Sunday, November 25, 2012

HATUA 10 ZAKUKUWEZESHA KUPANDISHWA CHEO

Hatua 10 za kukuwezesha kupandishwa cheo I Watu wengi hutamani sana kupandishwa vyeo baada ya kuchoka sana na nafasi walizokuwa nazo kwa muda mrefu, au pia wengine wanatamani sana kupandishwa vyeo kwasababu ya kuongeza kipato ili kufikia malengo fulani maishani, kila mmoja ana sababu binafsi ya kuhitaji kupandishwa cheo. Taarifa za kupandishwa cheo ni za kufurahisha kwa kila mmoja wetu, wako ambao kuilazimisha fursa hii hata kwa kwenda kwa waganga, kuhonga, kujipendekeza, kujitoa miili yao na njia nyingine nyingi ili tu kupata cheo. Mara nyingi tumejiuliza kwanini sipandi cheo, wengine wapya wanakuja hapa wanafanya kazi kidogo mara wanapandishwa cheo, wanabadilishiwa ofisi, wanapata gari la ofisi, nyumba, na marupurupu mengine lakini siyo mimi, ukweli ni kwamba sababu kubwa ni sisi wenyewe, vitu vinavyotuangusha na kutufelisha siyo vile vilivyo nje yetu bali vile vilivyo ndani yetu, yaani vilivyo ndani ya uwezo wetu. Leo unaweza kuamua kufanya jitihada binafsi za kujua namna ya kuweza kupandishwa cheo. Yamkini wewe ni mmoja wa hawa ninaowazungumzia hapa ili uweze kujikwamua Jaribu kufuata kanuni hizi rahisi: 1. Jitahidi kujuana na watu Unaweza kufikiri kuwa njia pekee ya kubadilisha mazingira uliyonayo ni kukaa na kuwaza sana, hapana, hii siyo kweli, jaribu kujipenyeza kufahamiana na wengine, usijitenge sana, shiriki maisha yako na wale walioko karibu nawe. Usifikiri kuwa wewe hustahili kujichanganya katika mazungumzo ya kawaida na watu wa ofisini kwako, usifikiri kuongea na bosi wako masuala ya kawaida ni kujipendekeza, kumbuka kwa kuwajua na kujichanganya na wafanyakazi wenzako tunajenga nguvu ya umoja wa kazi, taratibu wote tunakuwa ni timu moja katika utendaji. Pia usibaki umefungiwa katika kiti chako au meza yako ya kazi hata zile nyakati ambazo wengine wanapumzika au kujiburudisha, kama kuna hafla ya ofisi na wenzako wanaenda basi shiriki nao, usifikiri wanapoteza muda, kama mwenzako anatukio fulani la furaha nyumbani basi usiache kushiriki, na kama wewe unatukio kama hilo kwako basi wakaribishe wenzako na usisahau kumualika hata na bosi wako pia. Taratibu unapoanza kumfahamu zaidi bosi wako ni mwelekeo mzuri katika kuelekea mafanikio yako. 2. Usijifanye mkamilifu katika kila kitu Usije ukafikiri kuwa haukuumbiwa kufanya makosa, kufanya kosa kupo katika maisha ya mwanadamu. Kama wewe ni mtu unayefanya kazi sana siyo kitu cha kushangaza sana ukikosea kitu. Ikiwa unatokea kufanya kosa, basi usikae ukijilaumu nakujiuliza kwanini umefanya kosa bali jifunze, pata somo katika kukosea kule na uendelee mbele. Kama utaweka akili yako yote katika kujichunguza kila kitu unachokifanya ili usikosee basi hata basi wako anaweza kufikiri kuwa wewe nikati ya wanaojifanya wakamilifu katika kila wafanyalo na kinyume chake cheo kikaenda kwa wenzako na siyo wewe. Usisahau kuwa waweza kujikuta unafanya vimakosa vingi zaidi wakati unajitahidi kujiweka mkamilifu katika jambo. 3. Kuwa mwaminifu Uaminifu ni kitu kizuri na cha maana sana na kinachowashinda wengi wetu. Wakati wowote unapopata nafasi ya kuongea na bosi wako, kuwa mkweli katika kila neno litokalo kinywani mwako, liwe dogo au kubwa, liwe kuhusu wewe mwenyewe au kuhusu mtu mwingine, kuwa mkweli hata katika yale yanayoonekana kukuathiri wewe, amua kuwa mkweli bila kujali mazingira. Kuwa mkweli katika yale unayoyatamani na katika maswala mazima ya maendeleo ya kazi yako, siyo tu unazungumza kile unachofikiri bosi wako angetamani ukiseme.Staili za kuongea zaweza kutofautiana mtu na mtu lakini ujumbe ubaki kuwa wa kweli. 4. Penda mazingira masafi. Wakati wowote penda kuyaweka mazingira yako ya kazi safi, hatakama ofisi siyo ya kuvutia sana lakini bado unaweza kuvipanga vitu katika meza yako au pale unapofanyia kazi vikawa vema na vyenye mpangilio mzuri. Wengine wamekuwa wakijidanganya kuwa kama wakipoteza muda wao kufanyia usafi eneo lao la kazi basi mabosi wao wataona kuwa hawana kazi za kutosha za kufanya, hii ni kinyume kwa maana hali yako ya ndani ya kiutendaji yaweza kuonekana pale tunapotazama mazingira ya wewe unapofanyia kazi.

No comments:

Post a Comment