioandika taarifa yao katika jarida la Minerva Ginecologica la nchini Italia kwamba uchovu unaoletwa na mawazo ndiyo unaochangia kwa kiasi kikubwa watu wasipate watoto licha ya kwamba kibaiolojia hawana matatizo.
Tafiti za hivi karibuni zimebaini kuwa, wanawake wengi wenye viungo salama lakini hawazai, wana kiasi kikubwa cha homoni ya Cortisol inayoletwa na uchovu. Kwa mujibu wa utafiti huo aina hii ya homoni ndiyo inayosimamisha mchakato wa uzalishaji mayai kwa wanawake wakimbia riadha. Hivyo basi uwiano huu wa kasoro za ukuzaji mayai kati ya wakimbia riadha na wanawake wagumba unaweka usawa baina ya uchovu mkubwa wa mazoezi ya viungo na ule uchovu unaotokana na msongo wa mawazo ya ugumba.
Uchovu wa kihisia huweza kumfanya mwanaume au mwanake asiweze kuzaa kabisa katika maisha yake. Hii ina maana kuwa watu wanaotingwa zaidi na mawazo ya kukosa fedha, migogoro katika ndoa zao na kujaribu mara kadhaa kupata watoto bila mafanikio wana uwezekano mkubwa wa kutokuzaa hata kama maumbile yao yataonekana kitabibu hayana kasoro.
Imebainika kuwa watu wengi hujisogeza wenyewe katika nguvu ya kukosa mtoto kutokana na ukubwa wa kiu yao ya kupata mtoto, huku wakilazimisha kimawazo mchakato wa kubeba au kubebesha mimba kwa wakati ulipangwa na malengo yao.
Mkazo huu wa mawazo huwakumba hasa wanandoa na wapenzi ambao wanatamaa ya kupita kiasi ya kupata mtoto katika uhusiano wao. Hawa hujiweka katika uzalishaji mkubwa wa homoni ya Cortisol ambayo huchipuka kwa kasi kutokana na msukumo wa kiu kubwa na ya haraka ya kukumbatia mwana.
Kutokana na ukubwa wa tatizo hili la msongo wa mawazo, imebainika kuwa wagumba wengi wasiokuwa na kasoro katika viungo vya uzazi wanaweza kupona au kupata watoto bila hata kupewa tiba ya miti shamba au vidonge. Tiba yake kubwa iliyobainishwa ni kupatiwa nasaha zitakazowaondolea mawazo tasa, wasiwasi na kutojiamini.
Ukweli wa tiba hii ya ushauri imethibitishwa hivi karibuni na kituo kimoja nchini Marekani kinachojishughulisha na utafiti wa kuzalisha watoto, ambapo majibu yake yalichapishwa katika majarida na mitandao mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa ya kituo hicho asilimia 75 ya wanawake waliokosa watoto ambao walifika kituoni hapo na kupewa ushauri walifanikiwa kuzaa baada tu ya kuhudhuria kliniki na kupewa ushauri uliowatoa katika msongo wa mawazo.
Nasaha ambazo zimekuwa zikitolewa na wataalamu hao si ngumu, bali ni zile zilizojaa maneno yenye kugeuza fikra hasi zenye kuondoa kiu kali ya kupata watoto kwa utashi na nyakati zilizopangwa na wahusika. Pia wagumba hufundishwa namna ya kuepuka migogoro ya kimapenzi na kutoumizwa kupita kiasi na kejeli za watu kuhusiana na kutozaa kwao, huku wakijengewa imani kuwa kuzaa ni suala linalowezekana kwao, hivyo kuwafanya watupilie mbali hofu na mawazo kuwa wao ni wagumba.
Lakini pamoja na nchi zilizoendelea kuwa na vituo vya kutolea nasaha kwa waathirika, bado wanasaikolojia wanakiri kwamba mtu mwenyewe anaweza kujiepusha na uchovu unaoletwa na mawazo kwa kurahisisha tatizo lake kutoka kutowezekana na kuwa linawezekana kutatuliwa. Akili ya mtu ndiyo inayopima na kuongoza utambubuzi wa ukubwa wa tatizo na si kwamba kuna matatizo makubwa na madogo kama watu wanavyofikiria.
Kwa maana hiyo ili mtu ambaye amejiwekea ukuta wa kutozaa kwa msongo wa mawazo yake kama nilivyosema aweze kuzaa lazima aondoe mawazo ya kwamba yeye ni mtu asiye zaa, kwani hakuna mtu wala vipimo vilivyompa majibu ya kwamba ni mgumba. Jambo jingine la kufanya ni kupuuza maneno ya kukatisha tamaa toka kwa watu wengine. Hii ina maana kuwa lawama zozote toka kwa mume/ mke au wanafamili zinazohukumu kosa la mtu kutokuza lazima zipuuzwe na zisipewe nafasi ya kutia simanzi moyoni.
Sambamba na hilo kuna suala la wanawake kuzingatia kalenda zao kwa kujichunguza na kubaini muda muafaka wa kukutana kimwili na mwanaume ili kupata matokeo mazuri ya utungishaji mimba. Kwa mantiki hii kuna wanandoa wengi wameshindwa kupata mtoto kwa kutozingatia siku zenye uwezekano wa kupata mimba ambazi ni siku ya 11 hadi ya 16 tangu siku ya kumaliza hedhi.
Lakini kwa kuwa kuna suala la utumiaji wa dawa za uzazi wa mpango ni budi wahusiaka kusimamisha matumizi yake pindi mtoto anapohitajika ndani ya ndoa. Hata hivyo kuna umuhimu wa kutumia mitindo ya kuvuta kizazi nyakati za kufanya mapenzi, ili kuzipa msukumo wa haraka mbegu kunasa kwenye mfuko wa uzazi.
Sambamba na hilo wanaume wanatakiwa kuepuka ufanyaji holela wa mapezni ili kuzifanya mbegu zikomae na wakati wa tendo kuvuta hisia kali ili kuongeza msukumo wa manii kutoka kwenye uume kwenda kwenye uke. Na jambo la mwisho katika mchakato wa kupata mtoto ni lishe bora miongoni mwa wanandoa. Lazima miili iwe na nguvu za kutosha kusimamia uzalishaji wa mbegu bora. Inashauriwa wanaume waepukane na uvaaji wa nguo za ndani za kubana ambazo zinatajwa kuongeza joto kwenye kiwanda cha kuzalisha mbengu na hivyo kuzidhoofisha.
EXCLUSIVE INTERVIEW WITH REDDS MISS TANZANIA TOP MODEL 2012 (MAGDALENA ROY).
Miongoni mwa Warembo Waliokuwa kwenye ushindani mkubwa kwenye mashindano ya mwaka huu ya Miss Tanzania ni Magdalena Roy.
Huyu Ni Miongoni mwa warembo walioleta ushindani mkubwa kwenye mashindano yale na hasa ikizingatiwa kuwa tayari alishakuwa mshindi kwenye kinyang'anyiro cha Redds Miss Tanzania Top Model na kupata nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye nusu fainali ya mashindano yale.
Nimepata nafasi ya kufanya naye interview Mrembo huyu ambaye pia ni Super Model Na Pia Ni Video Vixen kuweza kufahamu mengi kumhusu na alikuwa na haya ya kusema;
1 . Nini kilikufanya Ufikirie Kuwa model na ulianza lini?
Maggie; nimeanza kujishughulisha na mambo ya fashion kwa ujumla mwaka jana mwezi wa sita na ni kwa sababu ilikuwa kwenye damu yangu tangu zamani na ndio maana sikuona tabu sana kuacha kazi yangu niliyosomea ( Civil Engineering) na kuingia huku kwenye mambo ya fashions pamoja na wengi wa watu kuwa na mtazamo hasi kuwa kazi hii ni uhuni lakini ninaamini nimefanya uamuzi sahihi.
2. Unakumbuka kazi yako ya kwanza kufanya ilikuwa ipi?
Maggie; Kazi yangu ya kwanza ilikuwa ni Dar Fashion Festival ambayo hufanyika kila mwaka na nilipata experience ya kutosha sana na nilikutana na designers wengi ambao walionyesha moyo wa kufanya kazi na mie. Baada ya hapo nikaja kufanya kazi Ya Photoshoot kwenye kampuni za Susneakers Inc Na Pedama Communications Agency Chini Ya Fashion Photographer, Eric Shio Na Mkurugenzi Wa Pedama, Mr. David Ndaiga. Kilichofuata baada ya hapo ni mafanikio zaidi.
3. Unaionaje Tasnia Ya Fashion Kwa Ujumla Hapa Tanzania?
Maggie; Kwa navyoona tasnia ya fashion kwa hapa tanzania inakua tena kwa kasi, models wanaongezeka na Young designers wanakuja kwa kasi sana na hata malipo kwa sasa at least sio mabaya sana hasa nikizungumzia kwa upande wangu.
4. Umewahi kushiriki mashindano makubwa kama Miss Dar City Center, Miss Ilala Na Hatimaye Miss Tanzania, Umejifunza nini na unawashauri nini wanaotamani kuingia kwenye sekta hii?
Maggie; Ni Kweli nimejifunza mengi sana na hasa jinsi ya kuishi na watu tofauti, kuwa na uvumilivu na cha muhimu zaidi msimamo kwenye maisha, nawashauri wanaotaka kuingia humu wawe na effort ya kutosha, when you real need something then go fot it, dont hesitate and have faith. usisikilize watu wanasema nini bali jiamini na usonge mbele.
5. Miss Tanzania ndo hiyo imeisha na umefanikiwa kuwa Redds Miss Tanzania Top Model, Nini matarajio yako ya baadae?
Maggie; Ni kweli nimepanga kuwa kuwa role model kwa wanaochipukia na kuwajengea msingi imara wengine wanaotaka kufika mbali so nitajitahidi kwa khali na mali kuwa international model na kuwa mwanga bora kwa wote wanaotaka kufika mbali.
6. Nani ni role model wako na kwanini??
Maggie; Flaviana Matata ni role model wangu kwa sababu ana juhudi na ninaamini nitafika kuwa kama yeye, hajawahi kuni-dissapoint hata siku moja.
7. Siku za hivi karibuni kumezuka taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa wewe ni LESBIAN na ulitangaza hivyo, Je Ni Kweli Au Lah???
Maggie; Habari Hizo Hazina Ukweli Wowote na ni kwamba ilitokea tu siku moja simu yangu iliibiwa tulipokuwa kwenye event na aliyeiba nadhani alikuwa ananifahamu na sikuwa nimeweka security code hivyo akatumia nafasi hiyo kuweza kuandika hivyo kwenye Facebook Na BBM kwa nia ya kuniharibia kwa sababu nilishakuwa kwenye mashindano.
8. Kwa wasiokufahamu unaweza kuwaeleza ulipotoka na hadi ulipo sasa kihistoria zaidi?
Maggie; Nimezaliwa mwaka 1991 nikiwa ni first born kwa familia yetu na nimesoma shule ya msingi Leganga, Usa-River na sekondari nimesoma Ailanga Seminary iliyopo hifadhi ya taifa ya arusha na baada ya hapo nikajiunga na Arusha Technical College kusomea Civil and Highway Engineering kwa miaka mitatu na baada ya hapo nikaingia kwenye mashindano ya Miss Universe 2011 ambapo nilifanikiwa kuwemo kwenye tano bora na baada ya hapo nikapata nafasi ya kufanya training pale Qatar Airways kwa miezi 3 na baada ya pale ndo kama unavyoona nimefika hapa nilipo leo.
9. Ukipewa nafasi ya kushukuru watu 5 utawashukuru nani na nani??
Maggie; Kwanza ni Mungu kwa kunifikisha nilipo leo, Pili ni Familia Yangu Yote Kuanzia Baba, Mama, Aunty Neema Na Wengineo, Tatu ni marafiki wote, nne ni Manager Wangu Mr. Martin na Endless Fame Management na mwisho ni Fans wangu wote.
10. Ni Swali gani hujawahi kuulizwa na ungependa siku moja uulizwe, na jibu lake ni lipi?
Maggie; ha ha ha ha labda Hobbies zangu, napenda sana music na hasa ya Rihana, Ciara, Nicole, Beyonce,etc. pia mazoezi ya viungo na michezo mbalimbali na pia movies hasa horror movies and series.
Posted by David Ndaiga at 12:08:00 PM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
Reactions:
Friday, November 16, 2012
DHAMBI HIZI 2 HUTASAMEHEWA;
Dhambi zote Mungu anasamehe isipokuwa mbili... Je unazifahamu?
Ninamshukuru Mungu kwa kunipa wasaa huu wa kuongea neno lake hapa. Leo ningependa tuongelee dhambi, wote tunajua Mungu anasamehe dhambi unapomwomba msamaha..., Lakini je tunafahamu kuwa kuna dhambi mbili ambazo Mungu hasamehe?
Kama ulikuwa haufahamu basi ni vyema leo ukazifahamu ili kuhakikisha unajiepusha na dhambi hizo.
- Dhambi ya kwanza ni ya kumkashifu roho mtakatifu. Katika biblia takatifu tunaiona kwenye kitabu cha Mathayo mtakatifu 12: 31-32. Neno la Mungu linasema.......
.......12:31 Kwa sababu hiyo, nawaambieni, watu watasamehewa dhambi na kufuru zao zote, lakini hawatasamehewa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
12:32 Tena, asemaye neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa, lakini yule asemaye neno la kumpinga Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao.
Dhambi ya pili ni kutokusamehe. Hii tunaipata katika kitabu cha Mathayo Mtakatifu 6:14-15, neno la Mungu linasema......
..........6:14 Kwa kuwa kama mkiwasamehe watu wengine
wanapowakosea, Baba yenu wa mbinguni
atawasamehe pia na ninyi.
6:15 Lakini msipowasamehe watu wengine makosa yao,
wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Hivyo basi wandugu ni vyema tukajiweka wasafi mbele za Mungu kila wakati, ili siku ya hukumu tusijejikuta tunahukumiwa kwa dhambi ambazo zinaepukika.
Posted by David Ndaiga at 5:30:00 PM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
Reactions:
Monday, November 5, 2012
New Hit In Town '' Oweoo'' -- J4C
Wengi Walimfahamu kwa mara ya kwanza alipotoka na wimbo wake ulioitwa ''Fimbo Ya Mbali'' akimshirikisha Mkali Q-Jay.
Jina lake kimuziki anaitwa J4C na kwa mara nyingine tena amerudi akiwa na 'Club Banger' Matata sana safari hii na kazi imefanyika pale Arusha katika studio za NoizMekah na wimbo unaitwa ''Oweoo''.
Listen/Download Here;
Oweoo -- J4C
Posted by David Ndaiga at 3:58:00 PM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
Reactions:
Tuesday, October 30, 2012
'' Nataka Kulewa '' -- Diamond
Sikiliza ''Nataka Kulewa '' By Diamond Hapa;
Posted by David Ndaiga at 6:58:00 AM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
Reactions:
Saturday, October 27, 2012
WASHIRIKI WA MISS EAST AFRICA 2012
Wafuatao Ni Baadhi Ya Washiriki Waliokwishateuliwa Na Nchi Zao Wa Mashindano Ya Miss East Africa 2012 Yanayotarajiwa Kufanyika Tarehe 7 December Mwaka Huu Dar Es Salaam, Tanzania.
Fainali za mashindano haya zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano Haya Huandaliwa Na Kampuni Ya Rena Events Ltd.
Ariella Kwizera - Burundi
Akuot Phillip - South Sudan
Ayisha Nagudi - Uganda
Jocelyn Diana Maro - Tanzania
Lula TekleHaiManot - Ethiopia
Rahwa Afeworki - Eritrea
AnnaBelle Pointe - Seychelles
Ellidas Chirwa - Malawi
Posted by David Ndaiga at 7:07:00 AM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
Reactions:
Thursday, October 25, 2012
EXCLUSIVE INTERVIEW WITH JOKATE MWEGELO.
Tulipokuwa tunaelekea mwishoni mwa wiki iliyopita,kuna jambo jipya lilikuwa linatokea. Jokate Mwegelo ambaye kwa wengi hahitaji utambulisho wa kina,alikuwa akizindua kampuni yake inayokwenda kwa jina la Kidoti Loving ambayo itajikita zaidi katika bidhaa mbalimbali zinazoendana na masuala ya urembo.Kwa kuanzia, Jokate alizitambulisha aina nane za nywele(weaving) ambazo Kidoti Loving tayari imeshaziingiza sokoni.
Baada ya pale nilimtafuta Jokate kuongelea zaidi Kidoti Loving na mengineyo. Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC: Jokate,karibu tena na naomba nianze kwa kukupa hongera nyingi sana kwa hatua uliyofikia ya kuzindua rasmi Kidoti Loving Brand.Hongera sana.
JM: Asante sana….
BC: Kidoti bila shaka,na wewe mwenyewe umeelezea kwamba hilo jina linatokana na “birth-mark” uliyonayo hapo usoni kwako. Fine.Unakumbuka ni mtu gani wa kwanza kuanza kukuita kidoti? Na ilikuwaje ukafikia uamuzi wa kuiweka kidoti kuwa ndio brand name?
JM: Mtu ambaye naweza kusema ndio alichangia kwa mapana zaidi jina la “Kidoti” ni mdogo wake rafiki yangu wa karibu sana. Ilikuwa mwaka jana na nakumbuka nilikuwa kwenye pressure ya kutafuta jina la kuweka kwenye meza kwenye hafla ya Red Ribbon. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kushiriki na mwandaaji mkuu wa Red Ribbon Gala,Khadijah Mwanamboka alikuwa akihitaji jina la designs zangu. Nikiwa kwenye pressure hiyo yule mdogo wake rafiki yangu ndio akaniambia kwanini usiziite Kidoti? Basi nikajikuta nasema tu zinaitwa Kidoti na kuanzia hapo ndio jina la Kidoti likawa rasmi na ndio mpaka sasa limeshazoeleka hivyo.
BC: Nguo,nywele na viatu ni miongoni mwa vitu vitatu ambayo vina nafasi ya kipekee kwa binadamu na hususani wa jinsia ya kike. Kwanini wewe umeamua kwamba uanze na nywele na kama ulivyosema, nguo zitafuata. Kwanini nywele?
JM: Yapo mambo kadhaa yaliyochangia uamuzi wa kuanza na nywele. Lakini muhimu zaidi ni kwa sababu kwanza brand yangu nataka iweze kuhudumia mass market hivyo inahitaji investment/capital ya kutosha na vile vile reliable producer.
Nilifanikiwa kuvipata hivi kwa uharaka zaidi kwa upande wa nywele hivyo nikaanza kulifanyia kazi. Na nimefanyia kazi kwa mwaka mzima mpaka jana ndio tumeingia sokoni..
BC: Tunaposikia habari za nywele(hususani hizi za bandia-weaving,wigs,etc) ni vigumu wakati mwingine kwa mtu wa kawaida kuelewa tofauti inayoweza kuwepo katika brand fulani mpaka nyingine.Kwa lugha nyepesi tu Kidoti Loving inajitofautisha namna gani na nywele zingine zilizopo madukani?
JM: Kama nilivyosema awali tumefanyia kazi hili suala kwa muda wa mwaka mzima. Na ninaposema kazi, ninamaanisha ninamaanisha pamoja na utafiti wa kina kujua nini hakipo kwenye soko la sasa hapa nchini kwa mfano, ambapo sisi tunaweza kuingia sasa.
Nywele za Kidoti ni za kiwango cha hali ya juu lakini muhimu zinapatikana kwa bei nafuu. Tumezijaribu na wasusi mbalimbali na wamezipenda kuanzia material yake, urahisi wake wa kusukia, haizifungamani, nyepesi, style na rangi tulizochagua ni za kisasa kabisa. Na hata branding/packaging ina mvuto wa kipekee.
BC: Mwaka 2006 ulishiriki mashindano ya Miss Tanzania na kuibuka mshindi wa 2. Baada ya hapo ukaenda au kurudi shuleni na kupata degree yako.Unadhani ushiriki wako katika masuala mbalimbali ya urembo na elimu vimekusaidia vipi kujiandaa na hii ngwe ya ujasiriamali ambayo umeianza rasmi?
JM: Urembo umenisaidia kupata platform ya ku-network na kuonekana na style zangu mbalimbali ambazo zimekuwa zikivutia watu mbalimbali mpaka wengine kuniita “fashionista”. Pia nimekuwa nikishirikiana na wabunifu wa mitindo na shughuli zingine ambazo ziliwavutia hata business partners wangu na kujenga imani yangu kwao.
Lakini shule imenisaidia zaidi kwenye jinsi ya kupanga mikakati na kuelewa soko na jinsi ya kuingia sokoni.Pia discipline ya kazi na professionalism kwenye kazi.
BC: Wakati wa uzinduzi wa Kidoti Brand umekaririwa ukisema kwamba unaanza ujasiriamali rasmi ili uweze kujitegemea na kusimama wewe kama wewe. Unaweza kuipanua kidogo hoja hiyo? Ulikuwa unamaanisha nini hasa?
JM: Kama kuna kitu nakiogopa maishani ni kuombaomba au kuwa tegemezi kwa mtu fulani hasa mwanaume. Naona ni kama utumwa hivyo. Iko kwenye damu yangu na kila siku naomba Mungu anisaidie niweze kujitegemea kimaisha, kujiingizia kipato kitakachonisaida kukimu mahitaji yangu ya kila siku na ya ndugu zangu bila kuwaza kumtegemea mtu.
BC: Umejipanga vipi kwenye suala la usambazaji na kuhakikisha kwamba unakidhi mahitaji (demand and supply)? Na tukiongelea upatikanaji wake,nywele za Kidoti zitakuwa zinapatikana wapi na wapi? Bei?
JM: Supply itategemea sana na demand. Producers wangu wako tayari so haina neno…. Nywele zinapatikana Kariakoo, Msasani, Mwenge, Sinza kwa kuanzia ila tutakuwa nchi nzima na nchi za jirani very soon inshallah! Bei zinaanzia elfu 9-12.
BC: Tofauti na makampuni au brand zingine kadhaa ninazozijua wewe umeanza na tayari unao mwelekeo wa jinsi ya kusaidia jamii.Hebu nieleleze kidogo kwa faida ya wasomaji wetu…Kasikana ni nini hasa na uhusiano wake na Kidoti Loving ukoje?
JM: Kwa lugha ya Kingoni, Kasikana inamaanisha “kasichana” ime-inspire Kidoti. Wengi wanafahamu ninapenda sana kujitoa katika mambo ya kijamii. Nina project yangu nataka niifanye kwa kuanzia mkoani Ruvuma kwa ajili ya wasichana. Sasa kama tunavyojua, ili liweze kufanikiwa lazima kuwe na hela. Sehemu za mapato ya Kidoti zitasaidia kulifanikisha hili. Kituo cha wasichana wanapoweza kubadili mazingira, kufanyia kazi talanta zao na kujenga kujiamini zaidi.
BC: Mpaka hapo ulipofikia bila shaka umekumbana na changamoto kadha wa kadha.Kwa maana hiyo upo katika mazingira mazuri ya kumpa mtu(mjasiriamali mtarajiwa) ushauri kuhusu biashara, kuthubutu nk. Angetokea mtu akakuomba umpe ushauri ungemwambia azingatie mambo gani?
JM: Awe na team yenye moto wa kuona kitu chenu kinasimama hata kama hakuna hela kwanza. Na hiyo timu iwe na watu wenye background na expertise , network na experience mbalimbali ili hata kama hela haipo bado ( which is normally the case) muweze kutumia networks na vipaji vyenu kwa kuanzia.
Kidoti haijaanza na hela nyingi, uzuri kupitia urembo na chuo nimekutana na watu wengi sana tukashirikiana vizuri na kuheshimiana kiasi wamekuwa mstari wa mbele kutoa msaada kwangu wa hali na mali. Team yangu ni ya wasomi waliomaliza chuo wenye kiu ya kusaka na kufanya kitu tofauti tulikutana chuo pia. So ni baraka tu. Usidharau mtu huwezi jua atakusaidiaje mbeleni.
BC: Bila shaka Kidoti Loving ina mipango mingi ya mbeleni.Nini mipango ya miaka kumi baadaye.Where do you want to see Kidoti Loving reaching?
JM: Nataka Kidoti isimame yenyewe bila jina Jokate. Kuanzia mwaka kesho nitakuwa na mashindano ya kusaka The New Face Of Kidoti ili brand iwe sustainable. Nitatambulisha rasmi nguo na vitu vingine mwaka kesho Q1.
Ila speaking long term nataka brand iwe kubwa zaidi yenye mvuto wa kipekee na kukubalika, madukani kote na kwenye mikoa mikubwa nk… Ila kwa mfano unaoonekana napenda sana nitengeneze kitu Kama Victoria’s secret, Zara…. Hiyo ndio mifano ninayoisoma kwenye biashara hii. Sasa mchanganyiko wa brand kubwa kama hizo lakini iwe na taste ya kiafrika ni hatari sana…
BC: Asante sana kwa muda wako Jokate na kwa niaba ya timu nzima ya BC,nakutakia kila la kheri
JM: Asante sana.
Special Thanks To; Jeff Msangi (www.bongocelebrity.com).
Posted by David Ndaiga at 9:57:00 AM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
Reactions:
Monday, October 22, 2012
CHAPA LAPA -- NURU Ft. VEDASTO (New Hit On Town).
Umeshamsikia Kwenye Nyimbo Nyingi Na Baadhi Ya Hizo Ni Pamoja Na Ile Aliyoitoa Kwa Ushirikiano Na Bob Junior Kutoka Sharobaro Records Iliyokuwa Ikiienda Kwa jina la '' Muhogo Andazi''.
Alikuja tena kivingine akikwambia ''Super Star'', wimbo ambao ulifanya vizuri pia kwenye masikio ya wengi.
Huyu hapa amerudi tena na safari hii anatuletea kitu kingine kutoka G-Records, akiwa amemshirikisha Vedasto na wimbo unaitwa '' CHAPA LAPA''.
Uangalie Hapa Chini;
Posted by David Ndaiga at 2:26:00 PM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
Reactions:
Friday, October 19, 2012
'' JUST SIMPLE '' WEDDING DRESS 2012/13
Posted by David Ndaiga at 9:14:00 AM No comments:
Umasikini
Mipaka na vipimo vya umaskini Nchini Tanzania vimejitokeza katika kipindi cha muda mrefu. Muda wa mabadiliko katika kufahamu mipaka yanatokana na tofauti zilizopo na muda na nafasi ya kueleza nini maana ya kuwa na hali njema.
Maelezo ya awali yalilenga kwenye mahitaji muhimu ya msingi kwa ajili ya kumwezesha mtu kuishi katika kipimo cha chini. Gharama za chini za mahitaji ya lishe ndiyo kitu muhimu cha kipimo kiwango cha umaskini. Maelezo hayo ya kipimo cha umaskini vilijumuisha vigezo vya jamii na uchumi vinavyohusika na viwango vya juu vya magonjwa na vifo, kushamiri kwa lishe duni, kutoweza kusoma wala kuandika, hali ya juu ya vifo vya watoto na akina mama, umri mdogo wa kuishi, mahali duni pa kuishi, nguo duni, mapato ya chini na matumizi finyu na miundombinu mibovu (mawasiliano, usafirishaji, huduma za jamii n.k). vipimo vingine pamoja na uzazi wa mara kwa mara, kukosekana kwa huduma za msingi kama vile maji safi, ukosefu wa chakula na kuwa na teknolojia duni. Kwa ujumla, vipimo hivyo vinaweza kutumika kumtambua mtu na nyumba maskini, jamii na jumuiya maskini. Nyumba wanayoishi watu au jamii inayokabiliwa na baadhi au vipimo vyote hivyo inaweza kusemwa kwamba ni maskini.
Masuala mengi yanayohusu vipimo vya umaskini vinaegemea zaidi kwenye hali ya uchumi. Hatimaye, vingi vya vigezo vyake vinaweza kupimwa. Hivi karibuni, maelezo ya umaskini yameweza kupamuliwa zaidi. Maelezo mapya yanajumuisha matatizo ya heshima binafsi, uwezekano wa kupatwa na hatari za ndani na nje, kutengwa kutoka mpango wa maendeleo na kukosekana kwa mtaji wa jamii. Nyongeza hizo mpya kwa maelezo ya umaskini zinagusa ubora wa hali njema ya jamii na uchumi.
Mkusanyiko wa ubora na wingi wa vigezo vya umaskini vinatumika kutambua nani ni maskini, ukubwa wa umaskini wao, wapi wanaikoshi na wanajishguhulisha na kazi gani ili waweze kuishi. Maelezo ya vigezo hivyo pia vinasaidia kutayarisha sera kwa ajili ya kusaidia maskini kukuza uchumi, kupanga matumizi kwa ajili ya watu, mipango ya usalama na kutayarisha vifaa kwa ajili ya kutathmini matokeo ya mipango na miradi juu ya kupunguza umaskini. Kwa kawaida umaskini ni matokeo ya vitu vingi na mara nyingi vitu ambavyo vinaingiliana ambavyo vinajumuisha ukosefu wa rasilimali ya kuzalisha utajiri, kutojua kusoma wala kuandika, magonjwa maafa kama vile mafuriko, ukame na maafa yanayoletwa na binadamu, kama vile vita.
Katika ngazi ya kimataifa, kukosekana kwa usawa katika kushirikiana kiuchumi na kisiasa kama inavyojionyesha katika masharti yasiyoridhisha ya biashara na shughuli nyingine yaliyopangwa kwa ajili ya nchi zinazoendelea pia ni moja ya sababu kubwa ya umaskini katika nchi zinazoendelea. Baadhi ya sababu za umaskini hazijionyeshi wazi wazi kama vile desturi na mila ambazo zinazuia matumizi ya rasilimali ipasavyo na kukosa kushirikishwa katika masuala ya kuongeza kipato.
Tathmini ya kiwango na mwelekeo wa umaskini unatibuliwa na kukosekana kwa taarifa za mara kwa mra, kutopatikana kwa vigezo vinavyojulikana rasmi vya umaskini.
Kutopatikana kwa vigezo vilivyo rasmi vya umaskini kumewafanya baadhi ya wachunguzi kuamua kutumia matokeo ya uchunguzi wao wenyewe. Hivyo, “vigezo vya chini” huonyesha mahitaji ya msingi ya chakula yasiyothibitishwa kwa mfano tabia za kula, mahitaji ya lishe na gharama, na “vigezo vya juu” vinahusu mahitaji ya chakula, pamoja na mahitaji mengine muhimu, kama nguo, nyumba, maji na afya. Zaidi ya hayo, kigezo kingine cha umaskini ni matumizi ya dola moja ya Marekani kwa siku kwa kulinganisha na nchi nyingine.
Umaskini mikoani na kukuza Hali njema
Umaskini na vigezo vya hali njema vinatumika hapa katika kupanga nafasi za mikoa 20 ya Tanzania. Uchambuzi huu ni wa awali, unahitajikaji kuchujwa zaidi, na hivyo utumike kwa hadhari. Kutokana na uchambuzi huu, Dodoma, Kagera, Lindi na Pwani ni mikoa inayoathirika zaidi na hali ya umaskini Mikoa ya Dar es Salaam, Ruvuma na Kilimanjaro inaathirika kidogo sana.
Umaskini unazidi kubaki kuwa zaidi ni suala la vijijini, ingawa idadi ya watu maskini katika maeneo ya miji hasa wasio na kazi na wale waliopo kwenye sekta isiyo rasmi, idadi yao ya umaskini inaongezeka kwa kasi katika eneo hili katika maeneo yote ya mjini na vijijini. Maskini wanakosa mtaji na rasilimali aliyonayo mtu mwenyewe kwa mfano elimu duni, hali mbaya ya afya na familia kubwa. Hali ya umaskini inahatarishwa zaidi kwa kuzidi kuongezeka kwa magonjwa hasa kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa wa UKIMWI.
Hatua zinazochukulwia kuondoa umaskini
Tangu kupatikana kwa uhuru 1961 Serikali ya Tanzania iliweka suala la kuondoa umaskini kuwa moja ya malengo yake makuu. Moja ya mikakati iliyobuniwa ni kuanzisha na kutekeleza sera za jamii na uchumi ambazo zinahusika na suala la umaskini katika ngazi za taifa na ya mtu binafsi. Utaratibu huu unamaanisha kwamba serikali iingilie kati kusaidia katika masuala ya elimu na maeneo mengine ya ustawi wa jamii, pamoja na kujenga mazingira mazuri ya kumwezesha mwekezaji binafsi kuingia katika sekta za uzalishaji.
Katika harakati za mipango ya kupunguza umaskini ambao umeenea kote, Tanzania ilitayarisha mwaka 1999 na kukubali kutumika kwa Dira ya Maendeleo 2025 na mpango wa Taifa wa kuondoa umaskini (NPES) hapo mwaka 1997, mipango inayofafanua dira kwa ajili ya jamii fukara na kustawisha hali ya jamii. Mpango wa Taifa wa kuondoa umaskini ambao ulianza kutumika 1997 ulilenga katika kutoa mwongozo kwa washika dau katika kuchambua, kutunga, kutekeleza na kutathmini umaskini wao. Lengo la mpango huu ilikuwa ni kutoa maelekezo ya kuongoza juhudi za kuangamiza umaskini kwa nia ya kuondoa kabisa umaskini ifikapo 2025. Ili kufanikisha malengo ya mpango wa Taifa wa kutokomeza umaskini serikali umezishirikisha sekta muhimu tano:
¨ Elimu
¨ Afya
¨ Maji
¨ Kilimo na
¨ Barabara za vijijini
Mpango umechagua maeneo matatu ya kushughulikiwa, nayo ni yafuatayo:- maeneo yanayotengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kutokomeza umaskini, maeneo yanayojenga uwezo wa kupambana na umaskini na maeneo yanayotokomeza umaskini. Mpango huo pia umetamka majukumu yatakayotekelezwa na ngazi mbalimbali katika juhudi za kuondoa umaskini. Dira ya 2025 iko sambamba na mpango wa maendeleo wa kimataifa ambao unatumia dira kusaidia kupata taarifa za kazi zinazofanyika katika kuangamiza umaskini.
Mwezi Juni, 1999 serikali ilitoa kijitabu cha vigezo vya kusimamia umaskini na hali njema ambacho kina nia ya kutoa msingi wa kusimamia utekelezaji na kutathmini msukumo wa mpango wa kutokomeza umaskini. Vigezo vilivyoko katika kijitabu hiki vitasaidia kutoa taaifa za uhakika za maendeleo kwa kufahamu hali ya umaskini na ustawi ili kuongoza shughuli za sera na mipango ya kupunguza umaskini. Mpango wa Taifa wa kuondoa umaskini (NPES) na kijitabu cha vigezo vya kusimamia umaskini na hali njema vilitayarishwa kwa kushirikiana na washika dau mbalimbali. Sambamba na NPES, serikali imechagua maeneo ya kupewa kipaumbele ya kutumia fedha za umma kwa utaratibu wa “The Medium Term Expenditure Framework” (MTEF) ambao utekelezaji wake unasimamiwa chini ya utaratibu wa mwaka wa Public Expenditure Review (PER) ambao pia unawahusisha washika dau. Utaratibu huu ndio uliokuwa unatumika kuongoza bajeti kwa miaka mitaktu sasa. Mfumo huu wa kuendesha bajeti utaingizwa katika mpango mzima wa maendeleo ambao unashirikisha msaada kutoka nje.
Mfumo unajumuisha malengo yote mawili ya kuendeleza uchumi na jamii kwa kuzingatia sekta zilizopewa kipaumbele mkazo ukielekezwa kwa maeneo yakfuatayo:
¨ Kuimarisha zaidi sera ya mazingira na masoko yanayokubalika. Kujenga mfumo imara ambao ndiyo ufunguo wa kipimo cha kustawi na njia ya kupunguza umaskini kwa kiwango kikubwa. Lakini, ufunguo wa kupunguza umaskini kwa kiwango kikubwa katika Tanzania ni kuongeza kasi ya kustawi. Makadirio ya kuonyesha kupungua kwa umaskini yanaoenda sambamba na ustawishaji na kuonyesha kuwa ongezeko la kustawi kunaweza kupunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya mstari wa umaskini ambao kwa sasa ni asilimia 50 hadi kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2015.
¨ Kufanikiwa kwa lengo la kuongeza ustawishaji kutahitaji juhudi nzito za kuzidisha uzalishaji na kuongeza uwekezaji katika mtaji wa watu na mali.
¨ Kuongeza uwekezaji kwa kutumia nguvu na uwezo wa binadamu kunahitaji kuchukuliwa hatua za kuwaongezea wahusika motisha na kuongeza faida kwa shughuli hizo za uwekezaji na kuongeza msaada wa umma katika maeneo yaliyo nje ya mfumo kwa mfano msaada wa elimu ya msingi na afya.
¨ Marekebisho ya mfumo.
¨ Shughuli za kudhibiti ukimwi zinatakiwa kuwekwa ndani ya sera ya maendeleo na ihusishe sekta zote.
¨ Mpango wa muda mrefu unaoambatana na ukuaji wa kilimo nchini Tanzania unahitaji angalao hali ya uchumi uliotulia, utafiti unaofaa na upanuzi, miundombinu iliyoimarishwa na kuendeleza mfumo uliofungamana, uimarishaji wa asasi zinazosaidia mabadiliko ya kilimo na maendeleo ya vijiji kwa mapana zaidi.
Mipango ya kuondoa umaskini
Mpango huu unaangaliwa kama ni chombo cha kupitisha juhudi za taifa kuelekea mwenye madhumuni tuliyokubaliana pamoja na nyenzo zilizo dhahiri na matokeo kimsingi. Ufafanuzi na utekelezaji wa mpango ni utaratibu unaoendelea. Wakati maamuzi yanayohusu masuala mengi yalikwishaanzishwa, matayarisho ya mipango ya baadhi ya sekta kama vile kilimo na elimu bado hayajakamilika. Zaidi ya hayo, uamuzi wa utekelezaji wa mabadiliko yanayolenga kuhamasisha jukumu la kutunga kutekeleza na kusimamia upunguzaji wa umaskini kusimamiwa na wilaya, manispaa na jumuia katika ngazi za chini umeanza, lakini zoezi hilo litachukua muda kukamilika. Kwa hiyo mpango mzima wa kupunguza umaskini itabidi ushughulikiwe taratibu ili kuruhusu kujumuisha mipango na shughuli nyingine zitakazojitokeza kutokana na kazi zinazoendelea. Mpango wa kupunguza umaskini kwa kiwango kikubwa, ni sehemu ya mabadiliko makubwa ya uchumi na mfumo unaosaidiwa chini ya mpango wa “Poverty Reduction Growth Facility” unaogharamiwa na Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) na mpango wa Poverty Structural Adjustment Credit unaogharamiwa na Benki ya Dunia IWB).
Wakati huo huo katika kuizumgumzia hoja hiyo ngumu ya umaskini Benki ya Dunia na shirika la Kimataifa la Fedha hapo mwaka 1999 walianzisha juhudi za mpango wa “Enhanced Highly Indebted Poor Countries”, (HIPC). Madhumuni ya kuanzisha mpango huu ni kutoa msamaha wa kodi kwa nchi zinazokabiliana na mzigo mkubwa wa kulipa madeni. Msamaha utakaopatikana kutokana na unafuu wa madeni utaiwezesha Tanzania kutumia rasilimali zake kuimarisha maendeleo na kupunguza umaskini na kuimarisha upatikanaji wa huduma za elimu na afya. Jumuiya ya wahisani kwa kupitia HIPC imetoa unafuu ambao umeiongezea Tanzania uwezo wa kupigana na umaskini na kutekeleza Sera zake za maendeleo. Silaha kuu zinazotumika katika kufanikisha mpango huu ni kutekeleza yaliyomo katika Poverty Reducation and Growth Facility ya IMF na Programmatic Structural Adjustment Credit ya WB na PRSP.
PRSP ni sehemu ya mpango wa HIPC na unaolenga uhusiano katika kupunguza umaskini. PRSP inazingatia shughuli zinazohusu umaskini ambazo hazihitaji msaada wa fedha lakini ni muhimu katika upunguzaji wa umaskini.
Kazi za PRSP imehusisha mazungumzo ya ushauriano baina ya washika dau kitu ambacho kimechangia kuweka msingi madhubuti wa kutekeleza madhumuni ya Sera za maendeleo ya nchi pamoja na mapngo wa wa kupunguza umaskini. Juhudi madhubuti kuelekea kwenye upunguzaji wa umaskini zinazohuchukuliwa na washirika wa kimataif bado zinatekelezwa nje ya mfumo wa bajeti ya Serikali kuu. Ili kuhakikisha kwamba maendeleo ya kiwango cha juu kinapatikana katika upunguzaji wa umaskini na fedha iliyoombwa kwa shughuli hiyo inapatikana, jitihada zitazidishwa na mipango kutekelezwa kulingana na umuhimu wake.
PSRC, wakati inaweka mipango dhidi ya umaskini pia itashughulikia marekebisho ya mifumo, kuweka uchumi imara na kuendeleza kustawisha uchumi kufuatana na mpango wa dira ya Taifa wa maendeleo wa 2025
Aidha kufuatana na mpango wa muda mrefu wa kuondoa umaskini Serikali imeanzisha (kuanzia Julai 1998) Multilateral Debt Fund ambamo Nchi hisani zimekubali kuchangia jumla ya US$ 145.56 millioni. Hadi kufikia Desemba 1999, US$ 109.5 milioni zilikwisha changwa kati ya fedha zilizoahidiwa kwa ajili ya kulipia mipango inayohusika na aya na elimu. Wapo watendaji wengi wanao jushughulisha na usimamizi wa mipango ya PRSP ambao huhusika na ukusanyaji wa taarifa, uchanguzi na matumizi ya taarifa.
Jukumu kuu la kusimamia suala la umaskini kitaifa liko chini ya ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ni chambo cha Serikali kilichopewa jukumu la kuratibu masula ya kuondoa umaskini kwa kuhakikisha kwamba washika dau wote wanaohusika wanashirikishwa katika masuala ya ufuatiliaji.
aba za watu wasioweza kufanikiwa kimaisha
Watu wasioweza kufanikiwa hujaa fikra za kutofanikiwa na mara nyingi hulalamikia sana matatizo yao. Wakati mwingine wasioweza kufanikiwa hugeuza mambo mema na kuyafanya yaonekane mabaya, jua likiwaka watalalamika joto, likipoa watalaumu baridi, watalaumu foleni za barabarani, yaani kwao kila jambo wataligeuza na kulipa sababu mbaya. Hata wanaposhindwa kutekeleza jambo hutoa sababu, yote ni kuzilinda fikara zao za kutofanikiwa.
Tabia hii hukua mpaka kufikia hatua wanapowatazama wenzao hudhani kuwa wanawasengenya, kuwafanyia mambo mabaya, kuwasaliti, ilimradi tu ni kuwa kinyume na mambo mema. Watu wa namna hii hata kama watasaidiwa namna gani hugeuza misaada hiyo kuwa ya kujipendekeza na mara nyingi hupuuza wema haraka na kueneza mabaya ya mtu. Lakini pamoja na yote kutokana na fikra zao kuwa za kushindwa watu wa tabia hii hukata tamaa mapema, pale wanapofanya jambo na kuonekana lina ugumu kidogo.
Hutenda kabla ya kufikiri
Tabia ya pili ya watu wasioweza kufanikiwa kimaisha ni hii ya kutenda jambo kabla ya kufikiria. Watu wa aina hii, kuwa wepesi sana kununua vitu barabarani mara tu wanaposhawashiwa na macho au wauzaji. Utakuta mtu bila hata kujiuliza faida za kitu hicho anaamua haraka kukipata. Ataamua kwa haraka kuoa, kuolewa, kukubali kujiingiza katika mapenzi na hata kufanya jambo lo lote bila kujiuliza atanufaika vipi?
Hupenda kuzungumza zaidi ya kusikiliza
Watu ambao wako katika hatari ya kutofanikiwa ni wale ambao daima ni wazuri katika kuzungumza kuliko kusikiliza. Wao huwa ni wajuajia wa kila kitu, hawako tayari kupokea ushauri. Siku zote wanapokuwa kwenye makundi ya watu pengine wajuzi zaidi yao wao huwa hodari kujenga hoja kutetea mambo yao hata kama hayafai. Unaweza kumkuta mtu ni kiongozi wa ngazi za juu, amefanya kosa na watu wote wameona kuwa kakosea lakini mhusika hujiona si mikosaji.
Mtu anapokuwa muongeaji sana huwa mgumu kupokea ushauri wa ye yote, anachoamua yeye hukifanya kwa imani kuwa kinafaa. Ukiwa mtu mwenya tabia ya aina hii huwezi kufanikiwa kabisa katika maisha yako. Watafiti wa masuala ya biashara ulimwengini waliwahi kushauri kuwa mipango mizuri ya kibiashara hutoka kwa watu masikini, ambao walisema hufikiri zaidi namna ya kujikomboa kuliko matajiri wanavyofikiri katika kujiendeleza, hivyo wakasema kama mtu anataka kufanikiwa kibiashara lazima asikilize mawazo ya masikini si kuwapuuza kwa kujiona ni bora zaidi yao.
Hukata tamaa mapema
Watu wanaotaka kufanikiwa huchukulia ushindwa kama hatua ya kuelekea kwenye mafanikio, lakini watu wasioweza kufanikiwa wanapojaribu mara moja au mbili kuvuka kikwazo fulani cha kimaisha na kushindwa hukata tamaa na kutotaka kujaribu tena kusonga mbele. Wanye tabia ya kushindwa kimaisha hawako tayari kudumu na jambo moja linaloonekana kushindikana kwao kwa muda mrefu. Akiona mwanamke ambaye ni mkorofi kidogo, haraka hukimbilia kumwacha na kutafuta mwingine, mara nyingi si watu wavumilivu.
Akijaribu biashara ya vitumbua kwa wiki moja na akaona havinunuliwi, anaaza kupika maadazi, wiki moja baadaye yuko kwenye mihogo, basi ilimradi ni kuhangaika kusikokuwa na tija katika maisha. Ukitaka kuwa mmoja kati ya watu wasiweza kufanikiwa kimaisha, basi jaribu kuishi maisha ya kukata tamaa mapema unapofanya mambo.
Hujaribu kuwarudisha nyuma wengine
Wasioweza kufanikiwa katika maisha huwa na tabia moja ya ajabu ambayo ilianzishwa na Hawa mwanamke anayetajwa katika Kitabu cha Biblia kuwa ni mtu wa kwanza kufanya dhambi. Mwanamke huyu alipodanganywa na nyoka na kuchuma tunda hakutosheka na dhambi zake, bali alimpelekea na mumewe Adamu naye akala. Mara nyingi watu walioshindwa kimaisha kuwa na tabia za kuwashawishi watu wengine wawe kama wao katika mawazo na matendo.
Tabia za watu wa aina hii huwa si za kimaendelezo kwa vile wao hudhani kuwa njia zao ni sahihi na hivyo hujaribu kwa nguvu zao kuwarudisha wengine nyuma ili wawe kama wao. Ni watu wenye wivu wa ‘kijinga’ wakiona mwingine anaendelea katika hiki na kile humpiga vita ili afilisike. Ni wingi wa fitina, uchonganishi. Wenye tabia za kutofanikiwa hudhani kuwa kukwama kwao hutokana na vikwazo vinavyoletwa na wengine. “Kwa sababu jamaa kanikwamisha hiki na kile, nimkwama kwa sababu ya kaka yangu”
Hupoteza muda mwingi
Watu ambao hawawezi kufanikiwa ni wale ambao hupoteza muda mwingi kufanya mambo yasiyokuwa na tija, kwa kuangalia Tv, kusengenya watu, kunywa pombe, kufanya starehe na kutumia muda hovyo kwenye kazi ambazo hazina msaada kwao. Wapo watu mahodari kutembelea kwenye nyumba za wengine na kuongea huko kutwa nzima bila kujali kama muda waliopoteza wangeweza kufanya kazi na kujipatia kipato.
Huchagua mambo rahisi
Wakati mwingine mafanikio huhitaji kufanya kazi ngumu zenye kuchosha, lakini watu wasiokuwa na uwezo wa kufanikiwa wanapoletewa mambo mawilii huwa wepesi zaidi kuchagua jepesi kulifanya. Kama ni kazi, basi zisiwe ngumu sana ziwe nyepesi nyepesi ambazo watazifanya bila jasho. Watu wasiokuwa kwenye njia ya mafanikio hawapendi kujituma, wepesi kuchoka na mara nyingi hupenda sana kufanya kazi kidogo na kulala sana.
Tabia za watu wasioweza kufanikiwa huwa ni za kukwepa kuwajibika. Hata kama kuna mtu anataka kumpatia kitu na akamwambia awahi kesho yake asubuhi, huchelewa kwa vile hawezi kujihimu asubuhi na kuacha raha ya usingizi, wakati mwingine hata akiambiwa asubiri mpaka muda fulani huwa hayuko tayari kusubiri.
UFANYEJE KATIKA HALI NGUMU YA UCHUMI?
Matatizo ya ugumu wa uchumi katika dunia hii siyo mapya. Tangu baada ya mwanadamu kuanguka katika dhambi – amekuwa mara kwa mara akisumbuliwa na matatizo ya uchumi. Ukisoma habari za Isaka na za Yakobo utaona jinsi hali hii ilivyojitokeza.
Lakini biblia inaeleza wazi kuwa siku hizi ni mwisho. Katika siku hizi za mwisho, biblia pia inasema wazi kabisa kuwa dunia itapita kwenye vipindi vigumu vya uchumi
Kwa Mfano: Katika Mathayo 24:7 na Ufunuo wa Yohana 6:3-6 tunaona ya kuwa katika siku hizi za mwisho kutatokea njaa – au upungufu wa chakula. Sababu ya kuja kwa njaa hiyo ni vita vitakavyokuwa vinatokea katika nchi mbalimbali. Ni wazi kabisa kuwa palipo na vita au palipo na ugomvi, panakuwa na matatizo ya ulimaji mashamba na usafiri wa kuleta chakula toka sehemu zingine. Matokeo ni hilo eneo au nchi kukosa chakula, haya mambo yaliyotabiriwa kutokea siku hizi za mwisho wa dunia.
Ukisoma katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana sura za 17 na 18 utaona ya kuwa hali ngumu ya kibiashara imetabiriwa kutokea katika siku hizi za mwisho. Kuuza au kununua kutafanyika kwa vibali. Watu watapenda fedha sana kuliko kumpenda Mungu. Kutakuwa na uhusiano mkubwa sana kati ya utajiri na biashara na uasherati. Wafanya biashara wa siku hizi za mwisho watakuwa na sehemu kubwa katika utawala wa miji au vijiji wanavyokaa – hata wakati mwingine katika maongozi ya nchi au mataifa mbalimbali.
Matokeo ya hali namna hii inawafanya watu watafute njia au mbinu za kuweza kuishi katika vipindi vya namna hiyo. Lakini ni wazi kuwa si mbinu zote au njia zote ambazo wanadamu wanazitumia katika kuishi wakati wa hali ngumu ya uchumi zinampendeza Mungu.
Kunapotokea hali ngumu ya uchumi, tabia za watu zinabadilika. Mara kwa mara mambo yafuatayo hutokea;
Kubana matumizi Kununua vitu kwa wingi na kuvirundika Uchoyo – kupunguza tabia ya utoaji na ukarimu Watu huacha kumtumikia Mungu na badala yake mtu huitumikia mali Rushwa, wizi na dhuluma huwa ni vitu vya kawaida Miradi ya kila namna huibuka kuanzia kwa watoto hadi watu wazima.
Jambo linalowafanya watu wawe na tabia hizi, ni lile la kutaka kutafuta namna ya kuishi katika kipindi kigumu cha uchumi. Je!mkristo afanye nini ili aishi katika kipindi hiki kigumu cha uchumi bila kufanya mambo yatakayomkosea Mungu?
Wakristo wengine wamefika mahali pa kuhalalisha miradi ya kuwapatia fedha ambayo ni kinyume na ushuhuda wa kikristo – Je! hii ni sawa?
Wengine wamefika hata mahali pa kufunga nira na wasioamini (wasio wakristo) KWA JINSI ISIYO SAWASAWA (yaani isiyokubalika) na neno la Mungu ili waweze kupata fedha kutokana na mradi wanaofanya pamoja. IKO "jinsi iliyo sawasawa" na utaifahamu ikiwa utakuwa mtendaji wa neno la Mungu.
Wakristo si wa ulimwengu huu
Ndugu au Dada unayesoma sasa mambo haya – sikiliza! Sisi kama wakristo si wa ulimwengu huu ingawa tunaishi hapa ulimwenguni. Fahamu na kumbuka hili kila wakati. Yesu Kristo alisema hivi;
"Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni" (Yohana 17:14-18).
Je! unafikiri Yesu Kristo anaweza kututuma hapa duniani bila kutuandaa kuishi kiushindi katika majaribu yaliyomo ndani yake na hali ngumu ya uchumi?
Je! unadhani Yesu Kristo anaweza kukuokoa halafu asikutunze kiuchumi katika maisha mapya ya wokovu? Nafahamu kuna wakristo wengi walioanguka kiroho kwa sababu ya kutafuta njia za kujisaidia kimaisha.
Biblia inatuambia ya kuwa Yesu Kristo huwalisha na kuwatunza watu wake ili ajiletee kanisa (wakristo) walio watakatifu. Soma Waefeso 5:25-33.
Katika vipindi vyote vya matatizo ya uchumi, Mungu ameweza kuwalisha na kuwatunza watu wake. Wamekula na kuvaa na kulala ndani ya mpango wake bila kumkosea.
Katika siku hizi za mwisho, Kristo anazungumza na kulikumbusha kanisa (wakristo) juu ya njia au mbinu za kuchukua wakati wa hali ngumu ya uchumi mahali walipo.
Mashauri muhimu ya kufanya
Fuata maongozi ya Mungu na siyo ya dunia: Ni rahisi sana kusikia na kufuata ushauri wa wanadamu kuliko ushauri wa Mungu hasa mtu anapobanwa na shida. Lakini kwa mkristo nakushauri siku zote kuwe na shida au kusiwe na shida, fuata ushauri wa Mungu kama vile anavyokuongoza kwa Roho Mtakatifu katika neno lake. Tuangalie jinsi Isaka alivyofanya alipokumbwa na hali ya njaa.
"Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari. Bwana akamtokea, akasema, usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia …. Nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki …" (Mwanzo 25:1-3).
Njaa ilipotokea huko Gerari, watu walianza kuondoka huko na kwenda Misri, ili kutafuta chakula. Ni wazi ya kuwa hata Isaka alitaka kufanya hivyo. Bwana akamzuia akamwambia asiondoke bali akae katika nchi aliyomwambia na katika nchi hiyo atakuwa pamoja naye na kumbariki au kumfanikisha.
Nataka kukukumbusha ya kuwa baraka za Mungu kwetu hazitegemei jinsi hali ya hewa na uchumi wa dunia hii unavyokwenda bali zinategemea NENO LA KRISTO.
Isaka akatii, hakuondoka bali alibaki katika nchi hiyo ambayo watu walikuwa hawapati chakula wakilima.
"Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, Bwana akambariki" (Mwanzo 26:12).
Siku zote kaa na kufanya kazi mahali ambapo Mungu amekuongoza kukaa. Usihame mahali au kuacha kazi, bila uongozi wa Mungu. Kufanikiwa kwako hakutegemei mipango yako bali kunategemea mpango wa Mungu.
Ukiwa ndani ya Kristo utafanikiwa mahali po pote pale ambapo Mungu atakapokuweka hata kama mazingira yake kibinadamu si mazuri kwa kufanikiwa. Ukiwa ndani ya Kristo, "Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani … utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa utokapo …. Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako" (Kumbukumbu ya Torati 28:3,6,8).
Endelea kutoa hata wakati wa upungufu
Katika hali ya kibinadamu upungufu unapotokea mahali watu wanabana matumizi – na hali ya ukarimu na utoaji huwa inafifia sana hata wakati mwingine kupokea kabisa. Wakristo wengi pia wamekumbwa na hali hii – wanasema wamepunguza utoaji kwa kuwa wamepungukiwa na hali ya uchumi ni ngumu. Je! hii ni sawa?
Wakati wa ukame ulipotokea wakati wa maisha ya Nabii Eliya Mtishbi; Bwana alimwambia Eliya, "Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe" (1Wafalme 17:9).
Unakumbuka jinsi yule mama alivyojitetea wakati Eliya alipofika kwake ili alishwe? Yule mama alijitetea kama watu wengine wanavyojitetea siku hizi wakitakiwa kutoa au kuchanga walivyo navyo kwa ajili ya kazi ya Mungu. Naye yule Mjane akasema;
"Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tule tukafe" (1Wafalme 17:12).
Kwa jinsi ya kibinadamu, Eliya angeweza kumwonea huruma yule mama, asile chakula chake; na aondoke na aende kwa matajiri wa siku zile kupata chakula. Lakini Eliya hakufanya hivyo- bali ALITII MAAGIZO YA MUNGU. Eliya akamwambia yule mjane hivi;
"Usiogope;enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie KWANZA mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao" (1Wafalme 17:13).
Ndivyo yule mama alivyofanya – alimpa KWANZA MUNGU kwa kupitia mtumishi wake. Mungu akambariki yule mama kwa ukarimu na utoaji wake wakati alipokuwa na upungufu. "Lile pipa la unga HALIKUPUNGUKA, wala ile chupa ya mafuta HAIKUISHA sawasawa na NENO LA BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya" (1Wafalme 17:16).
Katika hali ya upungufu ulionao, usiwe mchoyo bali endelea kumtolea Mungu, naye atakubariki na kukufanikisha. Na hii itaonyesha ni kwa kiasi gani unamtegemea Mungu wako na Neno lake.
Lazima ufahamu ya kuwa Yesu Kristo anaangalia sana jinsi tutoavyo. Siku moja akiangalia jinsi watu watoavyo fedha; "Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la Hazina; maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia" (Marko 12:43-44). Soma na kuyatafakari tena maneno hayo ya Yesu Kristo, halafu jiangalie jinsi utoavyo. Huyu mjane hakuwa na mali ya kutosha alikuwa maskini, lakini bado aliendelea kumtolea Mungu! Je wewe una la kujitetea katika kutomtolea Mungu wakati wa upungufu wako?
Weka hazina yako mbinguni
Yesu Kristo alisema;"Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo,na wezi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wezi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako" (Mathayo 6:19 – 21).
Utoaji wako utaonyesha kama moyo wako uko kwa Yesu au unaitegemea dunia. Moyo wako ukimtegemea sana Yesu, utatoa zaidi kwa ajili ya kazi ya Mungu kuliko mahali pengine. Mkristo anapopoa kiroho, utoaji wake HASA kwa kazi ya kuhubiri injili nao unapungua. Hata hivyo Biblia inatuambia katika siku za mwisho upendo wa wengi utapoa.
Mtolee Mungu zaka na dhabihu (matoleo) bila kuchoka, nawe utakuwa umeweka hazina yako mbinguni – mikononi mwa Mungu – ambamo wezi hawawezi kukuibia. Naye Bwana atakurudishia mara nyingi zaidi. Mradi mzuri na wenye uhakika wa mavuno kwa Mungu na kwako wakati wa hali ngumu ya uchumi ni mradi wa kuhubiri injili. Kwa hiyo siku zote hakikisha umeweka kiasi fulani katika mradi wa kuhubiri injili.
Dumu katika maombi
Hili ni muhimu sana. Kwa kuwa wakristo wengi wakiwa katika hali ya ugumu wa maisha na uchumi, wanapoa katika maombi – na wanakumbwa na majaribu ambayo mara nyingi yanachafua ushuhuda wao. Soma Luka 21:36, Mathayo 24:42 – 51 na Mathayo 26:41. Kwa hiyo dumu katika maombi, usikate tamaa, hata wakati wa hali ngumu kiuchumi kwa upande wako – bado zidi kudumu katika maombi.
SIRI YA UTAJIRI
Kwa nini watu wengine ni matajiri ?
Watu wengi wanajiuliza, "Siri ya utajiri ni nini?" Jee ni mbinu gani zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwa ya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa na ziada na faida. Kwa bahati mbaya sana, elimu hii haifundishwi darasani ila wanayo wafanyabiashara wachache na kila anayefanikiwa kujifunza siri hii huwa tajiri na huendelea kuificha. Kwa bahati nzuri, katika utafiti wagu nimeweza kuigundua siri ya utajiri. Kwa kuwa ninapenda wasomaji wangu waweze kufanikiwa na wapate manufaa kwa kununua kitabu hiki nimeamua kuiweka siri hii wazi:-
- Siri ya kwanza ya kuelekea ukwasi ni kubuni mradi unaojipa, yaani unaoweza kuitoa ziada na faida.
- Siri ya pili ya kuelekea kwenye utajiri ni kujifunza na kujenga tabia ya kuweka akiba
- Siri ya tatu ni kuwekeza fedha hizo za akiba katika vitega uchumi ambavyo vinazalisha faida endelevu.
- Siri ya nne ni kujifunza namna ya kufanya biashara na kuanzisha biashara yako ili iwe indelevu.
Kuna njia mbili za namna ya kupata utajiri zenye uhakika. Njia ya kwanza ni njia ndefu ambapo wataalamu na watafiti wa masuala ya fedha wameigundua njia hii ni rahisi kuifuata kwa sababu haihitaji uwe na kipato kikubwa, wanashauri kwamba ujenge tabia ya kuweka akiba, anza kuweka akiba ya T.shs 1,000 kila siku sawasawa na TShs 30,000 kwa mwezi, matokeo yake ni kwamba kama utaweka akiba yako kwa kipindi cha miaka 65 bila riba yoyote utakuwa na akiba TSshs 23,725,000 (Milioni Ishirini na Tatu Mia Saba Ishirini na Tano Elfu). Kama utawekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa kila mwaka itazaa na kukuletea TShs 2,750,000,000 (Bilioni Mbili na Milioni Mia Saba Hamsini). Hesabu hii inaweza ikakutisha na usiamini macho yako lakini hiyo ni siri ya nguvu ya hesabu na riba kama alivyozielezea mwanafizikia Enstein kwamba katika dunia hii hakuna kitu chenye nguvu kama hesabu za riba. Pengine njia hii inaweza kuwa ni ndefu sana na ya kukatisha tamaa. Wengi wetu hatuwezi kusubiri muda mrefu. Hivyo tungependa kuwa na mafanikio ya kiuchumi kwa haraka. Lakini nasisitiza kama kipato chako ni kidogo anza leo kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku.
Dundulizo la akiba hii hukutiririshia utajiri bila wewe kukusudia kwani utaweza kukidhi hitajiko la ghafla kama kuugua safari ya dharura gharama za likizo na hata kutumia mbinu hii kama mpango wa elimu kwa watoto wako iwapo utawaanzishia hivi mara tu kila mmojawapo anapozaliwa au unaweza kuutumia kama upanga wa siku zijazo kwa mirathi ukianza hivyo leo kwa kupangilia namna hiyo kwa kila kusudio lako la baadaye.
Hebu tuangalie njia ya pili.
- Njia ya pili ya mkato ni kuongeza kiwango cha kuweka akiba kama wewe ni mtu mwenye shughuli za kuzalisha ziada. Kipato chako kinaweza kuwa kinaongezeka kila mara. Badala ya kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku jiwekee malengo ya kuweka akiba ya TShs 10,000. Anza kwa kutenga asilimia 10% ya mapato yako hadi utakapofikia lengo la TShs 10,000 au zaidi kwa siku. Badala ya lengo lako kutimia kwa miaka sitini na tano (65) litatimia haraka zaidi. Kwa mfano ukiweka akiba ya TShs 10,000 kwa siku kwa muda wa miaka sita na miezi sita bila riba yoyote utapata TShs. 23,725,000. Ukiwekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa miaka sita na miezi sita utapata TShs. 33,917,505.78. Kama fedha hiyo utaendelea kuweka akiba kwa riba hiyohiyo hadi kufikia muda wa miaka kumi utapata TShs. 63,112,201.43.
Kwa kuwa kitu cha muhimu hapa ni kuweka akiba na kuwekeza akiba hiyo katika kitegauchumi chenye kutoa faida kubwa, utajiuliza jee uwekeze kwenye kitega uchumi chenye kutoa faida kiasi gani? Wataalamu wa mambo ya fedha wanashauri kuwa uwekeze fedha yako kwenye kitegauchumi chenye kutoa faida ya angalau asilimia 10% Kwa mfano unaweza kuwekeza kwenye Akaunti ya TAJIRIKA ya Standard Chatered Bank" inatoa riba ya asilimia kumi 10% pia unaweza kuwekeza kwa kununua hisa katika soko la hisa na mitaji.
Kwa wastani wa watafiti wa masuala ya fedha viwango vya mapato yatokanayo na hisa kwa gawio pamoja na kukua kwa mtaji ni zaidi ya asilimia 11% ambayo ni makubwa kwa kiwango cha kawaida cha asilimia kumi (10%).
Baada ya kueleza siri ya namna ya kupata utajiri nitazitaja njia zingine ambazo zinaweza kukuwezesha kuwa tajiri.
1. Unaweza kurithi mali na fedha kutoka kwa wazazi wako. Hii ni njia ya kubahatisha kwani watu matajiri siyo wengi na hivyo watoto wenye bahati kama hii ni wachache pia.
2. Unaweza kusomea ujuzi au utaalamu katika fani yenye malipo mazuri na kujiajiri mwenyewe. Kwa mfano, unaweza kusomea fani kama ya Uanasheria, Uhasibu na Udaktari au ufundi / sanaa na kadhalika.
3. Unaweza kuanzisha biashara yako na kuiendesha ili kupata ziada kubwa.
4. Unaweza kuendeleza vipaji vyako na kuwa mwanamichezo au msanii wa kulipwa.
5. Unaweza kutunga vitabu juu ya suala lolote unalolijua. Kwa mfano, kama wewe ni mtu uliyebobea katika masuala ya muziki unaweza kutunga kitabu kinachofundisha watu namna ya kuwa mwanamuziki. Watunzi wengi wa vitabu ni matajiri wakubwa. Hii ni kazi unayoweza kuifanya mara moja lakini ukavuna matunda yake kwa muda mrefu sana.
6. Unaweza kuwa mbunifu na kuanza kuuza mawazo yako au kutumia chombo ulichokibuni kukuingizia fedha.
7. Unaweza kucheza bahati nasibu na kushinda. Tatizo hapa soko na wateja wa aina hii ya huduma ni haba. Hiki ni kitu cha kubahatisha na nimekitaja makusudi ili kuwapa onyo wasomaji kwani watu wengi wanapenda sana kucheza michezo ya kubahatisha.
Uwezekano wa kutajirika kwa njia hii ni mdogo sana. Hivyo, nawashauri wasomaji kuachana na njia hii ya kutafuta utajiri. Nawashauri wachague njia yoyote inayofaa na inawezekana kwa kufuatana na mazingira yanayomzunguka mtu husika. Mkulima au mfugaji anaweza kuzingatia fani hii na kutajirika sana. Kwa kweli hakuna mipaka, hasa hapa kwetu Tanzania kwa sababu ya wingi wa fursa za kuweza kujishughulisha na kuwa tajiri.
Maelezo ya kina juu ya aina ya biashara au mbinu unaweza kuzitumia kutafuta na kupata faida utayapata katika sehemu ya pili ya kitabu hiki.
Inawezekana kuwa tofauti kati ya mtu tajiri na mtu maskini inatokana na kile tulichojifunza kutoka kwa wazazi wetu. Wazazi maskini huwaambia watoto wao wajitahidi kusoma sana ili wapate maksi nzuri darasani na ili baadaye waweze kupata kazi nzuri. Wakati wazazi matajiri huwapa watoto wao elimu ya namna ya kutafuta fedha. Kwa kawaida tukiwa shuleni tunapewa ripoti ya masomo. Katika maisha tunatakiwa kuwa na ripoti yetu ya maisha nayo ni orodha ya mali tulizonazo ikiwa ni pamoja na elimu ya kuzaliwa na ya kusomea na fedha taslimu zile zilizo katika hifadhi mbalimbali.
Kwa kufuata tafsiri ya Umoja wa mataifa mtu masikini ni yule ambaye kipato chake hakizidi TShs 1,000 kwa siku.
Inawezekana kuwa mfumo wa kifedha wa mtu maskini ni mfumo ambao humfanya kutumia kipato chake chote kulipia matumizi huwa hana ziada wala uwezo wa kuweka akiba hana madeni na hana mali.
Mfumo wa fedha wa mtu mwenye kipato cha kati ni mfumo ambao humfanya kuwa na mali kama magari, nyumba na kadhalika. Mara nyingi mali hizo huwa zinapatikana kwa mikopo na hutumia mshahara kulipia matumizi na madeni, hasa kama madeni ni makubwa, mtu mwenye kipato cha kati anapaswa kumuona mshauri wa maswala ya biashara. Hatua anazoweza kuchukua ili kujikwamua na tatizo la madeni anaweza kulazimika kuuza baadhi ya mali zake ambazo amezinunua kwa kutaka kuonyesha ufahari tu na ambazo hazina umuhimu. Kwa mfano kama mtu ana magari matatu ya kutembelea, anaweza kuuza magari mawili kubaki na gari limoja na fedha atakayoiokoa kuiwekeza au kutumia kama mataji na kuanzisha biashara ili kujiongezea kipato.
Mfumo wa mtu tajiri ni mfumo ambao unamwezesha kuwa na biashara yake, kumiliki mali nyingi, kuwa na fedha nyingi katika akiba na awe ameziwekeza kwenye vitega uchumi vinavyolipa faida kubwa zaidi ya asiliamia kumi, kama vile nyumba za kupangisha na hisa. Mtu huyu hana wasiwasi na maisha. Anaweza kusafiri au kuugua lakini vitegauchumi vyake vinaendelea kumwingizia fedha. Siri kubwa ya matajiri ni uwezo wa kutumia fedha na kuziwekeza kupata faida kubwa.
Hiki ni kitabu cha vitendo. Yote unayoyasoma humu inabidi uyafanyie kazi ili yakusaidie. Tofauti kati ya maskini na tajiri iko katika kuchukua hatua. Tajiri hujifunza mambo ya kumwendeleza na kuchukua hatua kwa kutekeleza kwa vitendo yale anayojifunza na anayoyaona yanaweza kumuinua kiuchumi. Maskini huwa anajifunza mambo na kuyaacha kichwani bila kuchukua hatua au kuyafanyia kazi aliyojifunza na hivyo fursa ya kupata utajiri inampita hivihivi.
NAMNA YA KUANZISHA BIASHARA.
Ukitaka kufanya biashara yoyote ile unatakiwa kufanya utafiti. Kutokufanya utafiti ni chanzo cha biashara nyingi kuharibika. Lazima ujiulize kwamba unataka kufanya biashara gani? Usiseme unataka kufanya biashara yoyote ile kwani kusema kwamba unataka kufanya biashara yoyote ile ni kupoteza mwelekeo kwa kuwa utakuwa hujui unataka kufanya nini. Kama hujui cha kufanya hakuna kitu utakachokifanya. Hili ni tatizo la watu wengi. Hata baadhi ya watu niliokutana nao wakitaka ushauri wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili. Njia ya kukusaidia kuamua ufanye biashara gani ni kwa kujiuliza umewahi kufanya kazi au biashara gani? Umesomea nini? Vipaji vyako ni vipi? Ni biashara ipi au kazi ipi unapenda zaidi kuliko nyingine na kwa sababu gani? Ukisha jiuliza maswali haya chukua kalamu na karatasi uandike maswali yako na kuyajibu. Ukikagua maswali na majibu yako utagundua shughuli unayoipenda, unayoiweza na una kipaji nayo na hiyo ndiyo inayokufaa. Ukishachagua biashara unayoipenda ni rahisi sana kufanikiwa kwani shughuli utazifanya kwa hiyari bila kujilazimisha. Kama unashindwa kuamua ni biashara gani ufanye, soma sura ya sita katika kitabu hiki. Nimeelezea kuhusu mawazo yanayoweza kukusaidia kuanzisha biashara mbalimbali ambazo unaweza kuzifanya. Kama utakuwa bado hujafikia uamuzi baada ya hapo basi tafuta na wasiliana na washauri ili mbadilishane mawazo na ufundishwe jinsi ya kuamua ufanye biashara gani.
Mambo mengine unayotakiwa kuyafanyia utafiti ni:-
(i) Kujua siri ya bishara unayotaka kufanya ili upate mbinu za kupata mafanikio. Unaweza kupata siri au kujifunza mbinu kutoka kwa watu wanaofanya biashara kama unayotaka kufanya. Suala hili ni gumu sana kwani wafanyabiashara wengi huwa wanaficha siri za biashara zao ili kulinda wasizidiwe maarifa na washindani wao. Unaweza kuipata siri hiyo kama utakwenda kupata ushauri toka kwa mfanyabiashara ambaye yuko mbali na mahali unapofanyia biashara, au tafuta ushauri kwa wataalamu wa mambo ya biashara.
(ii) Fanya utafiti wa soko la bidhaa unazouza au unazotarajia kuuza. Jiulize, je bidhaa unazotaka kuziuza zina soko? Utawauzia watu gani na utauzaje? Kama wewe ni mzalishaji, una mazao / bidhaa unapaswa kuuza kwa jumla, mchanganyiko ama rejareja? Je utatangaza vipi bidhaa zako? Maelezo ya namna ya kutangaza bidhaa zako utayapata katika Sehemu ya Tatu ya Kitabu hiki. Utafiti wa soko unaweza kuufanya kwa kuwauliza wafanya biashara waliotangulia maswali hayo ya utafiti kwani wao wamekuwapo kwenye soko na wanazijua siri za soko.
(iii) Tengeneza bajeti yako kwa kuorodhesha vitu vinavyohitajika na gharama zake ili kuweza kuanzisha biashara yako. Vitu hivyo ni:-
(a) Gharama za Kujenga au kupanga ofisi
(b) Gharama za Leseni ya biashara
(c) Makadirio ya kodi toka TRA
(d) Garama ya vifaa vya ofisi yaani, Samani, makaratasi, mitambo, mashine, nk
(e) Manunuzi ya malighafi au bidhaa za kuanzia biashara
(f) Idadi ya wafanyakazi na gharama za mishahara yao.
(g) Gharama nyinginezo kama vile, umeme, maji, nk.
(iv) Unatakiwa kujua ni mtaji kiasi gani unahitajika kuanzisha biashara yako. Mtaji huo utaujua baada ya kujumlisha gharama zilizoorodheshwa katika kupengele namba (iii)Gharama hizi ni za mwaka ule wa kwanza wa kuanzia
(v) Tafuta Mtaji.
Mtaji unaweza kupatikana kutoka kwenye vyanzo vifuatavyo:-
(a) Akiba au mshahara
(b) Msaada au mkopo kutoka kwa ndugu na jamaa.
(c) Kuingia ubia na mtu mwenye mtaji
(d) Mkopo toka baadhi ya asasi kama vyama vya akiba na mikopo (SACCOS), NGO za kifedha sipokuwa Benki kwani hizi huwa hazitoi mikopo kwa mtu anayeanzisha biashara.
TARATIBU ZA KISHERIA ZA KUFUATA ILI KUANZISHA BIASHARA
Baada ya kufanya utafiti na kupanga mipango ya kuanzisha biashara unatakiwa kwanza kuangalia taratibu za kisheria ambazo unatakiwa kuzifuata na kuzitekeleza. Kama biashara yako ni ndogo anza kama mtu binafsi. Faida ya kuanza biashara kama mtu binafsi ni urahisi wa kuanzisha biashara; urahisi na wepesi wa kutoa maamuzi kwani huhitaji ridhaa ya mtu mwingine kabla ya kutoa uamuzi; mtaji unaohitajika utakuwa mdogo kutokana na gharama za uendeshaji kuwa ndogo, biashara hii inaweza kuendeshwa kwa msaada wa familia kwa kumtumia mke au mume, watoto au ndugu na jamaa na raslimali za familia kama nyumba na samani. Unapoanzisha biashara na kuiendesha mwenyewe unakuwa huru tofauti na mifumo mingine. Matatizo ya kufanya biashara kama mtu binafsi ni:- Kushindwa kupanua biashara yako kwa ufinyu wa mtaji; kufilisiwa mali zako za binafsi iwapo biashara yako itafilisika kwani katika mfumo huu mali ya biashara na mali binafsi si rahisi kuzitenganisha; Kuongeza mtaji inakuwa ni vigumu, hivyo unaweza kushindwa kupanua biashara yako. Ili kuepukana na matatizo niliyoyataja hapo juu unaweza kuungana na watu wengine kufanya biashara kwa ubia. Faida za kufanya biashara kwa ubia ni: Kupata fursa ya kuongeza mtaji kwa kushirikiana na wafanyabiashara wengine ambao wataleta mitaji yao; Kuongeza ujuzi katika shughuli kwa kuleta wataalamu pale taaluma Fulani inapohitajika. Matatizo ya kuendesha biashara kwa njia ya ubia ni: Kufilisiwa mali zako binafsi endapo biashara yako itafilisika; kudhulumiana mali endapo moja wa wabia atakuwa si mwaminifu ambapo anaweza kuingia mikataba mibovu na kusababisha hasara ambayo itabebwa na wabia wote. Ni muhimu kuwachunguza watu tunaotaka kujiunga nao ili tujue kama ni waaminifu. Pia ni vyema kuwapo na mkataba wa maandishi mnapoanzisha biashara ya ubia mkimshirikisha mwanasheria kama shahidi ili kujikinga na kudhulumiana; Kufariki kwa mbia mmoja kunaweza kusababisha kuvunjika kwa ubia; kotokuelewana kwa wabia kunaweza kusababisha kuvunjika kwa ubia. Kama biashara ikikua unaweza kuanzisha kampuni. Mfumo wa uendeshaji wa kampuni unazo faida zifuatazo: unatenganisha majukumu ya wamiliki mali na kampuni yaani kampuni inaposajiliwa inakuwa inakuwa na hadhi na kutambulika kisheria kama ni mfumo tofauti na wamiliki. Mfumo huu unatenganisha majukumu kati ya menejimenti na wamiliki wa kampuni; madeni ya kampuni yatalipwa hadi kufikia kikomo cha mtaji uliowekezwa na wamiliki. Hivyo, mali binafsi za wamiliki wa kampuni haziwezi kukamatwa kufidia madeni ya kampuni endapo kampuni itafilisika. Mfumo wa kampuni unatoa nafasi ya kupanua mtaji kwa kukusanya mitaji kwa kuongeza wanahisa au kupitia soko la mitaji ya hisa. Mfumo huu ndiyo unafaa kwa biashara kubwa kwani unatoa nafasi ya kupanuka kwa biashara na kuendelea kuwapo kwa biashara hata kama baadhi ya wamiliki wake wakifa au kujitoa katika kampuni.
Mambo ya muhimu ya kutekeleza kisheria kabla ya kuanzisha biashara ni:-
(a) Kuwa na ofisi
(b) Kukata leseni
(c) Kusajiliwa na TRA kama mlipokodi na kupewa namba ya mlipakodi
(d) Kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato ya awali
(e) Kutimiza masharti mengine ya keshiria kuwa mfano kama wewe unataka kufanya biashara ya ukandarasi wa ujenzi wa majengo lazima usajiliwe kwenye Bodi ya Wakandarasi.
Kama unafanya biashara ya kati au kubwa unapaswa kufuata sheria. Ni makosa kufanya biashara bila kufuata sheria za nchi. Hata hivyo, kuna biashara zingine ndogo ndogo sana kiasi kwamba uanzishaji wake si rahisi kufuata sheria hizo hapo juu, mfano uuzaji wa maandazi, karanga na vitu vingine vidogovidogo. Hizi zinaitwa biashara zisizo rasmi au biashara ndogondogo. Ni vyema ukachunguza kama biashara unayoifanya ni ndogo au kubwa ili ujue kama unapaswa kufuata taratibu za kisheria au la, kwani kutokujua utaratibu na sheria siyo kinga ya kukufanya usishitakiwe.
CHARLES MSULUZYA NAZI
Mwandishi wa makala hii ni mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Kwa mawasiliano piga simu namba 0755394701 barua pepe cnazi2002@yahoo.com au tembelea tovuti yake www.mshauriwabiashara.com
Mfahamu mwandishi wako wa makala za ujasiriamali
Watu wengi wamekuwa wasomaji wa makala zangu kwa muda mrefu bila kunifahamu, na wengine wamekuwa wakinipongeza kwa kazi nzuri ya makala nilizoandika. Kwa leo ningependa niwaeleze mimi ni nani ili mnifahamu vizuri. Mimi naitwa Charles Paul Msuluzya Nazi ambaye ni mwandishi wa makala za ujasiriamali katika gazeti la Mtanzania kila siku ya jumanne. Nilizaliwa mwaka 1958 huko Mbogwe Wilaya ya Bukombe na nilisoma Shule ya Msingi Mbogwe na baadaye Sekondari Ihungo mwaka 1975 hadi 1978 ambapo baada ya kumaliza kidato cha nne nilijiunga na Chuo cha Ushirika na maendeleo ya jamii Tengeru. Baada ya kumaliza mafunzo niliajiriwa na serikali nikiwa ni Afisa Ushirika msaidizi wilaya ya Mahenge mwaka 1981 hadi 1983 ambapo nilijiunga na Shirika la Masoko Kariakoo nikiwa ni Mkaguzi wa mahesabu ya ndani. Mnamo Mwaka 1988 nilijiunga na Shirika la Umeme TANESCO nikiwa ni Mkaguzi Mwandamizi wa mahesabu ya ndani, ambako ndipo nilipo hadi sasa. Mbali na kufanya kazi za za Mwajiri wangu nimekuwa pia nikijishughulisha na kazi zangu binafsi pamoja na kuhudumia jamii. Miongoni mwa kazi nilizozifanya ni Kuongoza Soko kuu SACCOS nikishika nafasi ya Katibu na Mweka hazina kuanzia mwaka 1985 hadi 1988. Katibu wa TANESCO SACCOS toka 1997 hadi mwaka 2005. Pia mnamo mwaka 2005 na 2010 nilishiriki katika kura za maoni kuomba kugombea Ubunge wilaya ya Bukombe na jimbo la Mbogwe kupitia CCM ambapo sikupata kura za kutosha kuteuliwa kugombea ubunge. Mimi nimeoa na katika familia yetu tumebahatika kupata watoto 5 wa kike 3 na wa kiume 2.
Kuhusu shughuli zangu binafsi Mimi ni mjasiriamali ambaye nimefanya shughuli mbali mbali na kubuni miradi mbali mbali, kwa mfano nimewahi kuanzisha kampuni ya Ujenzi, kiwanda kidogo cha chaki, kuendesha biashara ya mtandao kupitia Makampuni mbali mbali ya kigeni , biashara hizi nimeachana nazo. Sasa hivi najishughulisha na kutoa huduma ya Ushauri wa biashara. Huduma ambazo nazitoa ni; Kutoa ushauri wa biashara kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa, Kuandaa michanganuuo kwa ajili ya kuomba mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili, Kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wafanyabiashara, Kuandaa mifumo ya utunzaji wa mahesabu na kuweka mifumo ya Kompyuta kwenye utunzaji wa hesabu, Kuandaa katiba za vyama na nyaraka za uandikishaji wa makampuni, Kuandaa nyaraka za Tenda, Kutoa ushauri kwa SACCOS ili ziendeshwe kwa ufanisi, Kutoa ushauri kwa Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, Kutoa ushauri nasaha na semina kwa wanafunzi.
Mimi ni mtunzi wa vitabu na nimetunga kitabu cha Ujasiriamali kinachopendwa sana, kiitwacho, Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Kitabu hiki nilikitunga baada ya lengo la kuwafikia wajasiriamali kwa nja ya semina kukwama ambapo nilikuwa nikitoa matangazo kwenye magazeti lakini watu hawafiki. Kitabu hicho kinalenga kumsaidia mtu yeyote ambaye anatafuta utajiri kwa kufanya biashara ndogondogo hadi kubwa. Pia kinatoa maarifa, mbinu na mikakati mbalimbali ya kupambana na umaskini, kinatoa elimu ya biashara na mbinu mbalimbali za namna ya kupata pesa kwa njia halali ili kukurahisishia safari yako ya kuelekea kwenye kutafuta na kupata utajiri. Kitabu hicho kina sehemu mbili, sehemu ya kwanza inaeleza kuhusu taratibu za kuanzisha biashara, sheria, utafiti wa masoko, utunzaji wa hesabu za biashara na utatuzi wa matatizo ya biashara. Sehemu ya pili inaelezea kuhusu mawazo na mbinu mbalimbali za biashara unazoweza kuzifanya na kupata faida na hivyo kutajirika.
Kitabu hicho ni matokeo ya utafiti na uzoefu katika kazi za ukaguzi nilizozifanya kwa kuangalia matatizo ya uendeshaji wa biashara mbalimbali pamoja na ushauri nilioutoa kwa watu walioomba ushauri kutoka kwangu. Kitabu hicho kilichapishwa kwa mara ya kwanza na Business Printers mwezi March mwaka 2008 na mpaka sasa zimechapishwa nakala 4,000 na kuuza nakala 3,000 kwa muda wa miaka 3.Kitabu hicho kiapatikana kwa njia ya Posta au email katika mfumo wa PDF unaweza kunitumia Sh. 5000 kwa MPESA Kwenye simu namba 0755394701 kisha ukanitumia email yako nami nitakutumia kwenye email yako kama kiambatanisho.
Mafanikio yangu ni pamoja na kupata wateja wengi waliopata ushauri wangu na kuufurahia. Pia niliweza kupata wateja wengi walionunua kitabu changu na kukifurahia. Baada ya kuchapisha kitabu nimehojiwa na vyombo mbali mbali vya habari kama vile; ITV, Star TV, TBC 1 TV na TBC1 Radio na Wapo Radio. Hata hivyo kila palipo na mafanikio hapakosi matatizo. Nimekuwa na malengo ya kuwa na kipindi changu cha Ujasiriamali ambacho kimekubalika na vyombo vya habari mbalimbali pamoja na wasikilizaji na watazamaji, lakini nimekosa wadhamimini wa kukidhamini kipindi hiki ambacho kinapendwa sana na wajasiriamali.
Malengo yangu ya baadaye ni kuhakikisha kwamba elimu ya ujasiriamali inaenezwa nchini Tanzania. Pia kuendelea kutoa huduma bora za ushauri kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa,kwa SACCOS na Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi. Ili kutekeleza hayo nitafanya yafuatayo; Kutoa elimu kwa njia ya makala, Radio, Televisheni na semina na Video ya ujasiriamali. Ninao mpango wa kutunga vitabu zaidi katika masuala ya Ujasiriamali saikolojia na ushauri nasaha. Mimi ni mwana harakati wa kupigana vita na umasikini ambaye pia naamini kwamba umasikini hapa Tanzania utatoweka pale ambapo elimu ya ujasiriamali itakapokuwa imeenezwa kila sehemu, kwani watu wengi wanakosa fursa za kiuchumi au kujiingiza katika uwekezaji mbovu kwa kukosa maarifa. Pia naamini katika kutenda. Tatizo la Watanzania wengi ni kuwa na tabia ya kulalamika na kulaumu pale wanapokutana na mtatizo, lakini hawajitumi na wala hawatafuti maarifa na njia za kutatua matatizo.
Nawashauri viongozi wa Serikali pamoja na wadau wengine waweke utaratibu wa kufundisha elimu ya jasiriamali kwa vijana wetu kuanzia Shule za msingi hadi elimu ya juu ili mara wamalizapo shule wawe waajiri kwa kuwa wajasiriamali badala ya kuwa waajiriwa. Pia nashauri Serikali kutilia mkazo elimu ya juu kwa watanzania ili kuwakomboa Watanzania. Nchi zilizokazania elimu kwa watu wake, kama vile India, Japan na China, wamejikuta wakiwainua watu wake ambao walipata ajira nje ya nchi na kuinua uchumi wan chi kwa ujumla. Eneo lingine ambalo ninaloliona kuwa linatakiwa kuangaliwa ni uwezeshaji wa wananchi kwa kupatiwa mitaji. Utaratibu unaoweza kutumika ni kutoa ruzuku si kutoa mikopo kwa wajasiriamali kwani wengi hawana uwezo au ujuzi wa kuizungusha mikopo hiyo na kurejesha. Mbinu nyingine inayoweza kusaidia kuwainua wananchi ni njia ya kuanzisha asasi za wananchi zitakazo wafundisha utaratibu wa kujiwekea akiba na kukopeshana mfano VIKOBA pamoja na SACCOS. Ninaishauri Serikali kuweka mkazo kwenye kilimo hasa cha Mashamba makubwa na kuanzisha viwanda vya kusindika mazao kuyaongezea thamani badala ya kuuza kama malighafi ambapo bei yake ni ndogo. Pia serikali iangalie kuweka utaratibu mzuri wa masoko ya mazao ya wakulima hasa wadogo wadogo ili kuondoa umasikini wa kipato kwani tatizo lao kubwa ni masoko ya kuuzia mazao yao. Wataalamu wa uchumi wameonyesha kwamba nchi zote zilizoweka mkazo kuwekeza katika kilimo uchumi wake uliinuka haraka sana na huwa hauyumbi yumbi.
Ninatoa ushauri kwa wajasiriamali kwamba wakitaka kuanzisha biashara wasikurupuke wafanye utafiti kwanza kuhusu masoko na siri za biashara wanayotaka kuifanya.Wanaweza kufanya utafiti kwa kuwauliza watu waliofanikiwa katika biashara hizo au washauri wa biashara kama mwandishi wa makala za ujasiriamali na mshauri wa biashara. Kwa kuwa tatizo la watu wengi ni mtaji waanze kujenga tabia ya kujiwekea akiba kidogo kidogo na kufanya biashara ambazo zinaanza na mtaji kidogo halafu wapanue biashara kidogo kidogo. Mfano wa biashara ambayo wanaweza kuanza kwa mtaji kidogo ni ya Ufugaji wa kuku wa kienyeji na bustani. Kama wewe ni mjasiriamali mwerevu, ili ufanikiwe unapaswa kutafuta ushauri kutoka kwa wataalamu kwa ajili ya kutatua matatizo yako.
Subscribe to:
Posts (Atom)