Sunday, November 25, 2012

NJIA 10 ZA KUTIMIZA LENGO LAKO MAISHANI

Njia 10 za kutimiza lengo lako maishani Je,unakabiliwa na ugumu katika kutimiza malengo yako kimaisha? Bado hutakiwi kukata tamaa hata kidogo. 1.KUWA MAHUSUSI NA MALENGO YAKO Kwanza kabisa katika kuelekea kutimiza malengo yako, unatakiwa kuwa mahususi na unachokitaka. Lakini pia, ni lazima ujitengee muda maalum wa lini unatakiwa kutimiza lengo hilo. Usijiwekee malengo yasiyo na mipaka katika kuyatizimiza. Vinginevyo utaishia kuwaza kila kukicha. Baada ya hapo, yaandike malengo yako kwenye karatasi, kwa kufanya hivyo kunakusaidia kujiweka karibu na malengo yako. 2.JIKUMBUSHE MARA KWA MARA Hakikisha kuwa kila siku unajikumbusha juu ya majukumu yako katika kutimiza malengo hayo. Weka karatasi hiyo mahali ambapo utakuwa unaiona kwa urahisi kila mara. Mfano, iweke kwenye kioo chumbani mwako kwani ni rahisi kuiona na hali hii itakufanya uzidi kujikumbusha zaidi nini unatakiwa kufanya. Au unaweza kuiweka kwenye meza yako unayofanyia kazi kila mara. Kama nilivyosema hapo awali kuwa, kiini hasa katika kufanya hivi ni kuzidi kujikumbusha juu ya malengo yako kila mara. Ni amini, hufanya kazi. 3. JIHAMASISHE KUCHUKUA HATUA Watu wengi hushindwa kuchukua hatua katika kutimiza ndoto zao kwa sababu hawahamasiki vya kutosha juu ya malengo yao. Tafuta vichocheo madhubuti vitakavyokusaidia kuhamasika na kuchukua hatua za muhimu, ni lazima lengo litimie. Kwa mfano, labda lengo lako ni kuacha uvutaji wa sigara na binti yako ndiye hamasa kubwa katika hili, mfikirie kila unapokuwa unataka kuvuta. 4. JIADHIBU UNAPOSHINDWA, NA JIPONGEZE UNAPOFAULU Kila unaposhindwa kuchukua hatua, basi unapaswa kujiadhibu na jipongeze unapofanikiwa kutimiza kile ulichojipangia.Hakikisha kuwa kila lengo unalojiwekea ni lazima uwe na mikakati ya kulitimiza. Kwa upande mwingine, unaweza kujiadhibu kwa kuchelewa hata kulala kama hujatimiza lengo la siku hiyo. Katika kufanya hivyo utajiwekea mazoea akilini na mwilini kufanya kazi kutokana na jinsi ulivyolenga au kupanga. 5. JIONE KAMA UMETIMIZA LENGO LAKO Hakikisha kila siku unatumia angalau dakika 15 kufikiri akilini mwako katika mfumo chanya kuwa umeshalitimiza lengo lako. Hili ni zoezi la muhimu sana katika kuelekea kutimiza malengo yako. Kujiweka kama umeshatimiza Malengo yako akilini mwako, utakuwa unazidi kujihamasisha na utakuwa unafikisha ujumbe kwenye ulimwengu wa mafanikio kile unachokitaka maishani. Watu waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali kimaisha, hufanya hivi kila mara, hutimiza malengo yao akilini kabla ya uhalisia. Hii ni kanuni ya kitaalamu. 6. CHUKUA ANGALAU HATUA 1 AU 3 KILA SIKU Inashauriwa kuwa, unapaswa kuchukua angalau hatua moja au tatu kila siku zitakazo kuwezesha kutimiza malengo yako. Hakuna kitakachotokea kwako kama hutachukua hatua yoyote. Hapa naomba nieleweke kuwa, hata kama utatumia muda mwingi kiasi gani kuangalia hiyo karatasi yenye malengo yako kila siku, lakini kama hauchukui hatua yoyote hakuna kitakachotokea. Kwa hiyo chukua angalau hatua moja au tatu zitakazo kupeleka katika malengo yako kila siku. 7. JIZATITI KWA WENGINE Jaribu kuwaambia baadhi ya watu wako muhimu juu ya malengo yako. KWANZA kabisa kama ilivyoada nimshukuru Mungu kwa kuweza kunipa nguvu ya kuandika haya nitakayoandika leo na pia kumuomba atuzidishie amani yetu hapa nchini. Bado tunaendelea na mada yetu ambayo tuliianza wiki iliyopita na hapa tunahitimisha kwa hoja zilishoshiba. Kabla ya kuendelea na makala yetu, naomba nieleze jambo moja muhimu sana maishani. Unapokuwa katika harakati za kutimiza ndoto zako, basi vikwazo na vizingiti vingi sana vitaibuka kwa lengo la kukukatisha tamaa, hata siku moja acha kabisa tabia ya kukata tamaa. Siku zote maisha ni magumu hivyo ni lazima upambane nayo kwa silaha ya uvumilivu. Na vikwazo visikuzuie kusonga mbele. Sasa tuendelee na vipengele vilivyosali. 7. JIZATITI KWA WENGINE. Jaribu kuwaambia baadhi ya watu wako muhimu juu ya malengo yako. Uko siriazi katika kutimiza malengo yako? Kama ni kweli, jizatiti juu ya malengo hayo. Mwambie kila mtu juu ya kile unachotaka kukitimiza maishani mako. Mwambie mke wako juu ya malengo yako, waambie wazazi wako, waambie rafiki na jamaa zako juu ya malengo yako na lini hasa unapanga kuyatimiza. Ukifanya hivi, utakuwa huna jinsi zaidi ya kutimiza malengo yako, maana umewaabia watu wa muhimu sana hivyo kushindwa kwako kutimiza malengo hayo, ni sawa na kujiletea aibu kubwa. Hivyo utachukua hatua siriazi na kujiletea matokeo halisi. Lakini naomba nitoe angalizo kuwa, simaanishi kwenda mitaani na kuanza kuwatangazia watu wote, namaanisha watu muhimu tu. 8. PIMA MATOKEO YAKE Pima na jiwekee muono juu ya matokeo yako. Kamwe huwezi kujua kama unavuka hatua kuelekea kwenye lengo lako kama hupimi matokeo ya kile unachokifanya kila siku katika utendaji wako wa kazi. Kama ukigundua kuwa hauzalishi matokeo unayoyataka, basi huenda huchukui hatua za kutosha, au mikakati unayoitumia siyo sahihi. Hivyo unapaswa kubadili mikakati katika kujipatia matokeo unayoyataka. Kama unazalisha matokeo unayoyataka, basi hongera. Chukua hatua zaidi ili ujipatie matokeo zaidi. 9. KUWA NA SABABU. Ni lazima uwe na sababu za kwa nini unataka kutimiza lengo hilo maishani mwako. Ukiwa na lengo lisilo kuwa na sababu mara nyingi huwa ni vigumu kulitimiza maana hakuna kitu kinachokusukuma katika kufanya hivyo. Hakikisha unajikumbusha kila mara akilini mwako kuwa ni kwanini unataka kutimiza hilo lengo maishani mwako. Sababu yako yakinifu ndani ya moyo ni chanzo cha hamasa. Mara zote kumbuka hili. 10.JIKUMBUSHE YA JUU. Ni muhimu sana kujikumbusha yote uliyoyasoma hapo juu. Utafiti umaonesha kuwa ukitaka tabia fulani ijekengeke, ni lazima uifanyie mazoezi kila siku ipitayo angalau ndani ya siku 21mfululizo. Japo siyo rahisi mwanzoni. Ni kama tu kuhamia mazingira mapya, unaweza kujisikia ugumu kidogo, lakini muda si mrefu utazoea maana akili yako itakuwa imejikita huko. Ni sawa na hapa. Fanyia mazoezi tabia njema kila siku kwa muda wa siku 21 na tabia hiyo itakuwa yako milele. Watu wengi huwa hawajiulizi ni kwa jinsi gani husugua meno yao kila asubuhi. Unajua ni kwa jinsi gani unasugua meno yako kila asubuhi? Bila shaka ni vilevile kama kawaida. Hivyo ndivyo ninavyomaanisha kitabia. Unapoanzisha tabia mpya, utafanya mambo vilevile kila siku. Kwa kufuata njia zote kumi nilizozianisha hapa chini, naamini kwa nguvu zote kuwa kutimiza malengo yako haitakuwa tatizo tena. Fanya hivyo kwa dhati na utaona matokeo ya kushangaza. Naomba niishie hapa kwa leo. ZINGATIA HAYA. Katika maisha, hakuna kinachoshindikina kama kweli utaamua kwa dhati kukipata. Kinachochangia watu wengi kutotimiza kile wanachokitaka maishani, ni kutodhamiria kwa nia na nguvu zote kufuatilia malengo yao. Lakini pia woga huchangia kwa kiasi kikubwa sana. Kabiliana na hofu. Tunapokuwa waoga, huwa tuna sizi kiakili, kimwili na kihisia na hushindwa kabisa kuchukua hatua.

No comments:

Post a Comment